Watangazaji Wetu na elimu zao

Bandugu naomba mnpe elimu za hawa watangazaji
1.regina mwalekwa
2.manfred masaku
3.gerald hando
4.maulid kitenge
5.orest kawau
6.masoud kipanya
7.suleiman semunyu
8.arnold kayanda
9.millard ayo
10.scholastica mazulla!
skia madu...mi mwenyewe niliishia darasa la saba lakin ofisin nawakimbiza kwa mbali sana kiufanisi wa kazi wenye madegree kiasi cha wakuu wangu kuniamini sana kuliko hao wasomi.kibongobongo elimu its not a big deal
 
Umemuelewa vibaya mtoa mada. Hajasema wanatangaza vibaya au vizuri, anataka kujua profile ya elimu yao tu. Umejistukia halafu unajidefend eti unawakimbiza wenye digríi na nini sijui.? Ndo mana tunasema watu waende shule , ona sasa ulivyoapost utumbo.!
 
umenijib kimasaburi sana,wewe kweli mchemsho.sio kosa lako.lol
 
Utangazaji ni kipaji na sio elimu, japo nakiri kuwa kuwa na kipaji pekee hakutoshi kukufanya mtangazaji mahiri zama hizi za utandawazi hivyo kuwa na elimu bora ni added advantage.

Kwa vile utangazaji kwanza ni kipaji ndipo elimu inafuatia, hata ukiwa na elimu vipi, bila kipaji ni bure.

Katika vituo vya Utangazaji nchini, TBC ndio inayoongoza kwa madegree holders na cha mwisho kwa kuwa na degree holders wachache zaidi ni Clouds leo nimemsikia mtangazaji mmoja ndio amegraduate Saut.

Japo TBC ndio onayoongoza kwa watangazaji wenye shule kubwa, karibu watangazaji wao wengi wenye vipaji vikubwa, shule zao ni za kawaida na wale shule kubwa vipaji vyao ni hafifu, huku Clouds yenye wenye shule hafifu lakini vipaji vikubwa ndio wanaowashika haswa watazamaji/ wasikilizaji.

Pasco huwa naheshimu sana mawazo yako. Leo katika hili naomba kutofautiana nawe kwa kiasi kikubwa kwa sababu zifuatazo:

1. Mara nyingi tunawalalamikia wanahabari kuwa wana upeo finyu katika kutuletea habari zao (hii ni pamoja na waandishi wa magazetini na wa radio na TV). Tunawalalamikia sababu wengi wao wanafanya kazi kwa hicho ambacho wewe unaita ni kipaji na sio elimu. Kwa kutegemea kipaji badala ya elimu, tutaendelea kuwalalamikia hadi mwisho wa dunia.

2. Waandishi (naomba niwajumuishe wote, Radio, TV na magazeti) wanapokuwa na vipaji na elimu finyu, wanakuwa hawana uwezo wa kuchanganua mambo. Hawana uwezo wa kuhoji kitu kwa misingi ya ku-dig for information. Matokeo yake wengi wao ni maripota tu kwa maana ya kwamba wanaandika na kutangaza kile kilichopo tu ama kinachosemwa na source, na sio kutafuta kilichojificha behind the scene. Huu sio uanahabari na hii inasababishwa na kutegemea kipaji na sio elimu.

3. Hebu chukua watangazaji wa TV za nje kama Christine Amanpour, Larry King, Vicent Makori, Shaka Salli, na wengineo wengi, angalia CV na elimu zao zikoje. Wote hao wana shahada na wengine shahada za juu (PHD) na unaweza kujionea hilo wanapokuwa wana-host kipindi. Kama ingekuwa ni swala la kipaji na sio elimu zao, wasingekuwa na upeo na ufahamu mkubwa kama walionao sasa. ELIMU!

