waswana ni watu wa ovyo sana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

waswana ni watu wa ovyo sana

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Ballot, Feb 12, 2012.

 1. Ballot

  Ballot Member

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakati mwingine najiuliza hivi huku botswana nafanya nini mimi??kuishi na watu wanaonitia hasira kila siku nimechoka kabisa''jana nimepita mitaa fulani nikaona jamaa wanamchinja ngo'mbe yaani ni machinjioni''yaani ndugu zangu nilijuta kwa nini nilipita mitaa ile na kosa kubwa nilipaki gari yangu karibu na kushuhudia unyama wa hali ya juu kabisa''yaani ngombe wanaletwa halafu anapigwa kamba'yaani ile process ni unyama mtupu'ngo'mbe alikuwa analeta ubishi kidogo basi alipelekewa kisu cha jicho''hajakaa vizuri akapelekewa kisu cha jicho la pili'kwa ujumla hapo tayari ni kipofu'huo unyama na jinsi wanavyomchinja unyama unyama imenifanya nisilale jana lakini cha kushangaza waswana waliokuwwa wakiangalia walicheka sana na kuona kama ni kitendo cha kawaida'kwa kweli nyie watanzania ni wastaarabu sana kulinganisha na hawa
   
 2. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  mkuu ushafanya ziara pugu machinjioni ?
   
 3. k

  khalidfundi Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni dini gani hao?au freemasonry.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  hao jamaa utajiri wao si ng'ombe?
   
 5. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Inaelekea hao jamaa ni wenzio ila hamjuani ! Wakati wanamchinja walimtaja na kumshukuru nani ? Hapo sie ndo tutakula kuku tu au tuchinje wenyewe !
   
 6. Kabembe

  Kabembe JF-Expert Member

  #6
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 11, 2009
  Messages: 2,238
  Likes Received: 931
  Trophy Points: 280
  Uroho tu ndio unaowasumbua kwa kujihalalisha kuwa nyie ndo wachinjaji rasmi.
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  hahahahaahaaah loh....
   
 8. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tembea Ujionee Usiongoje Kuambiwa !! Duniani Kuna Mengi !!! Yote Yanakusubiri !!! POLE SANA
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Nguruwe pia hupigwa nyundo kichwani maana hana shingo
   
 10. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Ndo maana wahenga wanasema tembea uyaone
   
 11. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,645
  Likes Received: 1,437
  Trophy Points: 280
  hongera kwa kuishi uswana!
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  huko ni Makafiri jumla !
   
 13. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #13
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Siku hizi wana mbinu nyingi, mojawapo ni kumchoma mkuki wa moyo. Wako mabingwa wa kulenga moyo!
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Feb 12, 2012
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Watu wa ovyo tunao happa Tanzania.

  Madaktari wanagoma kwa sababu za msingi kabisa.
  Katibu mkuu wa wizara ya afya anaiita fani yao ni fani duni pia wao madaktari ni watu duni na matusi mengine mengi jambo linalo watia hasira zaidi na kuleta maafa makubwa kwa Taifa.Mgomo unafikia kileleni hali ni mbaya sana. serikali inasalimu amri na kukubali yaishe. watanzania wanyonge wanaumia na wengine kupoteza maisha. Blandina Nyoni bado anajiona mzuri kama kigori haoni udhaifu na ufu wake. Watu kama Blandin Nyoni ni watu wa ovyo siyo Watswana.

  Waziri mkuu anahutubia waandishi wa habari na kutoa maamuzi ya kienda wazimu. Anakuza madai madogo na kuadidimiza madai makubwa Huyu ni mtu wa ovyo kwa kila kipimo.

  Rais Kikwete anaondoka kwenda Ulaya kuhudhuria mkutano ambako anajibu maswali kuhusu mikakati ya maendeleo ya Tanzania ovyoovyo bila mwelekeo na kuonyesha wazi kwamba Yeye Rais Kikwete na serikali ya CCM ni watu wa Ovyo waliopo madarakani kwa uroho wa Fedha Ujuha na ulimbukeni. Hawana mipango yeyote ya kulikwamua Taifa letu ila wana mipango dhabiti ya kututafuna watanzanaia na kututia upya katika ukoloni mambo leo kwa hila zozote . Rias huyu huyu na Watu wake ni wa Ovyo kabisa hafai hata bure.

