Watanzania amkeni!

Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,328
955
Tabia ya aliyekuwa waziri mkuu Ndugu El si nzuri kwa muktaba ya baadae hapa nchini mwetu. Sasa hivi amekuja na njia ya kukosoa serikali ili hali na yeye yuko katika chama kinachotawala. Mfano wake ni hapo aliposema mfumo wa elimu ubadilishwe. Swali ni je alipokuwa waziri hakuona hilo? 1.Je ccm hawashauriani katika vikao vyao ilhali wanasema wanatekeleza sera zao?
2.Kwa nini mipango aliyonayo kwa ajili ya maendeleo asiwaambie wenzake ili kuleta maendeleo badala ya kuizungumzia kimafumbo?(UBINAFSI)
3. Tabia ya kuchangia mamilioni kila aendako ni misaada kweli au ndiyo rushwa yenyewe kwa mlango wa uani? Hapa tujiulize amepata wapi hizo fedha,amezipataje,atazirudishaje?(UROHO WA MADARAKA)
4.Nini hatma ya makundi yao,faida na hasara kwa wananchi.

Kwa mtazamo wangu El anasura mbili yaani anaonyesha tabasamu/huruma ilihali moyoni anaroho ya ukatili.

Si kila tukio la kiongozi ni la kulifurahia/kutukuza.tujifunze kuyatafakari kwa kina faida na hasara kwa maisha ya kesho. Tuache kufikiria leo.
 
Demokrasia inaruhusu mwanchama wa CCM kuwa na maoni yake binafsi. Muache EL atoe maoni yake binafsi ingawa mwenyekiti wenu hashauriki. By the way Joka la Mdimi hana caliber ya kuwa Kiongozi wa hii nchi, yeye uwaziri aliopewa kwa Nepotism unamtosha
 
Back
Top Bottom