Watanzania na ustaarabu wa chooni...

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Kwanini lalkini?? Ustaarabu wa matumizi ya toilet kwa watz na hata waafrika wengine ni "0"
Je ni tamaduni zetu mbovu au?
Ukiacha public toilets ambazo huwa nI chafu karibu mara zote ukiacha
mahoteli makubwa ( huwa yana wasafishaji stand-by)..hata majumbani mwa baadhi ya watu utashangaa
uchafu ulivyozagaa...mimajimaji chepechepeeeeeee!! Hata maofisini! Miaka ya nyuma kidogo nakumbuka
ukiingia "Hazina" -yaani Wizara ya fedha kilichokua kinakupokea kuanzia mlangoni ni harufu mbaya ya choo!
Bora siku hizi kuna makampuni ya usafishaji yanafanya kazi nzuri lol!
Uswazi watu hufanya mambo yao kwenye mifuko ya "rambo" AU MAGAZETI na kutupa
barabarani usiku!
Binafsi kuna watu wakija nyumbani kwangu napata mashaka sana wakitaka kutumia
toilet!NAKWAZIKA LOL!

Sasa kuna wazo hapa..........nani alishajikuta yuko katikati ya mji au hata nje ya mji na anahitaji kutumia
toilet for short or long call........... utaenda vichakani au utafanyaje? Hata kama kuna choo cha umma au hata
cha "kulipia" sh 100-200/= unaweza ukapata homa ghafla utakapojaribu kuingia humo.
Nafikiria mobile/taxi toilets as an ideal business.... hahahah sipati picha itakavyokuwa .....
 
Tausi Mzalendo wewe km mimi, huwa napata shida saaana nikiwa kazini. yaani atleast haya makampuni ya usafi yanasaidia ila wale wafanyakazi wake wanalalamika mnooo. utasikia yule jamaa akiingia chooni km bata anasambaza uharo choo chote. au utasikia yule dada usistaduu wa nguoni akiingia chooni hata juu ya sink anaweza akayaachia hapo khaaaa. kwa kweli wa TZ kwenye matumizi ya vyoo bure kabisa, mtu analundika mzigo wake akimaliza hata ku flash hawezi. wanaume kwenye vile vyoo vya haja ndogo kmcvya mlimani city, utakuta mtu katupia toilet paper mlee kasababisha matundu yameziba. ma SINK sasa mtu anakuja katoka kula huko utasikia jinsi anavyovuta makoozi kwaaaaaaa kwaaaaa anatema kwenye sink halafu anaacha hivyo hivyo analala mbele. wa bongo tuwe wastaarab basi
 
Miye nakumbuka yalipokuja haya ma 'urinals' mtu mmoja alikaa akafanya biashara yake kubwa pale pale!
 
Chimunguru..yaani! Umenikumbusha kitu...
Kuna wadada walikuwa wanajishebadua mtaani kwetu kumbe usiku wanatumia magazeti na kuyalundika ndani mwao.
Yakishajaa mzigo wa kutosha..basi wanapakulia barabarani usiku.
Usione mtu mrembo au mtanashati.....
 
Tausi,hilo sio suala la rangi au taifa,hebu jaribu kujiuliza hata kidogo ustaarabu unahusiana nini na rangi/utaifa?Hakuna mahusiano hata kidogo,hayo yanatokana na malezi,katika maeneo yote duniani,kwenye public toilets na vichochoroni ambako hakuna anaesimamia usafi pote ni pachafu kwa namna inayofanana.Ni kwa sababu wote ni wanadamu tu!
 
Tatizo kubwa ni kwenye highways. Hakuna toilets za public. Sasa huko msituni ukikutana na za mwenzio sijui inakuaje! Ila nadhani this is got something to do with the texture of our skin
 
Tausi,hilo sio suala la rangi au taifa,hebu jaribu kujiuliza hata kidogo ustaarabu unahusiana nini na rangi/utaifa?Hakuna mahusiano hata kidogo,hayo yanatokana na malezi,katika maeneo yote duniani,kwenye public toilets na vichochoroni ambako hakuna anaesimamia usafi pote ni pachafu kwa namna inayofanana.Ni kwa sababu wote ni wanadamu tu!

Cjui kama umenisoma mpendwa! Sijazungumzia rangi au utaifa..nisome tena vizuri unifahamu.Ukija kwenye public toilets ulimwenguni ni kweli zinakuwa chafu - KAMA HAZINA USIMAMIZI.
Je inakuwaje kwenye nyumba za baadhi ya watu tena wasomi wenye vyeo vyao huwezi kuthubutu kuingia vyooni mwao!
 
