nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Na Mwandishi wetu | Nipashe
Watanzania takribani 120 wanashikiliwa katika mahabusu za Iran kwa makosa mbalimbali kwa miaka minne sasa huku jitihada za serikali ya Tanzania kuwanusuru zikiwa zimekwama.
Watanzania hao wanashikiliwa kwa makosa mbalimbali, yakiwamo ya kukamatwa na dawa za kulevya na kuingia Iran bila vibali.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Christopher Mvula, alithibitisha kushikiriwa kwa Watanzania hao katika mahabusu nchini Iran.
Mvula alisema mbali na Watanzania hao kushikiliwa, mazungumzo kati ya Tanzania na Iran kuhusu kuwarejesha nchini yanaendelea, lakini suala hilo linakuwa gumu kutokana na nchi hizo kutokuwa na sheria ya kubadilishana wafungwa.
Mvula aliongeza kuwa kikwazo kingine ni kutokana na Tanzania kutokuwa na ubalozi nchini Iran badala yake na kutumia ubalozi wa Falme za Kiarabu.
Alisema Iran kuwaachia watu hao siyo kitu cha haraka na rahisi kutokana na watuhumuiwa wengi kukamatwa na makosa makubwa.
Mvula alisema kuna makosa madogomadogo ambayo yanaweza kuzungumkika kama vile ya kusingiziwa, kuiba, lakini siyo yale makubwa kama ya dawa za kulevya.
Alisema vijana wengi wa kitanzania waliokamatwa Iran wamekamatwa kwa tuhuma za makosa hayo na wachache makosa madogo kama uzamiaji na ndiyo maana zoezi la kuwaachia na kuja kutumikia adhabu nchini linachukua muda mrefu.
Mmoja wa ndugu wa Watanzania hao ambaye pia ni Mwenyekiti wa wazazi wa ndugu hao, Bidie Bulushi, alisema lichas ya vijana wao kushikiliwa Iran kwa muda huo, serikali haijaonyesha jitihada za kuwanusuru.
Alisema miongoni mwao ni mdogo wake wa tatu, Ali Seif, aliyeingia Iran mwaka 2005 kwa lengo la kutafuta maisha akiwa na wenzake watatu, lakini wenzake walifanikiwa kurejea na yeye kukamatwa na kuwekwa mahabusu katika moja ya magereza nchini humo.
"Ni mdogo wangu wa tatu, alikwenda Iran kutafuta maisha akiwa na wenzake watatu, mmoja wa wenzake hao anaitwa Chalula, yeye ndiye aliyeleta taarifa kuwa Ali amekamatwa na yuko gerezani," alisema Balushi.
Alisema, walikwenda mara kwa mara katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kufuatilia suala hilo, lakini waliishia kuambiwa waandike barua yenye maelezo yanayoonyesha ndugu zao wamekamatwa kwa makosa yapi.
Alisema kwa mara ya kwanza walifikia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa idara ya Mashariki ya Kati mwaka jana, na kukutana na Hellen Kafumba aliyewaambia waandike barua ya maelezo kuhusu ndugu zao hao waliokamatwa nchini Iran.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuandika barua hiyo walijibiwa kuwa wasubiri wizara inalishughulikia suala hilo.
Alieleza kuwa walisubiri kwa kipindi kirefu bila kupata majibu ndipo waliporudi na wakapelekwa kwa mtu mwingine itwaye Kambona na kuambiwa kuwa mkakati uliopo kwa sasa ni mazungumzo ya kubadilishana wafungwa yanaendelea.
Moja ya chanzo cha habari ambacho NIPASHE imekipata kutoka ubalozi wa Iran nchini, zinasema kuwa Watanzania wengi hufika ubalozini hapo kuomba viza kwenda Iran kuabudu katika moja ya makaburi waliozikwa wajukuu wa Mtume Muhamadi (S.A.W) Hussein na Hassan yaliyopo katika mji wa Kerbala.
Habari zaidi zinaeleza kuwa wanapofika huko na muda wao wa kukaa ukiisha wengi hujificha huko, hali inayopelekea kukamatwa.
Jitihada za kumpata msemaji wa ubalozi wa Iran nchini zilishindikana kutokana na mwandishi kufika ubalozini mara kadhaa na kuambiwa kuwa hayupo.