Watambue wezi wa Malima

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078

Picha tatu juu ni baadhi ya watuhumiwa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi.
Bunduki na begi la Mhe Malima.

Hoteli ya Nashera lilipotokea tukio hilo la wizi.
 
Jamani hili sio gobore hili? Mbona huyo Kamanda wa polisi alisema alikuwa na bastola tu
 
masikini Watanzania wasio na hatia wakiwa wamefungwa pingu!

Lakini Polisi wajue kuwa katika vitu vibaya kabisa ni pale wananchi wanapopoteza imani na jeshi hilo. Angalia siraha, jeshi na zana alizokuwa nazo Ghadafi lakini ukosefu wa busara unafanya nchi isambaratike. Wenye akili hawatawalaumu waliompindua Ghadafi bali watamlaumu Ghadafi kwa kupelekea hali hiyo.

Polisi wetu jifunzeni kabla ya kuingizwa katika michezo ya kisiasa na watu ambao wana tamaa zao za miili pamoja na familoia zao wala sio tamaa ya kuliendeleza taifa!
 
Nimeona hapo katika maelezo ya Shigongo ni kwamba Malima aliibiwa na changudoa
 
ondoeni propaganda zenu hapa...mtu aibiwe na changudoa halafu mnatuonyesha picha za wezi wa tabora?!!!!
 
yuho ni bi mdogo wa malima na wanaume ni shemeji wa malima.
 
Kumbe ni shotgun, nilikuwa bado najiuliza sana ni G3, Rifle ama nini? Manake ilishapingwa kuwa haikuwa SMG. Ila nimeamini kuwa Naibu Waziri huyu ni mwindaji wa wanyama pori, si kawaida kubeba shotgun maeneo ya Moro, inawezekana alitembelea Mikumi.
 
Du hadi shigongo kakubali kununuliwa?? Hakuna mwizi wa kuacha bastola kati ya hao,hadanganywi mtu,chonde chonde machangudoa ni nomaaaaa!!!

masikini Watanzania wasio na hatia wakiwa wamefungwa pingu!

Lakini Polisi wajue kuwa katika vitu vibaya kabisa ni pale wananchi wanapopoteza imani na jeshi hilo. Angalia siraha, jeshi na zana alizokuwa nazo Ghadafi lakini ukosefu wa busara unafanya nchi isambaratike. Wenye akili hawatawalaumu waliompindua Ghadafi bali watamlaumu Ghadafi kwa kupelekea hali hiyo.

Polisi wetu jifunzeni kabla ya kuingizwa katika michezo ya kisiasa na watu ambao wana tamaa zao za miili pamoja na familoia zao wala sio tamaa ya kuliendeleza taifa!

Wakuu mbona kama kuna kitu cha ziada mnachofahamu kuhusu hili tukio?tujuzeni. Niliangalia kupitia ITV walisema dirisha lake lilivunjwa ndipo vitu vikaibwa,sifahamu zaidi.
 
Nitakuwa mtu wa mwisho kusadikishwa uongo huu, hakuna hapo hata mtu mmoja aliyekwenda hotelini kuiba tusifanyane watoto wadogo hapa.
Nimefanya kazi za tour operating kwa zaidi ya miaka 10, kwahiyo najuwa fika mahoteli yanafanyaje kazi zao, bunduki mteja huwa halali nayo chumbani isipokuwa bastora tu, bunduki unakabizi kwa porters kama wapo au reception unapewa tag kwa ajili ya utambulisho wa kuichukuwa utakapocheck out.

Hivi huu uonevu dhidi ya raia maskini utaisha lini? haiwezekani mtu muhasherati kama Malima aje kuwapotezea watu muda kwa kesi za kubambika wakati ni yeye Malima anapaswa kuhojiwa na vyombo vya dola kuhusu mienendo yake inayotia shaka! kuwa na bastora sawa ni self defence, je hiyo shotgun ni ya kazi gani yeye kwenye safari za kikazi, hapa nategemea kama kweli kuna tume ya maadili ya umma ninatalajia ianze kwa kumuhoji huyu bwana mipete Malima.
 
Mmh hii ina walakini,mahakama itende haki tu!wasije adhibiwa wale wasio na kosa
 
Haya mambo bana yanachekesha sana! Ati inasemekana kuwa hakuwa na short gun, ina maana Malima ni punguani, au mwenda wazimu, ilikuwaje the first time inaonyeshwa kwa TV alitaja vitu vilivyoibiwa na SG ilikuwamo!

Ati leo, mara hakuwa nayo!! Hii kitu ina maswali mengi zaidi ya majibu...
Ndo muendelezo wa wa-TZ kudanganywa...
 
Back
Top Bottom