Watanzania hatumtendei haki Vanessa Mdee

'''Naomba unirogee''' song la kiswaz kabisa
song la kiswazi lililojaa pozi za kibeyonce......muziki unataka timing.cheki snura hit moja tu la chura sasa hivi anazunguka nchi nzima kupiga show japo ni za buku tano tano kiingilio but si haba teh teh teh
 
Kinachomfelisha ni uzungu tu hakuna kingine, hakuna msanii aliyewahi kutoboa bongo kwa swaga za kizungu, lazima ajue anadeal na watu gani. Hata bwanaake Jux hawezi kutoboa bongo kwa aina ile ya mziki anayoifanya, na uhakika hata Shilole mziki umemnufaisha kuliko Vannesa, ni kwakuwa mziki wake unaendana na watanzania japo kipaji chake hamfikii hata robo Vannesa. Navy Kenzo na wenyewe walikuwa wazungu sana, ila tangu wametoa kamata chini wamefanikiwa kuturoga wabongo, sahvi wanapiga show kila wiki, abadilike kama anataka kufanikiwa kwny mziki, sio anatoa audio ya kiswazi ila video zimejaa uzungu, ataendelea kusubiri sana
sasa navy kenzo hiyo kamatia chini chorus peke yake ndo ya kiswahili ila verse zote zina lugha ngeni tu nafikiri ni melody kiukweli mziki hauna lugha pia kwa V money ni suala la wakati tu maana hata kina nahreel wana nyimbo nyingi hko nyuma
 
mziki
Lakini una mahadhi na asili kutoka na mahali na hadhira husika.....ndio maana kila jamii ina aina ya mziki wake unaowatofautisha na jamii zingine......
Ukipigwa mziki wenye asili ya Caribean kila mtu atajua....
Ukipigwa mziki wenye mahadhi ya kiNigeria kila mtu atafahamu.......hata hao wasanii wa africa magharibi wanatamba ulimwenguni kwa kupiga miziki yenye asili yao kuanzia ala za muziki mpaka aina ya uimbaji.....
Lakini unapojaribu kuuleta aina ya mziki mpya kwenye jamii ambayo tayari kuna aina ya muziki imeshaipokea na kuufurahia lazima muitikio wa mziki huo uwe mdogo kwenye jamii hiyo....[/QUOT
mahadhi anayofanya ya Vanessa sio mapya hapa bongo chunguza hata miziki ya kina unique sisters haina tofauti na ya V hili ni suala la muda tu atatoka Ila pia the bongofleva game is fucked up mashabiki wanalazimishwa kuamini mziki Wa aina flani ndio target sokoni
 
Mtoa mada tambua kitu kimoja, ma promoters hawaangalii ukubwa wa msanii wanaangalia mvuto na uwezo wakujaza watu, msanii anaweza kua mkubwa ila asiwe na mvuto wakujaza watu viwanjani, kua msanii2 haitoshi kuna mambo yaziada unatakiwa kua nayo ili uvute usikivu wa watu kwako, ndio maana diamond ataendelea kua juu
 
Ule wimbo wake wa come over baby, biti nzuri sauti nzuri video nzuri lakini tatizo lugha na uvaaji. Akipunguza uzungu nadhani atakua zaidi ya alipo sasa.
 
wabongo kwa unafiki..mbona kuna wanamuziki wanapiga nyimbo za kiswazi kabisa hawana uzungu wowote na wanakula ugali maharage uswahilini kwa mama ntilie lakini hawavumi? SOMETIMES KUVUMA NI BAHATI TU YA MTU NA MASKENDO YA HOVYO HOVYO
 
Aka kademu siku hizi kamejichubua na kanapaka marangi rangi usoni kamekuwa Kama kaclown ka birthday za watoto.
 
Lugha sio tatizo nilikuwa gaborone live band walipiga nyimbo za kiswahi sina makosa watu walicheza sana na kuimba
relative wa rafiki yng alishangaa naujua huo wimbo nikamwambia ni wa Tz akasema naupenda ingawa sijui maana yake. Vanessa lugha sio tatizo ni wewe hujui soko la ndani linataka nini pia live kuimba huwezi kucheza tu beyonce anaimba live so kaza buti
 
Naunga mkono wanaosema UZUNGU UMEZIDI, Ingawa una umuhimu wake Kimataifa ..!!

Yeye ndo hatutendei haki mashabiki wa nyumban, na sio kwenye music tu, hata kwenye mahojiano ya kawaida..!!

Aweke UZUNGU kimataifa na aweke USWAHILI nyumban, ajue kuchanyanga na kutenganisha majukwaa na mashabiki, ni muhim sana kwa Wabongo ..!!
 
Kuna watu walikuwa wanamfananisha Vanessa na Jide wakati hata kuandika tu mpaka amemsikilizie Barnaba.

Project yake ya Niroge imefeli mapema wakati Jide ana sold out concert.
 
Lakini una mahadhi na asili kutoka na mahali na hadhira husika.....ndio maana kila jamii ina aina ya mziki wake unaowatofautisha na jamii zingine......
Ukipigwa mziki wenye asili ya Caribean kila mtu atajua....
Ukipigwa mziki wenye mahadhi ya kiNigeria kila mtu atafahamu.......hata hao wasanii wa africa magharibi wanatamba ulimwenguni kwa kupiga miziki yenye asili yao kuanzia ala za muziki mpaka aina ya uimbaji.....
Lakini unapojaribu kuuleta aina ya mziki mpya kwenye jamii ambayo tayari kuna aina ya muziki imeshaipokea na kuufurahia lazima muitikio wa mziki huo uwe mdogo kwenye jamii hiyo....
Hivi kwaito na beat za naija anazotumia Diamond na wenzake asili yake ni Tz!? Ungesema mchiriku au singeli ningeelewa. Wote wanaiga tu.
 
uzungu umemzidia, kazi zake amelenga zaid watu wa nje kuliko soko la ndani!!
abadilike tu la sivyo itakua hivihivi tu miaka yote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom