Watanzania 120 washikiliwa mahabusu za Iran

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Na Mwandishi wetu | Nipashe

Watanzania takribani 120 wanashikiliwa katika mahabusu za Iran kwa makosa mbalimbali kwa miaka minne sasa huku jitihada za serikali ya Tanzania kuwanusuru zikiwa zimekwama.

Watanzania hao wanashikiliwa kwa makosa mbalimbali, yakiwamo ya kukamatwa na dawa za kulevya na kuingia Iran bila vibali.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Christopher Mvula, alithibitisha kushikiriwa kwa Watanzania hao katika mahabusu nchini Iran.

Mvula alisema mbali na Watanzania hao kushikiliwa, mazungumzo kati ya Tanzania na Iran kuhusu kuwarejesha nchini yanaendelea, lakini suala hilo linakuwa gumu kutokana na nchi hizo kutokuwa na sheria ya kubadilishana wafungwa.

Mvula aliongeza kuwa kikwazo kingine ni kutokana na Tanzania kutokuwa na ubalozi nchini Iran badala yake na kutumia ubalozi wa Falme za Kiarabu.

Alisema Iran kuwaachia watu hao siyo kitu cha haraka na rahisi kutokana na watuhumuiwa wengi kukamatwa na makosa makubwa.

Mvula alisema kuna makosa madogomadogo ambayo yanaweza kuzungumkika kama vile ya kusingiziwa, kuiba, lakini siyo yale makubwa kama ya dawa za kulevya.

Alisema vijana wengi wa kitanzania waliokamatwa Iran wamekamatwa kwa tuhuma za makosa hayo na wachache makosa madogo kama uzamiaji na ndiyo maana zoezi la kuwaachia na kuja kutumikia adhabu nchini linachukua muda mrefu.

Mmoja wa ndugu wa Watanzania hao ambaye pia ni Mwenyekiti wa wazazi wa ndugu hao, Bidie Bulushi, alisema lichas ya vijana wao kushikiliwa Iran kwa muda huo, serikali haijaonyesha jitihada za kuwanusuru.

Alisema miongoni mwao ni mdogo wake wa tatu, Ali Seif, aliyeingia Iran mwaka 2005 kwa lengo la kutafuta maisha akiwa na wenzake watatu, lakini wenzake walifanikiwa kurejea na yeye kukamatwa na kuwekwa mahabusu katika moja ya magereza nchini humo.

"Ni mdogo wangu wa tatu, alikwenda Iran kutafuta maisha akiwa na wenzake watatu, mmoja wa wenzake hao anaitwa Chalula, yeye ndiye aliyeleta taarifa kuwa Ali amekamatwa na yuko gerezani," alisema Balushi.

Alisema, walikwenda mara kwa mara katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kufuatilia suala hilo, lakini waliishia kuambiwa waandike barua yenye maelezo yanayoonyesha ndugu zao wamekamatwa kwa makosa yapi.

Alisema kwa mara ya kwanza walifikia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa idara ya Mashariki ya Kati mwaka jana, na kukutana na Hellen Kafumba aliyewaambia waandike barua ya maelezo kuhusu ndugu zao hao waliokamatwa nchini Iran.

Aliongeza kuwa mara baada ya kuandika barua hiyo walijibiwa kuwa wasubiri wizara inalishughulikia suala hilo.

Alieleza kuwa walisubiri kwa kipindi kirefu bila kupata majibu ndipo waliporudi na wakapelekwa kwa mtu mwingine itwaye Kambona na kuambiwa kuwa mkakati uliopo kwa sasa ni mazungumzo ya kubadilishana wafungwa yanaendelea.

Moja ya chanzo cha habari ambacho NIPASHE imekipata kutoka ubalozi wa Iran nchini, zinasema kuwa Watanzania wengi hufika ubalozini hapo kuomba viza kwenda Iran kuabudu katika moja ya makaburi waliozikwa wajukuu wa Mtume Muhamadi (S.A.W) Hussein na Hassan yaliyopo katika mji wa Kerbala.

Habari zaidi zinaeleza kuwa wanapofika huko na muda wao wa kukaa ukiisha wengi hujificha huko, hali inayopelekea kukamatwa.

Jitihada za kumpata msemaji wa ubalozi wa Iran nchini zilishindikana kutokana na mwandishi kufika ubalozini mara kadhaa na kuambiwa kuwa hayupo.
 
Mbona Makamo wa Rais wao alikuwa Bara na Zanzibar hakuna aliyegusia ?
Makamu wa Rais Bilal akaenda Mkutano wa Nchi zisizofungamana na Nchi zizote hakuongea na huyo Makamu wa Rais?

Tulibeba MELI ZAO kwa SIRI kwa Ubabe wa KIZANZIBARI hawakumbuki ?

Au hao Vijana wetu Wameshindwa kubeba Mabomu TUMBONI ???
 
Vijana wetu na biashara ya unga kutaka utajiri haraka.
 
yakhe vijana napeleka nyunga, wallwah serkal ifanyeje toba yarabi; Kiwete shakataza vijana hapana beba unga; watoto hapana sikia nakwenda kwa sadar beba nyunga.
 
