Wataalamu wa sheria za kazi wanisaidie hapa

proxy

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
1,468
1,329
Ninahitaji kuwa na mtu/ binti atakayesaidia shughuli ndogondogo kama vile usafi , kutumwa posta na kwingineko .

Atakuwa anakuja asubuhi muda wa kufungua ofisi na anaondoka muda anaomaliza majukumu ya usafi.

Je, ni mkataba wa aina gani natakiwa kuingia nae ili isije nisumbua baadae?

Kumbuka sitaki kumwajiri.
 
Mkatabata wa muda mfupi mkuu

Kuna aina tatu za mikataba kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini, aina hizo ni;
1. Mkataba wa Kudumu - Permanent and Pensionable
2. Mkataba wa Muda Maalum, na
3. Mkataba wa Kazi Maalum.
Mkataba wa kudumu ; mwajiriwa anakuwa wa kudumu hadi muda wa wake wa kustaafu kama hatapata shida ya kinidhamu.
Mkataba wa muda maalum; mtumishi anapewa mkataba kwa mfano miezi mitatu na ikiisha basi ajira imeisha.
Mkataba wa kazi maalum; mtumishi anapewa mkataba wa kazi maalum na hiyo kazi ikiisha basi na ajira imeisha. Hapa mfano ni kama unampa mtumishi kazi ya kujenga ama kufyeka eneo fulani, kazi hiyo ikiisha na ajira inaisha.
Sasa kwa case yako hapo naona unaweza kutoa mkataba wa muda maalum ambao utakuwa unaongezwa bila kuvunja sheria.
 
Back
Top Bottom