Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 4,783
- 14,975
Watalaamu wa masuala ya fedha na bajeti kutoka Tanzania, wakiongozwa na Kamishna wa Fedha za Nje katoka Wizara ya Fedha, Bw. Rishade Bade wanashiriki kikao hicho.
Agenda nyingine zitakazojadiliwa kwa kina ni pamoja na vyanzo mbalimbali vya fedha (resources mobilization) kwa ajili ya kugharamia miradi ya kikanda na utekelezaji wa uanzishwaji wa Mfuko wa Maendeleo wa Kanda (Regional Development Fund - RDF). Nchi 11 kati ya 16 za SADC ikiwemo Tanzania zimesaini mkataba wa uanzishwaji wa mfuko huo ambao utakuwa na jukumu la kugharamia miradi ya maendeleo katika kanda hiyo.
Kikao cha Kamati ya Fedha ni moja ya vikao vya utangulizi kuelekea Mkutano wa 47 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya hiyo utakaofanyika Machi 12 na 13. 2026.