Wataalamu wa uvuvi kupata ajira kimataifa

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1590149238471.png

WATAALAMU wa vyombo vya uvuvi nchini wataanza kuajiriwa kitaifa na kimataifa, baada ya Bunge kuridhia mkataba wa kimataifa wa viwango vya mafunzo na utoaji vyeti kwa wafanyakazi wa vyombo vya uvuvi wa mwaka 1995

Mawasiliano, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani, alisema kuridhiwa kwa mkataba huo kutaleta manufaa tisa kwa taifa. Dk. Kalemani alisema kwanza utatoa fursa za ajira za ndani na za kimataifa kwa wataalamu wa vyombo vya uvuvi.

Alisema pia kutahakikisha kuwapo kwa ukaguzi wa waangalizi wenye weledi ambao kuwapo kwao kutahakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari. “Kutaimarisha vyuo vya ndani vya mafunzo ya uvuvi na kutambulika kimataifa, kuwapo kwa viwango bora vya ufundishaji wa wanafunzi katika vyuo vya uvuvi nchini,” alisema Waziri Kalemani.

Alisema kuidhinishwa kwa mkataba huo kutaimarisha usalama wa wafanyakazi katika vyombo vya uvuvi na hivyo kupunguza ajali. “Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1994, kazi ya uvuvi ilionekana kuwa ni kati ya kazi hatari duniani kwa kusababisha wastani wa wavuvi 24,000 kupoteza maisha kila mwaka. Idadi hii ni zaidi ya mara 10 ya vifo vinavyotokea katika meli za biashara,” alisema Waziri Kalemani.

Alisema mkataba huo pia utawezesha kuimarika kwa ulinzi, usalama na uhifadhi wa mazingira ya bahari pamoja na kuimarisha kwa upatikanaji wa takwimu na taarifa mbalimbali katika sekta ya Waziri Kalemani alisema baadhi ya madhara yanayoweza kutokea iwapo mkataba huo hautaridhiwa ni pamoja na Watanzania kutoajirika katika nafasi za kimataifa eneo la uvuvi wa bahari kuu, kinyume na wale wanaofanya kazi katika meli za biashara.

Alisema pia Tanzania itakosa nguvu za ukaguzi na uangalizi wenye weledi kwa meli za kimataifa zinazofanya kazi katika bahari kuu kwa ajili ya kuhakikisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari. Alisema kutasababisha kukosekana kwa usimamizi wa ulinzi, usalama na uchafuzi wa mazingira ya bahari, Tanzania kutoonekana kuwa eneo salama la kuvua samaki kwa kutofikia viwango vya kimataifa.

Alisema Tanzania itakosa mapato kutokana na kukosekana kwa ajira za Watanzania katika soko la kimataifa. Akisoma ushauri wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hawa Mchafu, alisema ni muhimu kwa serikali kuzingatia mikataba ambayo ni mizuri na yenye faida kwa nchi na kuiwasilisha bungeni ili kuridhiwa mapema na kuanza kunufaika badala ya kusubiri athari zitokee.

Alisema ni muhimu serikali iharakishe kuandaa sera ya bahari kwa kuwa ni muhimu hasa kama nchi inataka kuwekeza na kunufaika na uchumi unaotokana na bahari. Vilevile alishauri Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), kuimarishwa na kuboreshwa kwa kuhakikisha linakuwa na vitendea kazi bora na vyenye kukidhi viwango vya Taifa na kimataifa kwenye kufanya ukaguzi
 
Ngonjera zisizokuwa na manufaa kwenye nchi tumezochoka kwa waalimu wapi wa kufundisha kiwango cha kimataifa?
Au ndio wale tunaowalazimisha kuchukua kadi za mbogamboga?
 
View attachment 1456661

Mheshimiwa Hawa Mchafu kumbe alikuwa Naibu Mwenyekiti wa kamati ya Miundombinu, huyu alitakiwa atetee sana sekta ya bahari. Maana yeye anaijua na ametokea familia ya baharia Marehemu Mzee Mchafu.
 
Kikubwa inatakiwa tuwe na sera ya Taifa ya bahari, hiyo mikataba ya kimataifa mingine hata ikipitishwa usimamizi utakuwa mdogo na wataalamu watatosha.

Bahari hapa Tanzania imesahaulika sana, wakati inaweza ikaleta mapato sawa au zaidi ya madini.

Raisi akijua namna gani tunapoteza mapato kupitia bahari anaweza akasikitika sana.
 
Back
Top Bottom