  Serikali inayoruhusu kila bidhaa fake kuingia Tanzania na kugeuza nchi Jalala hiyo ni serikai ya Ovyo.
  Kuna Bidha zinazo tengenezwa kutokana na mabki ya viwanda vya nchi zilizo endelea yenye sumu za mionzi na heavy metala kama Lead ambazo zinaingizwa Tanzania kutuangamaiza sisi na uzao wetu. Serikali yetu yote inakenua meno huku hali halisi ya afya na ustawi wa Mtanzania ikizidi kudolola kwa nguvu. Tuna watu wa ovyo kibao katika ngazi zote serikalini hadi Ikulu.

  Kodi ya Waswana unao waita wa ovyo ndiyo inayolipa mshahara wako.
  Fedha zao ndizo zinakufanya uwepo hapo na uishi maisha unayo ishi.
  Utaratibu wao ndiyo umekufanya uwepo hapo Botswana na usiwepo tanzania au Kongo

  Huku kwetu umekimbia Ushenzi na uovyo wa serikali yetu ya CCM na kuiona Botswana babu kubwa. Cha ajabu watswana unawaona wa ovyo kisa kuchinja ng'ombe huku wakimtoboa macho nchi yao unaiona babu kubwa.

  Hapa Tanzania kuna watu wanaoishi kwenye mahekalu ya nguvu sana fedha wametoa katika Mrdi wa Lishe ya watoto chini ya miaka 5.
  Kumtoboa ng'ombe macho si kitendo cha uungwana lakini kuiba fedha za uji na maziwa ya watoto ili umjengee hawala yako nyumba ya kukoga watu ni jambo ovyo na la kiuuaji. Watu wa ovyo wanao iba chakula cha watoto tunao hapa Tanzania.

  Watu wanaiba hata nyembe za wodi za akina mama. Ukitembelea wodi za Mwananyamala unaambiwa kupiti,a Tangazo ukutani linalosomwa na kila mtu kwamba ukija kujifungua uje na nyembe kabisa jambo ambalo ni matusi kitanzania . Huko Wizarani akina Blandina Nyoni wameiba fedha za nyembe ili wawanunulie Vijust wao magari ya kuwakoga vijana wengine wadogo kinamama wenzao.

  Viongozi wa serikali ya CCM, Maziri wabunge wanasimamia kuuza ardhi ya watu na kuwahamisha kwa nguvu wao na mifugo yao.
  wanauza hata meneo ya makaburi kisa Fedha Mamlaka na Ufahari.

  Sumaye akiwa waziri mkuu alishindwa kuwatetea Wahadzabe wa Arusha wasinyang'nywe ardhi yao na kupewa Kaburu wa Kiarabu.Hawadzabe wananyang'nywa ardhi yao ya asili ili apewe mgeni na waziri wa serikali ya CCM akusanye ngawila. Hata kwa vitendo hivi vya kinyama bado unadhani watswana ni watu wa ovyo.

  Lowassa amejilimbikizia fedha kupitia mradi wa Umeme wa Richmond. sasa anapita kila kanisa Tanzania na misikitini kuwarubuni wachungaji na mashehe kwa fedha za wizi ili mwaka 2015 achaguliwe kuwa rais wa Tanzania kw gharaa ya Giza. Huyu ni mtu wa ovyo.

  Spika wa bunge Anne Makinda naye yuko kwenye list ya watu wa ovyo.
  wabunge wengi wa CCM wako kwenye list ya watu wa ovyo.

  Kuna sehemu ya wananchi wa Tanzania nao pia wako kwenye list ya watu wa ovyo. Unapewa Khanga, Tshirt, kofia, Sahani ya pilau, nusu debe la Mahindi na elfu 10 kisha unamchagua fisadi. Unapewa laki mbili unashiriki kuiba kura na kuumpa ushindi Fisadi. Mtanzania unayeshiriki kuimarisha kiama chako mwenyewe wewe ni mtu ovyo.

  wewe Mtanzania unayeshangilia umaarufu wa Mafisadi na utajiri wao kwa faida ya ufukara na uduni wa maisha yako wewe ni lazima uwe mtu wa ovyo.

   
Loading...