Watanzania hatuko seriuos katika kutetea maisha yetu

Joined
Mar 9, 2011
Messages
89
Points
0
Joined Mar 9, 2011
89 0
Kama umesoma gazeti la Rai la Juzi tarehe 1/08/2011, ukabahatika kusoma Makala inayohusu Eneo la Ramsar la bonde la kilombero utaona ni jinsi gani watanzania wanaweza kujali masuala Rahisi kama maandamano na hoja za wabunge hata ajira ya mmoja kama bwana Jairo wakati kuna masuala yanayohusu maisha yao na hatima ya watoto wao wakayaona ni ya kawaida. katika makala hayo mwandishi amejaribu kueleza umhimu wa bonde la Kilombero kwa uchumi wa Morogoro na Tanzania kwa ujumla. Kwa kifupi maendeleo ya watu wa Kilombero na Taifa la Tanzania yatakuwa hatarini iwapo wafugaji ambao wamevamia bonde hilo hawataondolewa. Wafugaji hao waliotokea Ihefu wanachunga mifugo yao ambayo hakuna anayejua idadi yake lakini inatosha kusema kuwa wanaharibu bonde hilo ambalo umuhimu wake hauishii kilombero peke yake bali Mpaka Dar es salam na wakulima wa bonde la Rufiji kwa ujumla.Bonde hilo linachangia theluthi mbili ya maji ya mto Rufiji, Hii ni kusema kuwa hata pori la akiba la Selous litakuwa hatarini iwapo bonde hili litatoweka. Ndoto za kufua umeme wa maji Stiglers Goerge ni ndoto za mchana ambazo daima hazitakuwa kweli iwapo sauala la mifugo iliyozidi uwezo wa bonde haltachukuliwa hatua. Wale wanaopenda mchele wa Ifakara nao wasisahau kuwa wana miaka michache ya kula mchele huo, Na wakazi wa Kilombero waanze kufanya utafiti wa maeneo ya kuhamia maana bonde litakapokuwa tayari limekaushwa na mifugo hapatakalika hapo. Wana JM na wabongo tuiambie serikali yetu wakiwemo wanasiasa tuwe serious tusingoje mmbo yakiwa yameharibika ndipo tumtafute mchawi. tuwe Pro active.
 

Forum statistics

Threads 1,352,652
Members 518,177
Posts 33,065,365
Top