Haki na wajibu kwa wafanyakazi wa kazi za ndani

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
HAKI NA WAJIBU KWA WAFANYAKAZI WA KAZI ZA NDANI.

[PLEASE USIACHE KUSOMA HAPA]

Kazi za ndandani ni kazi zinazofanywa ndani au nje ya nyumba.
Mfano: usafi wa nyumba, kufua, kupika, kulea watoto, kutunza mifugo nk.

Mfanyakazi wa kazi za ndani ni mtu yeyote anayefanya kazi za ndani, ndani ya uhusiano wa kazi.

Mfanyakazi wa kazi za ndani anazo haki za msingi na wajibu sawa na wafanyakazi wengine katika kazi nyingine.

Kumekuwa na wimbi kubwa la uvunjifu wa haki dhidi ya wafanyakazi wa kazi za ndani. Lakini pia nao wamekuwa wakishindwa kutimiza wajibu wao.

Uvunjifu wa haki na wajibu unatokana zaidi na mwajiri na mwajiriwa kutokujua haki na wajibu wao pamoja na mipaka ya kazi kisheria.

Wafanyakazi wa kazi za ndani sawa na wafanya kazi wengine, wanalindwa na Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Pia wanalindwa na sheria za kimataifa hasa, Mkataba wa Kimataifa wa Kazi za Ndani wa mwaka 2011. Mkataba huo unaitwa "DOMESTIC WORKERS CONVENTION, 2011 (No. 189).

Wafanyakazi wa kazi za ndani wapo katika mkundi makuu mawili.

1. Wafanyakazi wanaoishi na mwjiri wao majumbani.

2. Wafanyakazi wanaoishi nje ya nyumba wanayofanyia kazi. Yaani anaishi sehemu nyingine ila anakuja kufanya kazi na kuondoka.

"Hao wote wanatakiwa kulindwa kisheria kwa kuzingatia haki na wajibu wao katika kazi.

Kwanza kabisa Katiba inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kufanya kazi na kila mtu ana haki ya kupata malipo stahiki kuligana na kazi yake. Kama ilivyoandikwa katika ibara ya 22 na 23 ya Katiba.

Hivyo, kila mtu ana haki ya kufanya kazi za ndani.

Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini imeweka kiwango sahihi cha umri wa mtu kuajiriwa kufanya kazi.

Join us telegram: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓

Umri sahihi wa mtu kufanya kazi ikiwemo kazi za ndani ni miaka 18 na kuendelea. Lakini, mtoto chini ya miaka 18 kushuka chini hadi miaka 14 anaweza kuajiriwa kufanya kazi nyepesi. Kazi ambazo hazitaathiri afya ya mtoto, masomo na ustawi wake kwa ujumla.

Hakuna mtu anayeruhusiwa kumwajiri mtoto chini ya miaka 14. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 5(1)&(2) wa Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini.

WhatsApp: TANZANIA LAWYERS FORUM 🎓 No. II

Swali la kujiuliza,

Je, ni wangapi tunawaajiri watoto chini ya miaka 14 kutufanyia kazi za ndani?

Tatizo linaanzia hapo, watu wengi wamekuwa wakiwaajiri watoto wa dogo tena hata wenye umri wa miaka saba kama wafanyakazi wa kazi za ndani. Wengi huogopa kuwaajiri watu wenye umri kuanzia miaka 18 au 14 kama inavyoruhusiwa kwa kazi nyepesi wakihofia pengine watajihusisha kimapenzi na wake zao au waume zao lakini hawajui tu kwamba wanavunja sheria.

Kumwajiri mtoto chini ya umri ulioruhusiwa ni kosa kwani kunamnyima mtoto haki zake za msingi ikiwemo shule na ukuaji bora.

Swali lingine
Je, ni wangapi mnawapa mkataba wa kazi hao wafanyakazi wa ndani?

Mfanyakazi wa kazi za ndani anahitaji kupewa mkataba wa kazi unaobainisha makubaliano na masharti ya kazi mazuri na yenye kueleweka kulingana na sheria, miongozo, kanuni na taratibu za nchi. Kifungu cha 13 na 14 cha Sheria ya Ajira na Uhusino wa Kazi kinaweka hayo bayana. Hii ni sawa na Kifungu cha 7 cha Mkataba wa kimataifa wa Kazi za Ndani wa mwaka 2011.

Mkataba unatakiwa uoneshe
1.Jina la mwajiri na la mwajiriwa

2. Mahali pa kazi.

3.Aina ya kazi zitakazotakiwa kufanywa.

4.Kiwango cha mshahara.

5.Masharti ya kuvunja mkataba kwa mwajiri akitaka kumwachisha kazi mfanyakazi wake au kwa mwajiriwa akitaka kuacha kazi.

Ni lazima pawepo na muda maalumu wa kutoa taarifa juu ya kuacha au kuachishwa kazi.
Lakini wengi hawafanyi hivyo, utakuta mfanyakazi wa kazi za ndani anatoroka bila taarifa au mwajiri anamfukuza ghafra mfanyakazi wa ndani. Hiyo hairuhusiwi kisheria.

6. Mkataba pia uoneshe masaa ya kazi. Masaa ya kazi yasizidi masaa 12 kwa siku. Kifungu cha 19 cha Sheria ya Ajira na Uhusiano Kazini.

Mwajiri anatakiwa atambue kwamba kwa mfanyakazi wa ndani mwenye chini ya umri wa miaka 18 haruhusiwi kufanya kazi za usiku. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 20(2)(c) cha Sheria ya Ajira na uhusiano Kazini.

Wafanyakazi wa kazi za ndanj hawaakiwi kutengwa wala kunyanyaswa kwa namna yoyote ile. Wanatakiwa kufanya kazi katika mazingira mazuri na waishi katika mazingira mazuri. Kama ilivyobainishwa katika kifungu cha 5 na 6 katika mkataba wa kimataifa wa wafanyakazi wa kazi za ndani wa mwaka 2011.

Pamoja na haki hizo lakini mfanyakazi wa ndani anatakiwa kuzingatia wajibu wake wa kazi ikiwemo na kufanya yafuatayo.
1. Kuipenda, kuiheshimu, kuijali na kuithamini kazi yake.
2.Kufanya kazi zake kwa ufanisi na kwa weredi mkubwa.
3.Kutunza siri za mwajiri wake.
4.Kumuheshimu mwajiri wake na familia kwa ujumla.

Kazi za ndani zinatamburika kisheria na wafanyakazi wa kazi za ndani wanalindwa kwa mujibu wa sheria za nchi na zile za kimataifa.

"TAMBUA HAKI NA WAJIBU WAKO, KISHA FUATA SHERIA."

It's me
A Lawyer and LifeCoach
Mr. George Francis
Whatsap 0713736006
 
Ashura mwenyewe mfanyakazi wa ndani ukimwelezea haya mambo atakuangalia akibaki anasema hiiiiiiii baghoshaaaa
 
Back
Top Bottom