Nawezaje kumsaidia Mwanamke anayefanya kazi baa na pia anajiuza?

Ridhwani Mbaraka

JF-Expert Member
Jun 18, 2017
484
1,135
Nimetembea mikoa kadhaa na nimeona mengi ya aina hii. Lakini kusema ukweli nilipofika Wilaya moja ya mkoa wa Kusini nilikutana na Mwanamke mwenye umri wa wastani wa miaka 28 hivi anaeonekana anajitambua na ana malengo.

Nilimhoji, nikaelewa kuwa ni mgeni maeneo hayo ametokea mikoa ya Kaskazini. Na kwamba ana mtoto mmoja lakini pia ni first born katika familia yao iliyo na kipato kidogo kutokana na Baba kutekeleza familia.

Katika maelezo yake anasema kwao wanajua yuko wilaya hiyo lakini hawajui kama anafanya kazi hiyo. Wakati mwingine unamkuta ana njaa, mie nampa pesa ya kula..Nilifanya hivi karibia siku tano lakini kilichotokea ni yeye kunishangaa.

Anamuuliza yule Chief/Mpishi kwamba inakuaje mimi namnunulia chakula na kuongea nae sana lakini hata namba ya simu simuombi. Next day akaniomba namba kwakua tayari tulikua tumezoeana kiasi. Ulipofika usiku wa saa tano akanipigia simu kuniambia anakuja, nikamwambia ninahitaji kuongea nae kirefu na kwamba muda huo mimi nilikuwa nimechoka na ninahitaji kupumzika ila atafute nafasi nyingine na hasa siku atakazokia mapunziko.

Kwa bahati mbaya muda huo hakuupata, nililazimika kufata muda wake ambao ni kuanzia saa SITA. Alikuja kikazi, tukalala alfajiri ya saa 10 akaondoka kurudi geto kwao. Nilijaribu kuongea nae na kuendelea kumdadisi akawa anaendelea kuongea yanayomhusu. Kubwa ni malengo yake ya kutafuta mtaji wa kufungua duka la nguo Dsm au Arusha.

Muda wangu wa kukaa eneo hilo ukawa umeisha natakiwa kusafiri. Nikamwambia nitabeba majukumu kadhaa ili mshahara na tips zako uendelee ku-save. Nikamlipia chakula cha siku 10 65,000/ kwa makubaliano kila baada ya siku 10 nitamtumia.

Nikasafiri, akaniunganisha na mama yake mzazi na wakati huo kulikua na harakati za mdogo wake kumpeleka form five. Hawakuwa na uwezo huo lakini mimi nililazimika kumtumia mama yake laki 2. Mtoto akapelekwa shule.

NILIAMUA kufanya utafiti binafsi ili nijue ni mzoefu au ni kweli kafika ulimwengu ule kutokana na shida za familia? Vijana niliowapa kazi ile walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa. Ikabainika kwamba ile ni kazi kwake na muda anaoutumia ni huo (Kati ya saa 7 usiku na 10Alfajiri)

Malipo ambayo analipwa na wateja ni wastani wa 30,000/

Taarifa zilikusanywa kwa siku tano na zoezi likawa endelevu. Sikumsanua bali nikaona niongeze ahadi za kutimiza ile ndoto yake ili nione anaweza kutoka kwenye huo ulimwengu. Nikaanza kumsaidia vile vitu alivyoniambia vinamsumbua zaidi hasa Kwa mama yake na mtoto. Lakini hakupunguza chochote, badae nikamtengenezea formula ya kupata mtaji anaoutaka kwa mwezi mmoja

Shida ikawa kuanza michakato ya kunifata hiyo formula ...huku kazi ya kumwangalia ikiendelea bila yeye mwenyewe kujua.

Mwisho nikagundua haya :
  1. Kweli anahitajika na familia kutatua shida za mama, nyumba yao inayohitaji matengenezo makubwa, kusaidia ndugu zake, mwanae na yeye mwenyewe.
  2. Kweli anahitaji msaada kwani hata afanyaje hawezi kupunguza mzigo alionao peke yake lazima apate MTU serious ili awe backup yake.
  3. Kutoka katika huo ulimwengu anataka lakini hawezi kwa sababu inaonekana imeshakua tabia. Kwamba hata siku ambayo hana mteja halali/anakua hapati usingizi mpaka around saa 11 alfàjiri. Na kwamba hata akifanikiwa kupata mtaji anaoutafuta bado atakua mtumwa wa kazi hiyo.
NB: Hii ndio imenifanya nije humu jamvini kuuliza kama zipo mbinu za kumchomoa mtu wa aina hii katika huo ulimwengu.

Let us be serious about this!

Kuokoa maisha ya samaki mmoja kwa kumrudisha majini Kati ya wengi walioachwa na maji kutokana na upepo mkali ni kulinda uzao kuliko kudhani ni kupoteza muda.

FB_IMG_1693748789107.jpg
IMG-20220823-WA0031.jpg
 
Nimetembea mikoa kadhaa na nimeona mengi ya aina hii. Lkn kusema ukweli nilipofika Wilaya moja ya mkoa wa Kusini nilikutana na mwanamke mwenye umri wa wastani wa miaka 28 hivi anaeonekana anajitambua na ana malengo.

Nilimhoji,nikaelewa kua ni mgeni maeneo hayo,ametokea mikoa ya Kaskazini.
Na kwamba na mtoto mmoja lkn pia ni first born katika familia yao iliyo na kipato kidogo kutokana na Baba kutekeleza familia.
Katika maelezo yake anasema kwao wanajua yuko wilaya hiyo lkn hawajui kama anafanya kazi hiyo.
Wakati mwingine unamkuta ana njaa ,mie nampa pesa ya kula..nilifanya hivi karibia siku tano lkn kilichotokea ni yeye kunishangaa.
Anamuuliza yule Chief/Mpishi kwamba inakuaje mimi namnunulia chakula na kuongea nae sana lkn hata namba ya simu simuombi...Next day akaniomba namba kwakua tayari tulikua tumezoeana kiasi. Ulipofika usiku wa saa tano akanipigia cm kuniambia anakuja..nikamwambia ninahitaji kuongea nae kirefu na kwamba muda huo mm nilikua nimechoka na ninahitaji kupumzika ila atafute nafasi nyingine na hasa siku atakazokia mapunziko.
Kwa bahati mbaya muda huo hakuupata,nililazimika kufata muda wake ambao ni kuanzia saa SITA.
Alikuja kikazi,tukalala alfajiri ya saa 10 akaondoka kurudi geto kwao. Nilijaribu kuongea nae na kuendelea kumdadisi akawa anaendelea kuongea yanayomhusu. Kubwa ni malengo yake ya kutafuta mtaji wa kufungua duka la nguo Dsm au Arusha.
Muda wangu wa kukaa eneo hilo ukawa umeisha natakiwa kusafiri .. Nikamwambia nitabeba majukumu kadhaa ili mshahara na tips zako uendelee ku-save. Nikamlipia chakula cha siku 10 65,000/ kwa makubaliano kila baada ya siku 10 nitamtumia.
Nikasafiri ,akaniunganisha na mama yake mzazi na wkt huo kulikua na harakati za mdogo wake kumpeleka form five. Hawakua na uwezo huo lkn mm nililazimika kumtumia mama yake laki2 ..mtoto akapelekwa shule.