Vijana wetu na biashara ya unga kutaka utajiri haraka.

shekhe podaar natia watoto balaa; Kikwete shasema siku nyingi; wallwah serkal fanya jithada watoto wenyewe balaa; Kwanini ile bwana kubwa Mbowe isende Tehran kusaidia watoto.
 
Inawezekana vipi IRAN iwe na balozi TZ na sisi tusiwe na balozi IRAN? Na kuhusu wafungwa ni kweli Wabongo shortcut tunazipenda sana na nchi za wenzetu sheria kwao zinafutwa sana...Kwetu raia wa kigeni ni wengi na hawana vibali vya kuishi lakini wapo achilia mbali raia wa kigeni ambao ni waarifu ni wengi sana...Cha msingi serikali inaweza kufanya swapping za wafungwa km wapo
 
Sasa wale wanaotaka sheria kama za Iran zije hapa Tz basi wasilalamikie vijana wetu ambao wameanza kuzionja huko!
 
Wengi wanatoka Zenj!!! Ukitaka vya ulaini laini basi mambo ni magumu kama hivi!! Na uturuki wapo kibao!!
 
Nikutokana na serikali ya ccm kutokutengeneza ajira. Ingekuwa china washanyongwa!
 
Ungetubandikia majina ili tuone kama ni ya ki-CUF, ki-CDM au ki-CCM ili tupanue wigo wa kuwasaidia. Ni mawazo tu.
 
Na Mwandishi wetu | Nipashe
Moja ya chanzo cha habari ambacho NIPASHE imekipata kutoka ubalozi wa Iran nchini, zinasema kuwa Watanzania wengi hufika ubalozini hapo kuomba viza kwenda Iran kuabudu katika moja ya makaburi waliozikwa wajukuu wa Mtume Muhamadi (S.A.W) Hussein na Hassan yaliyopo katika mji wa Kerbala.

Kuabudu makaburi?

Hivi kumbe wafu wanaabudiwa eti?
 
Kuabudu makaburi?

Hivi kumbe wafu wanaabudiwa eti?

Kanza hiyo ni kosa KERBALA iko IRAQ ni MJI MTAKATIFU wa SHIITE ni kama VILE JERUSALEM na Wakristo JAMANI...

* Kinachonishangaza kwanini WAFUNGWE HUKO IRAN>>> IRAN HAKUNA KERBALA; KERBALA IKO IRAQ...
 
Safi kabisa. Badala ya kupambana na mwizi wenu CCM mnajiingiza kwenye jinai. Hao jamaa hawana huruma na ni wabaguzi Mungu anajua. Tungekuwa na serikali inayowajali wananchi nasi tungeanza kukamata wairan na maponjoro waliojazana nchini kinyume cha sheria wakifanya biashara hiyo hiyo hata kuuza wanyama wetu. Na kwa sheria za kiislam wajue watachinjwa kama njiwa mchana kweupe huku chekacheka wao akiendelea kujifanya hajui ingawa amewatangeneza yeye. Laiti waliokamatwa angekuwamo Khalfan Miraji au Ridhiwan ngoma ingenoga.
 
Inawezekana vipi IRAN iwe na balozi TZ na sisi tusiwe na balozi IRAN? Na kuhusu wafungwa ni kweli Wabongo shortcut tunazipenda sana na nchi za wenzetu sheria kwao zinafutwa sana...Kwetu raia wa kigeni ni wengi na hawana vibali vya kuishi lakini wapo achilia mbali raia wa kigeni ambao ni waarifu ni wengi sana...Cha msingi serikali inaweza kufanya swapping za wafungwa km wapo

Wewe haujui DEPLOMASIA ? Sio lazima nchi ikiwa na UBALOZI Hapa nchini ni lazima na SISI tuwe na UBALONI nchini Mwao... Kuna NCHI itakuwa inatuwakilisha kule IRAN
 
Mbona Makamo wa Rais wao alikuwa Bara na Zanzibar hakuna aliyegusia ?
Makamu wa Rais Bilal akaenda Mkutano wa Nchi zisizofungamana na Nchi zizote hakuongea na huyo Makamu wa Rais?

Tulibeba MELI ZAO kwa SIRI kwa Ubabe wa KIZANZIBARI hawakumbuki ?

Au hao Vijana wetu Wameshindwa kubeba Mabomu TUMBONI ???

Swala la meli zao halihusiki hapa, wamekamatwa na unga wanastahili kuhukumiwa kwa sheria za iran.
Big up sana iran.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ungetubandikia majina ili tuone kama ni ya ki-CUF, ki-CDM au ki-CCM ili tupanue wigo wa kuwasaidia. Ni mawazo tu.
Unga ni unga tu, majina yao hayatusaidii chochote.
Wacha wale adhabu kenge hao.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Jamani elewesheni vijana wenu. Wawekeni chini huko ulaya maisha ni magumu. Sasa mwingine eti kaenda irna si kajitakia ku fi.r.ww.a tu? Hivi iran kuna maisha kweli? Ama kwa vile jina lake linaendana nao akadhani tu akienda anapewa kazi fasta?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom