Watangazaji wetu ni kasuku? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watangazaji wetu ni kasuku?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kitoto Akisa, Jun 11, 2009.

 1. K

  Kitoto Akisa Member

  #1
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana jamvi naomba hoja zenu katika hili mimi linanitatiza sana. Ni mara nyingi sana kila ninaposikiliza habari au matangazo mbalimbali katika redio zetu au Luninga ninapatwa na mshangao jinsi hao presenters wanavyo potosha jamii. Mfano mzuri ni jana, nilikuwa naangalia habari katika Luninga ya moja hapa Bongo, mtangazaji alikuwa anaelezea ziara ya waziri mkuu wa Kenya huko South Afrika, kilichonishangaza alisema eti nanukuu' waziri mkuu wa Kenya Bwana Raila Odinga amempongeza Rais wa Afrika Kusini Bwana Thabo Mbeki kwa uchaguzi wa Amani' sasa cha kujiuliza inamaana huyu mwandishi hajui kuwa Mbeki sio Rais wa A.kusini, ila Rais ni Jacob Zuma! na ajabu katika picha za Luninga za ziara hiyo zilimuonesha Raila akiwa na Zuma. Mimi nilifikiri yule mwandishi ataomba radhi kwa hilo, lakini wapi jamaa akaendelea na habri zingine as if ameongea kitu sawa. Siku nyingine nilikuwa nasikiliza Redio moja hapa Bongo, kilikuwa ni kipindi cha maswali kwa watoto. Mtangazaji aliwataka watoto waseme jina Moja la Mnyama, ambalo linaweza toa maneno matatu ya kiswahili yenye maana. Watot walijithidi lakini walikwama, ndio mtangazaji akatoa jibu, eti mnyama huyo ni Kangaloo, na akatoa ufafanuzi kuwa maneno hayo matatu yaliyo katika jina Kangaloo ni KANGA, ANGA NA LOO ( ladab alimaanisha "ROHO"), mimi nikakubaliana na maneno mawili ya kwanza, lakini hili la tatu, hapana . Nikajiuliza hivi neno Loo ninamaana gani katika kiswahili? na kama alinaanisha ROHO, inamaana huyu mwandishi alikuwa hajui kuwa Kangaloo haina "H" ili kuleta maana ya ROHO?

  Sasa ndio nauliza jamani hawa waandishi wetu ni kasuku ambao wanakaririshwa cha kusema, au wanauelewa? hivi hakuna wahariri wa vipindi kabla havijaenda hewani? Jamani tusipokuwa makini watangazaji wa jinsi hii watapotosha umma hasa watoto wetu! Nawasilisha
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Kukosea jina ni normal na ni human mistake haina uhusiano na ukasuku. Kwanza msomaji siye aliyeandika, mwandishi alikosea kumwandika Zuma ni Mbeki, msomaji alipewa script ya habari hiyo kuipitia nusu saa kabla. Naye kapitiwa kosa likaenda hewani kama kosa.
  Nikiwa mwandishi huko nyumma niliwahi kuhudhuria tukio mgeni rasmi ni Katibu Mkuu kiongozi, Philemon Luhanjo, kwenye story yangu nikaandika Katibu Mkuu Kiongozi Marten Lumbanga,
  Mhariri akaipitisha hivyo hivyo na msomaji akaisoma hivyo hivyo, picha ya Luhanja, jina la Lumbanga, huo sio ukasuku ni just mistakes.

  Hata hivyo sitetei kuwepo makosa kwenye fani ya habari, lakini
  Pia kuna waandishi na watangazaji wanaofanya ukasuku ili sio kihivyo.
  andishi
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,499
  Likes Received: 1,080
  Trophy Points: 280
  Mie pia, nilimuona mtangazaji mmoja wa channel ten, alishindwa kabisa kutamka wa-adventist! alihangaika mno, mara waadinaa... , waaannnnet!..waadedede!, watsist!.. mwisho alikaa kimya then akaendelea bila kulitamka tena neno hilo wala kuomba radhi kwa kosa hilo!
  Mimi nafikiri kuna umuhimu wa kupitia kwanza habari nzima kabla ya muda wake ili kujipa mazoezi kidogo, sasa hii ya kwenda kusoma moja kwa moja ndiyo inatusumbua!
   