Tausi, naona una kumbukumbu kama za samaki,hebu soma paragraph ya kwanza mpaka kwenye "0"uone ulichoandika.Ndo maana nikakuambia suala sio uafrika wala utaifa ni malezi!
 
Tausi, naona una kumbukumbu kama za samaki,hebu soma paragraph ya kwanza mpaka kwenye "0"uone ulichoandika.Ndo maana nikakuambia suala sio uafrika wala utaifa ni malezi!

Talking of kumbukumbu za "nzi" mpenda uchafu! .....Sikujua kama "UAFRIKA"( ndicho nilichoandika) ni rangi au/na taifa lol!
Waafrica - ni watu wanaoishi kwenye bara la Africa - wanaweza kuwa wa rangi mbalimbali au mataifa mbali....prove me wrong!
Kwamba ni malezi uko sahihi ..lakini hayo malezi yanakuwajekuwaje hadi tujikute kwenye hal ya kutokuwa na adabu za matumizi ya vyooni? Labda ungeanzia hapo
 
Kwanini lalkini?? Ustaarabu wa matumizi ya toilet kwa watz na hata waafrika wengine ni "0"
Je ni tamaduni zetu mbovu au?
Ukiacha public toilets ambazo huwa nI chafu karibu mara zote ukiacha
mahoteli makubwa ( huwa yana wasafishaji stand-by)..hata majumbani mwa baadhi ya watu utashangaa
uchafu ulivyozagaa...mimajimaji chepechepeeeeeee!! Hata maofisini! Miaka ya nyuma kidogo nakumbuka
ukiingia "Hazina" -yaani Wizara ya fedha kilichokua kinakupokea kuanzia mlangoni ni harufu mbaya ya choo!
Bora siku hizi kuna makampuni ya usafishaji yanafanya kazi nzuri lol!
Uswazi watu hufanya mambo yao kwenye mifuko ya "rambo" AU MAGAZETI na kutupa
barabarani usiku!
Binafsi kuna watu wakija nyumbani kwangu napata mashaka sana wakitaka kutumia
toilet!NAKWAZIKA LOL!

Sasa kuna wazo hapa..........nani alishajikuta yuko katikati ya mji au hata nje ya mji na anahitaji kutumia
toilet for short or long call........... utaenda vichakani au utafanyaje? Hata kama kuna choo cha umma au hata
cha "kulipia" sh 100-200/= unaweza ukapata homa ghafla utakapojaribu kuingia humo.
Nafikiria mobile/taxi toilets as an ideal business.... hahahah sipati picha itakavyokuwa .....

Hata hizo mobile toilets watazichafua tu. Inabidi awepo mtu wa kuwaelimisha watumiaji kabla hawajaingia na kusafisha mara baada ya mtumiaji kutoka. Mimi nadhani hii inatokana na malezi yetu tangu tukiwa wadogo. Na kwa bahati mbaya majumbani mwetu suala la kutunza mazingira ya chooni huwa halipewi msisitizo unaostahili.

Mfano mtu ambaye amekulia kwenye mazingira ya choo cha shimo au yule wa kijini anayekwenda porini mara anapopata haja anaweza asiwe mtumiaji mzuri wa choo cha kuflash kwani kwenye choo cha shimo au porini ukishamaliza shughuli kinachofuata ni kuinuka na kuendelea na shughuli nyingine. Inabidi kwanza mtu huyo aelimishwe umuhimu wa usafi na jinsi ya kutumia choo cha kukaa na kuflash. Hata huko kwenye choo cha shimo ukiingia inabidi usishike kuta hovyo, jaribu kwanza kuangalia kwenye pembe za kuta kwani unaweza kukuta watu wamepageuza kuwa ndio toilet paper.
 
Tausi mpendwa,

Leo umeamkia ubavu gani? Au ulibanwa ukakutana na ya kukutana?

Yaani hii sredi imenifanya nipate kichefuchefu........khaa!

We babu...halafu hiyo signature yako......
umepata kichefuchefu kwanini lakini? Au umekumbuka kitu/tukio baya?
 
halafu kuna wale wanamwagia maji bafuni yaani ukiingia maji ni kila mahali utadhani unaenda bwawani.. kwanini vyoo vingi haviwekwi amenities muhimu za kufanya iwe ni sehemu ya starehe?
 
We babu...halafu hiyo signature yako......
umepata kichefuchefu kwanini lakini? Au umekumbuka kitu/tukio baya?
Hahahahahaha!
Ilikuwa stand ya mabasi Moshi enzi hizo. Nimebanwa na kimba nataka nikakate gogo.......... kuingia msala hamu ya kuachia kinyesi ikaisha ghafla!

