watanzania na abusive culture

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,108
115,842
Kuna kitu kuhusu sisi watanzania,ambacho kwa maoni yangu kinaweza kuwa ni tatizo kubwa kuliko ufisadi,kwa mtazamo wangu hiki kitu kimechangia kuzaliwa kwa ufsadi,hiki kiti ni abusive culture ambayo watanzania wengi tunayo na hatujui kuwa ni tatizo kubwa,
kutokana na hii abusive culture tuliyonayo,kwanza utaona karibu kila mtu
huwa tunapenda kumkashifu na kum abuse hata bila sababu za maana,kwa tanzania mtu kuwa maarufu ni kama laana fulani hivi,kabla hata ze comedy hawajaanzisha kipindi cha alie fulia,tayari watu walikuwa wanapata tabu ya kukashifiwa mitaani,
moja yA sababu ni mtazamo potofu wa maana hasa ya umasikini,
wengine wanaona mtu kutokuwa na gari ndo umasikini,
na hata kama mtu ni masikini je ni halali mtu huyo kukashifiwa?????
anyway najaribu kusema kuwa sisi kama watanzania tuna tatizo la kutojithamini na kutojua thamani hasa ya watanzania wenzetu ndo maana
kuna watu huwa wanafikiri ili mtanzania awe na thamani ni lazima awe na hali fulani,misamiati kama kajambanani,wavuja jasho,au walalahoi imekuwa kawaida kumaanisha watu wa chini,as if watu wakiwa na kipato cha chini
wanakuwa na thamani pungufu hivi,mentality ya watanzania wengi
ni kuwa mtu mtu hawezi kujiona ni noble mbele za watu kama ni mlalahoi...
utawasikia watu wakiambiana kwenye daladala kuwa kama unataka heshima kapande taxi,as if mtu anakuwa si mtu kwa kuwa anapanda daladala,huo ni mfano mmoja tu,but mifani ni mingi sana......
hata mapenzi yetu yanatawaliwa na kuthamini vitu zaidi kuliko
chochote,watu washenzi wenye pesa huabudiwa,na watu wa maana wasio na kitu hukashifiwa,
chanzo cha yote hayo inferior complex inayowasumbua watanzania wengi sana,
wengi wetu hatujichukulii kuwa ni watu noble na wanapaswa kuwa treated with respect regardless hata kama ni watu masikini,
na madhara ya kuishi kwenye abusive culture ni makubwa sana,kubwa zaidi tunajikuta tunatengeneza cycle ya kufeli kila mara kwenye kila kitu
iwe politics au michezo au chochote kile,ukitazama tanthilia za tv utaona zote zinashabikia kudhalilishana na kushambuliana,
ukija kwenye muziki kwa mfani taarabu ndo kabisa
ni abusive culture hundred percent,kwa ujumla ile ambayo tunaweza
kuiita ni tanzania pop culture ni culture ambayo ina promoti watu kudhalilishana na kuzodoana as if watu wote tunapaswa kuwa na
hali fulani ya kufanana,
ndio maana ze comedy walipoanzisha kipengele cha aliefulia,
kipengele hiko kimekuwa maarufu sana,
ni kwa sababu deep ndani ya mioyo yetu tuapata faraja watu wengine
ambao ni watanzania wenzetu wakidhalilishwa,hata kama hatuwezi kusema
hadharani au tunajifanya hatupendi,
ni tatizo lililo ndani ya saikolojia yetu,since we feel we are not something
it feel beter if someone else is being told he is no body.
ni tatizo la self esteem i guess but ni widespread.
tatizo hili la watanzani unaliona kila sehemu hata humu ndani naliona.
 
Unayoyasema yana maana ila sasa mtiririko ndugu yangu, next time una post tumia para na acha space kati ya para na para. Otherwise inatia uvivu kusoma. All in all umegonga penyewe, tuna matatizo makubwa ya kifkra (sisi kama Watanzania). Na hili ni tatizo la kijamii linalohitaji tiba ya kijamii. Priorities za wengi wetu za ajabu sana, viongozi wanaopaswa kuonyesha mfano ndio usiseme, sasa wananchi wa kawaida huku chini ni reflection ya kile kilicho juu (viongozi). Pole pole tukianza kuzinduka toka usingizi huu na kujihoji kibinafsi, labda tutafika. Nasisitiza labda!
 
Haya mambo tumerithishwa na wakoloni na wahindi. Inabidi juhudi zifanyike na kila mtu hasa wale ambao tumesoma zaidi tuwasaidie wenzetu kwa kujirudisha chini kuwa sawa na wengine kwani matatizo haya yana anzishwa na wasomi na wafanya biashara wa kigeni.Sisi wasomi tukijiweka sawa na wenzetu tukajiona tuna haki sawa haya matatizo yataisha. Mtu asemaye kuwa na gari ndo utajiri, hawa ndo bado wana mawazo ya kikoloni, gari ni kitendea kazi kama jembe au baiskeli.
 
Mada nzuri sana: Culture yetu WTZ inaenda pabaya kwa kweli. Ni kweli ilianzishwa na Wakoloni - kuleta UTWANA na UTUMWA - na inasikitisha kwamba imeingia hadi kwenye VICHWA VYETU -

1. Maofisini - hapo ndio usiseme - mtu akiwa na cheo - basi anataka aabudiwe - ofisini BOSS ANAKOROGEWA CHAI (kwani ofisini kuna mke wake??) - HATA KUBEBA DOCUMENT - eti hawezi hadi abebewe

2. Njoo kwenye barabara - UMATI WA WATU KWENYE DALADALA, PRIVATE CARS - watasubirishwa masaa mengi mno - ETI MKUBWA ANAPITA - kwanini asijipange - akapita faster?? foleni inawekwa hadi akiwa bafuni anaoga hadi ale, amalize, BADO WTZ wamesimamishwa

3. Njoo kwenye entertainments - e.g. COMEDY - hivi kipindi cha ALIYEFULIA - kina maana gani??? yaani unamchukua mtu ambaye amepatwa na matatizo kwenye maisha ambayo ni safari ndefu - unaanza kumcheka eti AMEFULIA - mimi sielewi kinafundisha nini kipindi hicho

4. Njoo kwenye MAHUSIANO - familia inaweza kumkataza Kijana/Binti asifunge ndoa na mtu aliyempenda kisa - FAMILIA YA KIMASKINI - ama kweli

SASA KAMA UNAONA UKO JUU - SI UNATAKIWA KUSAIDIA WALIO CHINI??? THANK GOD SUPERMARKETS, SOKONI TUNAENDA PAMOJA - na unanua kadri unavyoweza!!

UKWELI NI KUWA SIO WATANZANIA WOTE WAMEHARIBIKIWA AU WANAYO ABUSIVVE CULTURE - ILA TUFIKIRIE CHA KUFANYA KWANI INAKWENDA KASI SANA
MUNGU TUSAIDIE!!!
 
Sababu mojawapo kubwa inayochangia tabia hii ni mmomomyoko wa maadili kiujumla haswa kupitia popular culture kama muziki, internet, vitabu, sinema etc. pamoja na mila na maadili ya Kizungu kama materialism and individuality.

Lakini mchanganyiko mkubwa na kiwango kikubwa cha tofauti baina ya watu katika jamii yaani heterogeneity (matabaka ya kiuchumi, kidini, kikabila, rangi, kielimu, nk) nayo inachangia kwa vile inapunguza sense of altruism kati ya Wanajamii.
 
Last edited:
unayoyasema yana maana ila sasa mtiririko ndugu yangu, next time una post tumia para na acha space kati ya para na para. Otherwise inatia uvivu kusoma. All in all umegonga penyewe, tuna matatizo makubwa ya kifkra (sisi kama watanzania). Na hili ni tatizo la kijamii linalohitaji tiba ya kijamii. Priorities za wengi wetu za ajabu sana, viongozi wanaopaswa kuonyesha mfano ndio usiseme, sasa wananchi wa kawaida huku chini ni reflection ya kile kilicho juu (viongozi). Pole pole tukianza kuzinduka toka usingizi huu na kujihoji kibinafsi, labda tutafika. Nasisitiza labda!

thanx.next time nitafanmya hivyo
 
Hii yote sababu ya Kanumba!

Amani na wewe sasa unatuangusha sasa hatujuhi unasupport hii mada au ndio unaponda , maana mtoa mada kaongelea hizo habari za kupondana sasa wewe unatuletea KANUMBA, haya ebu tuambie bac kanumba nae anahusika vipi humu, au na wewe ndio walewale
 
Wa-TZ hatupendi wenzetu wafanikiwe kiasi cha kutuzidi.Tuna wivu sana wa mafanikio ya wenzetu, ndio maana mtu akipata matatizo tunashangilia badala ya kumsaidia asiaibike.
 
Viongozi wetu wa dini wangetoa waraka kuhusu tabia kama hizi pia..! kwasababu huu nao ni ufisadi wa kifikra!
 
Back
Top Bottom