Beeb
JF-Expert Member
- Aug 18, 2018
- 29,389
- 59,151
Mwanaume wangu anafanikiwa sababu ya juhudi zake binafsi + kumtegemea Mungu kwa kila Jambo..Vipi kwako dada yna2? Je mumeo anafanikiwa kwa sababu yako au ni juhudi zake tu? Ushawahi kuhisi kama siku ukiondoka atapiga hatua kubwa zaidi hasa kiuchumi kuliko alivyo sasa?
Nilimkuta tayari ana uchumi mzuri na Namshukuru Mungu tangi niwe kwenye mahusiano naye hajawahi kuyumba ile kusema kufilisika hapana..Kuna changamoto tu za hapa na pale ambazo huwa hazidumu Namshukuru Mungu kwa hilo..kwa hiyo hata Kama nikitoka Katika maisha yake hakuna kitakachobadilika kwake zaidi naamini atazidi kubarikiwa sababu ni mpambanaji Sana.