4. Maswali yanayoulizwa na watangazaji wa vipaji katika radio na TV zetu ni AIBU Pasco! Please hebu fuatilia uone, mtangazaji wa michezo anamuuliza kocha ambaye timu yake imefungwa bao 3-0 eti UMEUONAJE MCHEZO? Niambie unategemea jibu gani wakati timu imefungwa? atasema mchezo mzuri kwao???????? Mtu anashindwa kuangalia mechi na kubaini dosari zilizokuwepo wakati timu iliposhinda bao 2-0 na leo ilipofungwa bao 3-0 na kumuuliza kocha kuanzia hapo na badala yake anamuuliza eti UMEUONAJE MCHEZO?????? Hivi vipaji vinatupeleka kubaya sana.

5. Fani ya habari (kuanzia magazetini hadi Radio na TV) inaonekana kwa sasa ni kimbilio la watu wenye elimu duni na waliofeli mitihani. Sio katika radio na TV tu, bali hata katika magazeti ni nadra kukuta mwanahabari mwenye degree walau ya kwanza na kuendelea kuanzia wahariri hadi waandishi. Ndio sababu wengi wao wanafanya kwa kupokea hongo, mishiko na kutumiwa zaidi badala ya kuitumikia taaluma yao. Ndio maana kuna utitiri wa vyuo vya mtaani kama DSJ, IAMCO, TSJ, MSJ, Royal School of Journalism na vingine chungu nzima ambavyo vyote vinafundisha uandishi wa habari kwa waliofeli form four. Ni hao ndio wanakuja kuwa watangazaji na waandishi kwenye magazeti yetu. Tutarajie nini toka kwao? Critical writings??? Never!!

Nina sababu nyingi lakini itoshe kuishia hapa na kusema kuwa Kipaji badala ya elimu inapeleka kubaya taaluma ya habari kwenye media zetu zote. Kila mwenye sauti nzuri anaweza kutangaza, lakini atakuwa critical kwa kiasi gani??? Au itakuwa ni kujiaibisha na kuiaibisha taaluma mbele ya wasikilizaji na wasomaji?????
 
Mwana Mpotevu,
Hakuna ubishi, fani ya habari imevamiwa, sio tuu na wasio na vipaji, wasio na elimu na wasio na uwezo tuu, bali hata wengine wameona huo ndio mteremko wa kutokea.

Kazi ya uandishi wa habari ni wito kama ulivyo ualimu, lakini kwa vile fani imevamiwa, imekuwa kimbilio hata kwa wasio na wito.
Sio kweli waandishi ni waliofeli tuu, ma editor karibu wote wa magazeti makini wana masters. Maripota wakuu wa magazeti yote serious ni madegree holders.

Sifa ya kujiunga TBC ni degree ya kwanza!.

Tatizo la tasnia ya habari kwetu hailipi!, hivyo inashindwa kupata waandishi waliospecialize, na wengi wa wa waandishi wakisha specialize, hawarudi tena newsroom, wanaelekea kwenye greener pasture!.

Hivi ujajua Benjamin Mkapa, Prof. Palamagamba Kabudi, Dr, Harrison Mwakyembe, Dr. Sengodo Mvungi, Suleiman Kumchaya, Mustapha Nyanganyi etc, wote walikuwa ni waandishi wa habari, walipospecialise uandishi bye bye.

Usitulinganishe sisi na BBC, na CNN huko ni mbali, nenda tuu hapo Kenya soma magazeti yao, angalia TV yao au nenda Uganda.
Kenya wana magazeti serious 4 tuu na TV Stations 3. Sisi tuna magazeti daily zaidi ya 10, vituo vya TV zaidi ya 10 vituo vya redio ndio usiseme, yaani ni utitiri kama vilivyo vyama vya siasa!. Matokeo yake, kasungura ni kadogo, huwezi kuwalipa vizuri waandishi mahiri.

