Watangazaji wa Star Tv mnaboa

Ila jamani sekta ya habari Tanzania ni janga kubwa sana kwa taifa letu, imefikia wakati mpaka wana habari wengi wanaendeshwa na Matukio! Kuna umuhimu mkubwa sana wa kukabiliana na hili mapema sasa otherwise tutajikuta pabaya sana hasa pale wana habari wanapokuwa wana mihemko inayovunja miiko ya maadili ya habari!!

Hilo la appearance kwa watangazaji wa Star TV kinachowabana na cheap labour, Mishahara ya Sahara media ni mibovu mno, Si ajabu wengi pale wanakopwa!!
 
Ni hatari Mkuu
 
Azam nao bado sana kwenye substance ya materials, wana FACILITY ila delivery na materials wanazokusanya kwa ajili ya kutujuza ni sun zero! Mfano yule mzanzibar hajui kichambua habari za magazetini.
Back to Star Tv: waache pia kuarika watu wenye matusi na mihemko.
 
Azam nawakubali tu kwa channels zao zinaonyesha quality nzuri kama Za HD, na wanastudio nzuri lkn upande wa kutangaza bado sana presenters wao masaa yote ni kuchekacheka tu hovyo hovyo
 
Azam
Channel ten
TBC
Star TV hawa ni bure kabisaaaaaaa
 
mmmhh!! kuna mama mmoja sijui anaitwa naaani looh !! tv yangu huwa inazima akitokea 😀
 
Muulizeni mmiliki wa Sahara Media Group Pesa yetu ya EPA alisharudisha na yeye ni jipu muda haujafika tu lazima atumbuliwe.
 

Kabla hujawanyooshea kidole hao startv jiulize huko kazini kwako unatimiza majukumu yako sawasawa au na nawewe kimeo.

Nachojua watz tulio weng tuna tatizo kubwa la kutopenda kazi zetu unafanya tu bora liende na ni mahodari wa kudai haki huku tukijua hatutimiz majukum swsw. Na hii ni hulka yetu (ukatae ukubali) na ipo kotekote si sekta binafsi wala serikali,sema kinachowaokoa sekta binafsi kuna ufatiliaji zaid.

Hapa nina hasira sn kuna taasis nawatafuta kwa sim toka jana sim zao zinaita wala hazipokelewi nalazimika kwenda fizikali na ni mbali!!!
 
Hii channel imedorora sana baada ya kuibeba CCM kwenye uchaguzi mkuu.
 
mi wananichoshaga tu kwenye habari za kimataifa tu yaan,utasikia mara ooh waasi wa houth huko mshariki mwa ukraine..wakati waasi wa houthi wanapatikana yemen..mara siku nyingne badala ya kutaja umoja wa ulaya wanasema umoja wa mataifa wakati habari kuhusu EU...afu utakuta mtu anarudia mara nyingi tu sa sielewi hizi habari watoaga wapi yani..mara waasi wa houth wa syria..sasa cjui houth wenyew wanajua ni kitu gani eti ya kwe international news wanazinguaga tu wa TZ weng hawana mpango nazo
 
ndomana
 
Unawaonea hao jamaaa TV gani hapo bongo watangazaji wako juu sana? Star TV wako vizuri sana
 
Star wako vizur ni chuki na wivu Wa kike maswali kwa mleta hoja hadi kuja na Uzi huu sio kuwa uliwatazama kwa bahati mbaya maana yake unawafuatilia acha hizo unajua kuvaaa vizur wewe?
 
Star tv mtangazaji mwenye ufahamu ni mmoja tu, yule jamaa anaeitwa dotto bulembo
 
Umewaonea starv, kwene vituo vingi vya redio na tv suala la umakin ni mdogo sana hasa kwenye usomaj wa habar. Inatokea mara nyngi unakuta mtangazaj anajisahau na kusoma kitu tofauti na kinavyotakiw kusomwa, picha kutofautiana na habari.

Wale watangazaj wa zamani wa RTD ndo walizingatia sana umakini kwenye kusoma habari lakin hawa wa leo wengi wao sio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…