Afu ndo nini kuchungulia uvunguni mwa babu?
 
Talking of kumbukumbu za "nzi" mpenda uchafu! .....Sikujua kama "UAFRIKA"( ndicho nilichoandika) ni rangi au/na taifa lol!
Waafrica - ni watu wanaoishi kwenye bara la Africa - wanaweza kuwa wa rangi mbalimbali au mataifa mbali....prove me wrong!
Kwamba ni malezi uko sahihi ..lakini hayo malezi yanakuwajekuwaje hadi tujikute kwenye hal ya kutokuwa na adabu za matumizi ya vyooni? Labda ungeanzia hapo

Kwa mwafrika choo ni mahali pa mwisho anapohitaji kuwepo ama kwenda. Ukirudi nyuma zaidi kwenye historia waafrika hatukuwa na utamaduni wa kujenga vyoo kwani mahitaji yote yalimalizikia porini. Na mpaka sasa kuna jamii ambazo bado hawajengi vyoo hata hivi vya shimo. Hivyo kwa mwafrika choo ni kitu kipya na ndiyo maana ukienda kwenye nyumba nyingi vyoo vinajengwa mbali sana na nyumba ili kuepuka harufu mbaya inayoambatana na uwepo wake. Ukifikiria choo kwa mwafrika unakumbuka harufu mbaya, uchafu na mara zote ni sehemu ambayo unatakiwa kutumia muda mfupi iwezekanavyo ili kuondoka.

Hata kwa wale ambao wanaishi mijini na hasa waliopanga kwenye nyumba za uswahilini ambapo watu kadhaa wanatumia choo kimoja bado vyoo vinabeba taswira ileile ya sehemu chafu ambayo kama ungepewa uchaguzi usingekuwa unaenda kabisa. Kwa bahati mbaya hata mashule tunayosoma bado vyoo havijapewa umuhimu unaotarajiwa.

Ukitembelea shule za msingi, sekondari na hata vyuoni ambapo ndio tabia za usafi zinajengwa bado kuna tatizo kubwa la uchafu uliokithiri wa vyoo. Wakati ninasoma shule ya msingi na hata sekondari kusafisha choo ilikuwa ni adhabu kubwa na walimu walikuwa wakiitumia kwa watoto wakorofi. Sasa unatarajia mtu ambaye amezaliwa na kukulia kwenye mazingira ya vyoo kuwa vichafu na ambaye amelelewa kuamini kuwa kusafisha choo ni adhabu anaweza kweli kubadilika tu ghafla na kuwa msafi anapoanza kazi? Hata wale waliopewa kazi ya kusafisha choo bado wameathirika na utamaduni uleule wa kuona choo kuwa ni mahali pachafu.
 
halafu kuna wale wanamwagia maji bafuni yaani ukiingia maji ni kila mahali utadhani unaenda bwawani.. kwanini vyoo vingi haviwekwi amenities muhimu za kufanya iwe ni sehemu ya starehe?
Si uitani mzee mwenzangu.......

Hakuna starehe tamu kama kuachia kimba katika choo kisafi......... Ukigongewa hodi huwezi kuitika karibu......
 
halafu kuna wale wanamwagia maji bafuni yaani ukiingia maji ni kila mahali utadhani unaenda bwawani.. kwanini vyoo vingi haviwekwi amenities muhimu za kufanya iwe ni sehemu ya starehe?

Hili nalo neno!
Maji chepechepe........ haya nayo huzidi kuchafua choo...
Sehemu nyingine utakuta wameweka vyoo ya kuchuchumaa (Asian type) na vya kukaa ( European type) hakuna "African type' lol...cha ajabu mtu mwenye kupenda majimaji hatumii cha kuchuchumaa, bado anakimbilia cha kuketi na bado anamwaga maji? Kwanini lakini?
 
Talking of kumbukumbu za "nzi" mpenda uchafu! .....Sikujua kama "UAFRIKA"( ndicho nilichoandika) ni rangi au/na taifa lol!
Waafrica - ni watu wanaoishi kwenye bara la Africa - wanaweza kuwa wa rangi mbalimbali au mataifa mbali....prove me wrong!
Kwamba ni malezi uko sahihi ..lakini hayo malezi yanakuwajekuwaje hadi tujikute kwenye hal ya kutokuwa na adabu za matumizi ya vyooni? Labda ungeanzia hapo

let me ask u,unaposema Africa whats kind of people are u "represent"?
 
Back
Top Bottom