Watanzania changamkieni ajira Umoja wa Mataifa --DK MIGIRO!!!

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Habari za Kitaifa Habari zaidi!
Watanzania changamkieni ajira Umoja wa Mataifa
Angela Semaya
Daily News; Sunday,July 20, 2008 @00:02

a asisitiza Bunge lijadili ripoti ya madini

Watanzania wametakiwa kuwa na tabia ya kuthubutu na kuchangamkia nafasi mbalimbali za ajira zinazotangazwa katika Umoja wa Mataifa na taasisi zake. Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Dk. Asha-Rose Migiro alitoa changamoto hiyo Dar es Salaam jana alipozungumza na waandishi wa habari.

Dk. Migiro alikuwa akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kuhusu uwiano wa ajira na kama Watanzania wana nafasi za kupata ajira kama watu wa mataifa mengine. Alisema ajira zimekuwa zikitangazwa kwa ajili ya watu wa nchi zote wanachama kuomba, lakini Watanzania wamekuwa wakisita hasa kwa hofu ya kazi za mikataba.

“Wenzetu wa mataifa mengine wanathubutu, lakini sisi Mtanzania anaona akiacha kazi huku nyumbani halafu apate mkataba wa miaka miwili wa kazi UN halafu itakuwaje…lakini hasa vijana mnapaswa kujiamini na kujaribu mambo mengine yatakuja mbele,” alisema. Aliwataka pia vijana kujiimarisha na kujifunza lugha mbalimbali za kigeni ili kujiwekea nafasi nzuri ya kupata ajira UN na taasisi zake.

Migiro alisema pamoja na nafasi yake UN, lakini bado Tanzania ina jukumu la kupeperusha bendera yake katika chombo hicho kwa Watanzania kufanya kazi, kujenga amani na kusaidia nchi nyingine katika kujitafutia amani. Akizungumzia masuala mengine yanayohusiana na shughuli za UN, alisema chombo hicho kimekuwa kikikabiliwa na changamoto nyingi na matatizo yanayohitaji ufumbuzi wa haraka.

Dk. Migiro alitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kupanda kwa bei ya mafuta na chakula, mabadiliko ya hali ya hewa, masuala ya usalama na maendeleo na utunzaji wa amani, kustawisha usalama na utengamano. Hata hivyo alisema changamoto hizo zinaweza kukabiliwa katika nchi husika iwapo zitaweka sera nzuri na usimamizi madhubuti ya kufikia malengo ya milenia.

Alisema Tanzania ni kati ya nchi ambazo zimekuwa na maendeleo ya kuridhisha na kwamba ikiwa na sera nzuri na usimamizi madhubuti inaweza kuyafikia malengo hayo na kuyataja baadhi ya mafanikio ambayo yameonekana ni katika suala la elimu, uwiano wa kijinsi na afya.

Akizungumzia suala la amani na usalama, alisema bado dunia imekuwa ikikabiliwa na changamoto katika eneo hilo, lakini UN imekuwa ikijitahidi kutafuta suluhu katika nchi zinazokabiliwa na tatizo la uvunjifu wa amani na usalama. Dk. Migiro alisema ukiukwaji wa haki za binadamu na kukosekana kwa demokrasia pia imekuwa chanzo cha kuhatarisha amani na usalama katika baadhi ya nchi.

Alisema bado katika baadhi ya nchi suala la demokrasia ni tete na matokeo yake kipindi cha uchaguzi migogoro mingi ya kisiasa huibuka. “Dawa ni kujenga misingi ya demokrasia ili kipindi baada ya uchaguzi usiwe ndiyo wakati wa kutatua migogoro ya kisiasa,” alisema. Akielezea suala la matumizi ya rasilimali alisema matumizi mazuri ya rasilimali katika nchi husika ni nafasi nzuri ya kujiletea maendeleo na kwamba UN ina sera mbalimbali ambazo zinaweza kusaidia Tanzania, Afrika na dunia nzima kutumia vizuri rasilimali na kupinga vita.
 
Asante tutajaribu, lakini historia inaonyesha huko kazi ni kwa majina. Ila kwavile umetupa moyo basi tutajitosa tu mama.
 
Ajaze Kwanza Wakina Mtengeti Na Migiro Ndio Tutakuja


Aige Nfano Wa Mama Mongela Ukoo Mzima Uko Kule Hata Uktuma

Unaweza Kuwa Na Uhakika Kidogo Thnx Mama Mig!!!

Big Up Kwa Mzee Kulenga Kichwa Chenye Akili!!!
 
Namshauri mh.sumaye ajaribu kutafuta kibarua huko, kwani tangu agraduate MBA pale havard hajapata ajira, wala hatujasikia japo chuo kimoja kikimwomba awe TA!
 
Hata wakufagia na kupiga deki tunaruhusiwa? na je security guard? kwi kwi kwi kwi!
 
Miratkad

ingia hapa na uji-register kwanza.....kwani ndio sharti la kwanza (ni ka-process karefu kidogo, lakini ukimaliza mengine mteremko!!!!)

https://jobs.un.org/Galaxy/Release3/vacancy/vacancy.aspx?lang=1200
 
Back
Top Bottom