Kufuatia soko kuwa kubwa, vyuo vya mtaani navyo vimeshamiri, kuna siku niko mahali, kuna tukio, mgeni rasmi ni waziri fulani maarufu, kuna kabinti kakanijia, na kunuiliza, eti huyu mgeni rasmi anayezungumza ni nani?, nikashangaa, hata hivyo nikamtajia huyu ni waziri fulani, akaniuliza tena ni waziri wa nini?. Binti yangu wa darasa la sita anamjua, yeye mwandishi hajui!. Nikamtajia na kumuuliza anatokea gazeti gani, (naomba nilihifadhi). Conclusion yangu huyo binti ni standard seven leaver!, katoa chochote chuo cha mtaani, kauziwa cheti, katika news room kagawa uroda, kaajiriwa!. Kesho yake nikalinunua gazeti lake kumsoma, nikakuta story safi tuu imesimama!.

Naomba tusilizungumze suala la waandishi na vibahasha, hili ni suala jingine kabisa!

Lengo la mada ni watangazaji na elimu zao, sio waandishi na elimu zao.
 
Utangazaji ni kipaji na sio elimu, japo nakiri kuwa kuwa na kipaji pekee hakutoshi kukufanya mtangazaji mahiri zama hizi za utandawazi hivyo kuwa na elimu bora ni added advantage.

Kwa vile utangazaji kwanza ni kipaji ndipo elimu inafuatia, hata ukiwa na elimu vipi, bila kipaji ni bure.

Katika vituo vya Utangazaji nchini, TBC ndio inayoongoza kwa madegree holders na cha mwisho kwa kuwa na degree holders wachache zaidi ni Clouds leo nimemsikia mtangazaji mmoja ndio amegraduate Saut.

Japo TBC ndio onayoongoza kwa watangazaji wenye shule kubwa, karibu watangazaji wao wengi wenye vipaji vikubwa, shule zao ni za kawaida na wale shule kubwa vipaji vyao ni hafifu, huku Clouds yenye wenye shule hafifu lakini vipaji vikubwa ndio wanaowashika haswa watazamaji/ wasikilizaji.

Very well put Pasco.
 
i3. Hebu chukua watangazaji wa TV za nje kama Christine Amanpour, Larry King, Vicent Makori, Shaka Salli, na wengineo wengi, angalia CV na elimu zao zikoje. Wote hao wana shahada na wengine shahada za juu (PHD) na unaweza kujionea hilo wanapokuwa wana-host kipindi. Kama ingekuwa ni swala la kipaji na sio elimu zao, wasingekuwa na upeo na ufahamu mkubwa kama walionao sasa. ELIMU!

Larry King ana shahada gani na ya wapi?

Larry King: Twelve or 13. When I finished high school, I didn't have good enough grades to go to college, my father had died when I was young, and I had to help my mother, so I worked a bunch of odd jobs. I worked on the United Parcel Service truck, I sold home delivery of milk. But always, in the back of my mind, I wanted to get into radio.

Source: http://www.achievement.org/autodoc/page/kin0int-1
 
mwanampotevu hizi degree za miaka ya leo, unaziamini kweli? Unamponda aliyepata Div IV o'level na kuingia kwenye Journalism. Mimi kuna bwamdogo mmoja amekuwa akifeli Primary school mpaka unamwita bongolala. Walihamia UK akawa kwenye mambo ya marketing na anayaendesha maisha yake vyema hivi sasa huko ughaibuni. Na hao wako wengi tu! Sidhani kama kila mwenye Div IV ni akaingia katika taaluma nyingine akaifanya kazi yake vema,asiitwe msomi. Basi atafutiwe jina lake!
 
Hii mada ina utata kidogo.... utangazaji ni kipaji na "passion" kwa kiasi kikubwa lakini elimu ni muhimu sana ili kufanya utangazaji wako uwe na mvuto zaidi na wenye upeo wa juu. Ni vema pia ujue unataka jamii yako ipokee nini kutoka kwako ili kuongeza umahiri na kufanya vipindi kinachoelekeana inaongeza ufanisi (sio leo mapishi, kesho burudani, keshokutwa michezo, jumapili unahoji wanasiasa).
Lakini ukiwa mwandishi elimu ina ulazima mkubwa ili kuandika habari zenye ukweli mwingi na ubunifu zisimchoshe mpokeaji. Elimu ukiitumia vizuri ukaelimika unakua na upeo mkubwa na mvuto wa aina yake
 
Utangazaji ni kipaji na sio elimu, japo nakiri kuwa kuwa na kipaji pekee hakutoshi kukufanya mtangazaji mahiri zama hizi za utandawazi hivyo kuwa na elimu bora ni added advantage.

Kwa vile utangazaji kwanza ni kipaji ndipo elimu inafuatia, hata ukiwa na elimu vipi, bila kipaji ni bure.

Katika vituo vya Utangazaji nchini, TBC ndio inayoongoza kwa madegree holders na cha mwisho kwa kuwa na degree holders wachache zaidi ni Clouds leo nimemsikia mtangazaji mmoja ndio amegraduate Saut.

Japo TBC ndio onayoongoza kwa watangazaji wenye shule kubwa, karibu watangazaji wao wengi wenye vipaji vikubwa, shule zao ni za kawaida na wale shule kubwa vipaji vyao ni hafifu, huku Clouds yenye wenye shule hafifu lakini vipaji vikubwa ndio wanaowashika haswa watazamaji/ wasikilizaji.
Mbona hapa huja-declare interest mkuu?
 
Labda Me Niweke Hv, Kila Ktu Kinahtaj Talent Mf. Marketing, Programing, Architect, Politics, Nk Japo Kwa Nchi Zetu Mackn Tunalazmisha Kutokana Na Soko La Ajira. Katika Tasnia Ya Habar Kunavtengo Vngi Hvyo Mtu Anaweza Kuchagua Kp Cha Kukiendeleza Kutokana Na Uwezo Wake Wa Kukimudu. Elimu Inahtajika Tena Sana Kwa Tasnia Yoyote Ile Sema Wenye Elimu Duni Ktk Secta Yoyote Wananafac Kubwa Kutokana Na Kujarib Bla Kuhofia Kufeli. Mf. Mwanahabar Aliyesoma Hawez Anzish Kpnd Cha Ushilawadu Au Ukute Anaandika Habari Za Udaku Au Marachache Msomi Kukuta Anatembeza Mihogo. Hzo Zote Ni Fursa Lkn Tatzo La Kusoma Unajijengea Limitations Kwenye Mambo Mengi Kuanzia Unacho Zungumza, Vpndi Unavotaka Kuvifanya, Mshahara Kwa Wamiliki Nk. So Kwa Maisha Ya Low Class Ni Rahc Kumjua Bilard Ayo Kuliko Adam Simbeye Au Yule Dogo Wa Capita Tv Na Kpnd Chake Cha Ung'eng'e. Au Ni Rahic Kumfahamu Mwandish Wa Ijumaa Kuliko Mwanachi. Au Ni Rahc Mtu Kuckiliza EFM Kuliko BBC Swahili, Au DW. Vpaj Vpo Lkn Ukwackiliza Sn Utakuta Hamna K2 Vchwani.
 
Kuna jamaa yupo Fm moja Mbeya kule ana uelewa mpana sana anafanya kipindi cha kiingereza jioni kwenye redio moja ya dini jina lake simkumbuki, ila ukimsikiliza unaona ni mtu anaejitambua sana, tatizo focus kubwa ni hawa watangazaji wa Dar ila viredio vya mkoa baadhi vina watangazaji wakali sana, nimewasikia pia baadhi ya watangazaji pale Moro wapo vizuri sana na Kili Fm pia Kwizera Fm, hawa wamiliki waajiri vijana wenye upeo mpana na wenye elimu inayoeleweka
 
Back
Top Bottom