 4. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Ha ha haaa umenikumbusha Masanja Mkoboaji enzi zile EATV... Spoost...Sposisissssss... Spooooooooooooossssssss...Spooootissssssss
   
 5. K

  Kitoto Akisa Member

  #5
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pasco sawa ninakubaliana na wewe kukosea kwa kupitiwa ni ubinadamu, lakini kama ni kweli mwandishi yule alipitiwa akakosea kuisoma script aliyopewa nusu saa kabla, kwa nini alipoona display ya Zuma na Raila katika screen asikumbuke! hii maana yake ni kuwa mtangazaji yule hajui. wewe unasema uliwahi kuwa mwandishi na kwa makosa uliwahi kutoa picha ya Luhanjo lakini jina ni Lumbaga, ikapita kwa mhariri wako, sawa hiyo hutokea lakini pindi itokeapo hali hiyo huwa tunaona toleo la gazeti lile lie ukurasa ule ule wakiomba radhi kwa makosa hayo, na pia huweka habri sahihi, hicho ndio nilitegemea kitokee kwa mtangazaji yule baada ya kuona picha ya ZUma na Raila,na sio Mbeki na Raila kama alivyotaka kutuaminisha!
   
 6. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  #
  Hapana. siyo Normal hayo ni makosa ambayo wahusika hawawezi kusameheka. Mwandishi. Mhariri na Mtangazaji wa habari hiyo. Health cynicism- miaka ile Mkufunzi wetu alitupigia kelele katika hilo kwenye somo la Editing. Sasa Urais wa Afrika ya Kusini ukamwachia Mbeki tena baada ya Zuma. Wapi Bwana? Mtangazaji naye ni kasuku kweli. Kwa nini anashindwa kuona kitu kama hicho? Ingekuwa jina la mtu asiye maarufu na akalikosea (kimatamshi) hapo ndio ungesema suala la kosa la kibinadamu.
   
 7. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hayo ni makosa ya kawaida,alichotakiwa kufanya ni kuomba radhi kwa kosa hilo.Mimi nadhani ukasuku wa waandishi wetu ni pale wanapotumiwa kupotosha ukweli makusudi kwa manufaa ya kikundi fulani.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,601
  Likes Received: 18,611
  Trophy Points: 280
  Asante umenipata na umemsaidia muanzisha thread kutafsiri ukasuku.
  Ukasuku kwa waandishi ni kulishwa maneno kama kinachoendelea kwa waandishi wa vyombo vya habari vya mafisadi wakiwepo wa papa na nyangumi.

  Kabla ya uchaguzi tutashuhudia ukasuku at its best na mpaka photoshop kutumika ili kumake belive.
   
 9. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Naamini kuwa kunaweza kukawa na makosa ya kibinadamu. Waandishi wetu wa habari siku hizi wanajitahidi sana ukilinganisha na miaka ya nyuma. Ninazungumza hili kwa maana ya mantiki zilizomo katika habari na si makosa ya kibinadamu kama mtoa hoja alivyoongelea. Wakati IPTL inakuja waandishi walilitupa taarifa za "ukasuku" kuonesha kuwa ni bonge la mradi lakini kumbe ulikuwa ufisadi tupu!!!

  Nawapongeza waandishi wetu wa habari kwa hatua nzuri waliyofikia pamoja na kuwa na makosa. Nawaomba wajitahidi kuboresha taaluma yao ili makosa kama hayo yafutike kabisa.

  Mungu ibariki Tanganyika na Zanzibar!
   
Loading...