NECTA: Watahiniwa 1,168,649 kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2026

NECTA: Watahiniwa 1,168,649 kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi 2026

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
434
Reaction score
586
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza kuwa jumla ya watahiniwa 1,168,649 waliosajiliwa kutoka katika shule za msingi 20,019 nchini watashiriki katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2026. Mtihani huo wa kitaifa unatarajiwa kufanyika rasmi tarehe 9 na 10 Septemba 2026 kote nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said A. Mohamed, alibainisha kuwa kati ya watahiniwa wote waliosajiliwa, wavulana ni 531,467 sawa na asilimia 45.48, huku wasichana wakiwa 637,182 sawa na asilimia 54.52.

Aidha, takwimu zinaonyesha kuwa watahiniwa 1,081,204 (asilimia 92.52) watafanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili, wakati watahiniwa 87,445 (asilimia 7.48) watafanya kwa lugha ya Kiingereza. Mtihani huu utajumuisha pia watahiniwa 4,867 wenye mahitaji maalumu, ikiwa ni pamoja na wasioona, wenye uoni hafifu, uziwi, ulemavu wa akili na viungo.

Elimu ya Msingi siyo jambo la muungano.
Lakini anayeizungumzia ni Mzanzibar
Nchi ngumu sana hii
 
Kumbe English medium ni elfu 84 tu!
Kumbe ni wachache kiasi hiki?
 
Baraza la mitihani la Tanzania-NECTA limetangaza kuanza kwa mtihani wa kumaliza elimu ya msinga utakaofanyika September 9 hadi 10, 2026 ambapo watahiniwa milioni 1 na 168 elfu 649 wamesajiliwa kufanya mtihani huo huku wavulana wakiwa ni laki 531 elfu 467 sawa na asilimia 45.48 na wasichana wakiwa ni laki 637 eflu 182.

Akitangaza Jijini Dar es salaam kuanza kufanyika kwa mitihani hiyo Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Mohammed amesema katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi jumla ya masomo sita yatatahiniwa ambayo ni kiswahili, english language,hisabati, sayansi na teknolojia, maarifa ya jamii na stadi za kazi pamoja na uraia na maadili.

Aidha ameeleza kwamba maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani pamoja nyaraka zote muhimu zinazohusu mtihani huo katika mikoa yote ya Tanzania bara huku akitoa wito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha kuwa usalama wa vituo vyote vya mitihani unaimarishwa na kwamba vituo hivyo vinatumika kwa kuzingatia sheria, taratibu ,kanuni na mwongozo uliotolewa na NECTA.

Aidha Baraza la mitihani la Tanzania-NECTA limewaomba wadau wa elimu na wananchi kutoa ushirikiano wakati wa uendeshaji wa mtihani ili watahiniwa wote wafanye mtihani katika hali ya utulivu lakini pia amewataka kutoa ushirikiano katika kudhibiti vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2026
SaveClip.App_800826197_18477370333117467_731139982586958812_n.jpg
 
Ila hizi takwimu zina fikirisha sana, hao milioni moja na laki watakao bahatika kupata kazi 2036 hawafiki elfu moja , sijui hao vijana milioni kuanzia 2030 watakuwa wanafanya nini ikiwa hali ni ngumu kiasi hiki?

Ukifikiria sana hali ilivyo uzazi ni mgumu sana aisee.
 
Back
Top Bottom