Wataalamu wa kiswahili ivi ili neno la muarobaini lina maana gani?

Mpigamsuli

JF-Expert Member
May 24, 2012
3,885
575
wana jf naomba mnipe maana ya hili neno la muarobaini kwa sababu nimekuwa nikilisikia likisemwa sana na watu
 
mpigamsuli .

mwarobaini = margosa tree, neem tree

Mwarobaini ni mti ambao huwa unatumika kwa kutibu magonjwa mengi ... watu wanadai unatibu magonjwa zaidi ya 40 ... ndio maana ukapewa jina la Mwarobaini.

Matumizi ya neno Mwarobaini katika kiswahili:

1.
Muarobaini wa mishahara hewa wapatikana .... SERIKALI inaandaa mpango wa kutumia programu mpya ya kompyuta kudhibiti mishahara isiwafikie watumishi hewa au waajiri kulipa mishahara mara mbili na wengine kulipa hata kwa watu waliofariki dunia.

2.
KATIBA mpya ijayo haitakuwa muarobani wa kutibu shida zote za wananchi kama viongozi hawatakuwa waadilifu na wazalendo kwa Taifa lao.

3.
Pinda ataka wadau wa elimu kutafuta muarobaini wa changamoto za elimu Tanzania


==

Sasa kwa namna neno linavyotumika ... inamaanisha ... kama kuna tatizo sehemu fulani basi litafutiwe dawa itakayolimaliza kabisa ... kama ukiumwa unakunywa mwarobaini ili kutibu zaidi ya magonjwa 40.

Basi na suluhisho ya tatizo fulani ni kupata njia nzuri ya kulimaliza kabisa ... (Mwarobaini)
.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom