Nitakuwa mtu wa mwisho kusadikishwa uongo huu, hakuna hapo hata mtu mmoja aliyekwenda hotelini kuiba tusifanyane watoto wadogo hapa.
Nimefanya kazi za tour operating kwa zaidi ya miaka 10, kwahiyo najuwa fika mahoteli yanafanyaje kazi zao, bunduki mteja huwa halali nayo chumbani isipokuwa bastora tu, bunduki unakabizi kwa porters kama wapo au reception unapewa tag kwa ajili ya utambulisho wa kuichukuwa utakapocheck out.
Hivi huu uonevu dhidi ya raia maskini utaisha lini? haiwezekani mtu muhasherati kama Malima aje kuwapotezea watu muda kwa kesi za kubambika wakati ni yeye Malima anapaswa kuhojiwa na vyombo vya dola kuhusu mienendo yake inayotia shaka! kuwa na bastora sawa ni self defence, je hiyo shotgun ni ya kazi gani yeye kwenye safari za kikazi, hapa nategemea kama kweli kuna tume ya maadili ya umma ninatalajia ianze kwa kumuhoji huyu bwana mipete Malima.