Watanzania Na Ugonjwa Wa Kulalamika Bila Kufanya Maamuzi

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Watanzania ni watu wa ajabu sana.Wanapenda mabadiliko Lakini hawataki kubadilika.Wamekuwa na sifa ya kulalamika tu pasi kujuwa tatizo la malalamiko yao
Mtakumbuka utawala wa Nyerere mwishoni kabisa tulimchoka.
Akaja mzee Mwinyi ndo usiseme. Kaingia Mkapa pia pale mwishoni tulilalamika sana.
Kachukua Kikwete naye hivyo hivyo mwanzo tulimsifu sasa hivi malalamiko chungu nzima.
UKAWA wamekuwa wakisema mara zote,Tatizo sio mtu ni mfumo,Na bila kuuvunja mfumo huo.Tutaendelea kulalamika siku zote huku tukidanganywa tupo kwenye mabadiliko.
Sasa tunae Magufuli,Sintoshangaa ifikapo 2019 yakajirudia yale yale ya kulalamika"Tukisahau sifa tunazomwagia sasa"Tena tunalalamika na siku ya kura tunarejesha mfumo ule ule wa kiCcm tukitarajia mabadiliko.
Sasa najiuliza huu ni Ugonjwa?Na kama ni ugonjwa wa watz ipi dawa sahihi ya gonjwa hili"Gonjwa la Kulalamika"
 
Last edited:
Taifa limejengwa kuwa na uoga.

Kizazi cha 70 rudi nyuma ni majipu makubwa,
Kizazi cha kulia lia tu,Tuna hulka ya kusifia jambo na baadae tunalia tena juu ya jambo hilo hilo
 
Hata ukiamua kwenda kushtaki hakuna pakushtakia. Hata ukiwa na ya kusema hakuna pakusemea. Hata ukiwa na taarifa zato hakuwa wa kuzifanyia kazi na kutetea. Ukisema ukweli wewe ni adui, ukisifu maovu wewe ndiyo kichwa. Tatizo ni mfumo.
 
UKAWA wamekuwa wakisema mara zote,Tatizo sio mtu ni mfumo,Na bila kuuvunja mfumo huo.Tutaendelea kulalamika siku zote huku tukidanganywa tupo kwenye mabadiliko.

Mfumo ndio lidudu gani?

UKAWA ni sehemu ya wafanya maamuzi katika halmashauri kadhaa, sijajua mabadiliko ni nini kwa tafsiri yako.
 
Mfumo ndio lidudu gani?

UKAWA ni sehemu ya wafanya maamuzi katika halmashauri kadhaa, sijajua mabadiliko ni nini kwa tafsiri yako.
Halimashauri zote ambazo upinzani wamekuwa wafanya maamuzi zimebadilika.Na kama nyie vidume kweli mbona mnang'ang'ania ilala na kinondoni?Mnashindana na number.Ovyo kabisa
 
Halimashauri zote ambazo upinzani wamekuwa wafanya maamuzi zimebadilika.Na kama nyie vidume kweli mbona mnang'ang'ania ilala na kinondoni?Mnashindana na number.Ovyo kabisa
Us against all mentality.

Hayo ndio mabadiliko mkuu, kama zimebadilika hizo na hizi za sasa zitabadilika ndio mwanzo wa nchi kubadilika. Hakuna mazingaombwe
 
Back
Top Bottom