Jumapili iliyopita nilikuwa nasikiliza kipindi cha watoto wa shule ya Msingi fulani katika manispaa ya Morogoro. Kipindi kilikuwa kinarushwa na radio moja maarufu Morogoro, nilimsikia mtangazaji anawaambia wanafunzi kuwa mlima K'njaro una urefu wa zaidi ya km 5,000 badala ya mita zaidi ya 5,000 pia alisema Mikumi ndiyo mbuga kubwa kuliko zote za wanyama. Wito wangu ni kwamba mtangazaji mwenye upeo mdogo asipewe kuendesha kipindi kama hicho ili wasikilizaji wasipotoshwe