EMT
Platinum Member
- Jan 13, 2010
- 14,477
- 15,347
Mara kwanza nilitonywa kuhusiana na kushamiri kwa biashara ya ukahaba inayofanywa na Watanzania nchini China. Sikuchukulia seriously juu ya hili suala, lakini inaonekana kweli lisemwalo limo. Lakini bado najiuliza inawezekanaje Watanzania 40 kukutwa katika hoteli moja nchini China kwa wakati mmoja huku kila mmoja akiwa na mitikasi yake Halafu kati yao, 38 ni wanawake. Kwani kuna mkutano mwingine wa wanawake Beijing huko China?
Hii imetokea huko Macau nchini China ambapo polisi wamewakamata makahaba wa Kitanzania baada ya kutonywa kuwa kulikuwa na makahaba waliokuwa wakifanya biashara za kuuza miili yao kwenye hoteli moja iliyopo mji wa Central District. Baada ya kuwakamata makahaba wanne wa Kitanzania, polisi walianzisha msako hotelini hapo ambapo walikuta wanawake wengine 38 na wanaume wawili ndani ya vyumba vitano vya hoteli hiyo. Ajabu wote walikuwa ni raia wa Tanzania wenye umri kati ya miaka 19 na 38.
Hata hivyo, wengi wa Watanzania hao walikanusha kujihusisha na ukahaba. Wengi wao walidai kuwa walikuwa wanasubiri kuingia China au kurudi nyumbani Tanzania. Hata hivyo, kulikuwa na mwanamke mmoja wa Kitanzania ambaye aliiambia polisi kuwa alilazimishwa kufanya biashara ya ukahaba nchini China. Mwamanke huyo alidai kuwa alipewa ofa ya kufanya kazi kama mchuuzi jijini Guangzhou lakini baadae alilazimishwa kuwa kahaba. Kipato chake chote cha ukahaba kilikuwa kinachukuliwa na mwanamke mwingine. Amedai kuwa alienda Macau kwa ajili ya kuongeza visa yke.
Mwanamke huyo aliendelea kuimambia polisi kuwa Aprili 3 mwaka huu aliwambia wengine hakutaka kuendelea kuwa kahaba na kuwa alitaka kurudi nyumbani lakini akakamatwa chumbani kwake na kupigwa. Baadae polisi walimkamata mwanamke anayedaiwa kuchukua kipato chake chote na kumkuta akiwa na aina mbili za nyaraka zinazoonyesha dalili za kufanya biashara ya ukahaba. Nyaraka ya tatu ilikutwa mikononi mwa mwanamke mwingine.
[video=youtube_share;ANkRsmQcxBA]http://youtu.be/ANkRsmQcxBA[/video]