NILIAMUA kufanya utafiti binafsi ili nijue ni mzoefu au ni kweli kafika ulimwengu ule kutokana na shida za familia?
Vijana niliowapa kazi ile walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa ..Ikabainika kwamba ile ni kazi kwake na muda anaoutumia ni huo (Kati ya saa 7 usiku na 10Alfajiri) .
Malipo ambayo analipwa na wateja ni wastani wa 30,000/.
Taarifa zilikusanywa kwa siku tano na zoezi likawa endelevu.
Sikumsanua bali nikaona niongeze ahadi za kutimiza ile ndoto yake ili nione anaweza kutoka kwenye huo ulimwengu. Nikaanza kumsaidia vile vitu alivyoniambia vinamsumbua zaidi hasa Kwa mama yake na mtoto. Lkn hakupunguza chochote..badae nikamtengenezea formula ya kupata mtaji anaoutaka kwa mwezi mmoja . Shida ikawa kuanza michakato ya kunifata hiyo formula ...huku kazi ya kumwangalia ikiendelea bila yeye mwenyewe kujua.

Mwisho nikagundua haya :

1. Kweli anahitajika na familia kutatua shida za mama,nyumba yao inayohitaji matengenezo makubwa,kusaidia ndugu zake,mwanae na yeye mwenyewe.
2.Kweli anahitaji msaada kwani hata afanyaje hawezi kupunguza mzigo alionao peke yake..lazima apate MTU serious ili awe backup yake.
3.Kutoka ktk huo ulimwengu anataka lkn hawezi kwa sababu inaonekana imeshakua tabia. .Kwamba hata siku ambayo hana mteja halali/anakua hapati usingizi mpaka around saa 11 alfàjiri. Na kwamba hata akifanikiwa kupata mtaji anaoutafuta bado atakua mtumwa wa kazi hiyo.

NB; Hii ndio imenifanya nije humu jamvini kuuliza kama zipo mbinu za kumchomoa mtu wa aina hii katika huo ulimwengu.

Let us be serious on this!

Kuokoa maisha ya samaki mmoja kwa kumrudisha majini Kati ya wengi walioachwa na maji kutokana na upepo mkali ni kulinda uzao kuliko kudhani ni kupoteza muda. View attachment 2737698View attachment 2737699
Mpe hela asahau shida zake
 
Endelea kumpatia pesa atatoka tu katka biashara hiyo unafanya vizuri... Lakini lakini lakini demu wa chuga sio type yako jamaa utafilisiwa vyote ulivyonavyo au kukutoa uhai ukiingia kingi nakutakia kumtoa kwema ridhwani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakula chao pendwa ni Pesa na starehe zikiisha jiandae kisaikojia, alafu usiwe unapenda hivyo utakufa mdomo umekaa upande au utakufa ukiwa umekenua mimeno

Na ukifa yeye ikifika saa 6 mpaka 10 anaenda kusuguliwa kwa 30,000/- tu in short angalia ustaarabu wako umedandia mtumbwi wa vibwengo subiri upigwe na kitu kizito
 
Anaweza kubadilika ikiwa atapata mbadala WA kazi.


Maana inshu ni kazi.
Mpe mtaji,au fanya Kama unamwunganisha kuuza duka awe Kama mwajiliwa umpime ujue yukoje kiakili.
Wengi wanapitia wengi.
Kiukweli hakuna Binti anapenda kujiuza.
 
Kwanza inatakiwa uangalie kama anashaurika, ukimwambia jambo analifanyia kazi...
kuna dada wengine unaweza kushawishika kumsaidia lakini hakupi nafasi ya kukusikiliza, wakorofi, ukimuuliza kitu cha ukweli anakuwa mkali kama simba.
nenda nae pole pole, muite sehemu mkae hasa Jioni mueleze unavyokwazika na matendo yake, onesha kwa vitendo namna utakavyomsaidia kama kweli ataacha na kumrudia Mungu, mwambie asali sana kulingana na imani yake. kama ni muelewa lazima utaona mabadiliko makubwa sana
 
Mshikaji kadata Kwa muuza K duuh kunguru hafugiki.We mhudumie na masela wataendelea kumtumia kama kawaida.
Huku Lindi na Mtwara ni wengi ila huyo unaemsema mi no yake ninayo ni mweupe,mdogo mdogo ila kwao kanisa ni Mwanza.
 
Back
Top Bottom