Waswahili Walisema Ndoa........!???Cheki Hii!

kaka yako dhaifu

mkuu naomba niendelezee hapo ili ujumbe umfikie vizuri aliyeleta mada hii...familia dhaifu huzaa watoto wa kiume dhaifu ambao nao huoa wake dhaifu nao wake zao huzaa watoto dhaifu na mwishoni ni familia legelege.... Mwambie kaka yako ajifunze kwa baba yako..

Kwani babako nyumbani aliishi na ukoo wa mamako??

Na short cut ya wanawake wanaolea ukoo wao kwa waume zao ni kwenda kumuolea mke mwengine mtaa wa pili...

So braza wako kulala gheto kwa mshkaji ni upuuzi...mwambie apange chumba mtaa wa pili kisha amwoe rafiki wa mke wake ili awe na wake wawili nadhani bi mkubwa wifi yako wa sasa atatia disipilini...

adui wa mwanamke mwanamke mwenzie.
 
Hiyo nyumba ya nani? kaka au shemeji maana kama shemeji amejenga au kupanga, mpe pole kaka yako.
 
alaa kumbee sa ilikuwaje ukamshtua tb namna ile we mwanamume khaaaa leo hata lunch sijui kama ana hamu nayo
 
Lah! Huo msalaba aliotwishwa ni kabambe kweli. Ningelikuwa mimi ningepiga BAN wote siku ya pili yake tu.
 
Mi naomba nichangie mambo mawili:

1. Hili si tatizo la ndoa kama ndoa, ni tatizo la uelewa mdogo wa mke wa kaka yako wa namna ya kuihudumia familia yake na mapenzi ya upofu ya kaka yako. Uelewa mdogo na kushindwa kupima uzito wa mambo humpata yeyote aliye kwenye ndoa na asiye kwenye ndoa, hivyo si jema kila baya la ndani ya ndoa lionekana ni tatizo linalosababishwa na ndoa!!! Akili gani ya kumpenda kuhudumia ndugu mpaka unaitesa familia yako mwenyewe?

2. Hapo penye bold ndugu yangu maelezo yako wazi sana kuwa kaka yako haoni taabu na hiyo extended family na mzigo wa kuhudumia hiyo familia. Wewe na ndugu wengine ndo mnaona shida. Mi nakushaurini tu kwa kuwa kaka yako hana taabu ni bora msiiingilie hiyo ndoa, utakuja kuonekana kuwa una chuki na mke wa kaka yako au pengine unataka kubomoa ndoa ya kaka yako. Ndiyo maana mambo mnayomshauri anakwenda kumwambia mkewe mnaanza kuimbiana taarabu ....! Mwache akifunguka akili, atawatafuta yeye mwenyewe!

Kuna wimbo ulikuwa unaimbwa zamani unasema "bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wenyewe mpaka watakapo elewana, lakini usiwangilie eheeee, wakijapatana, utabiki na aibu weee mtoto wa mamaaa"

Mchuma janga hula na ndugu zake. Huyu mwanaume anapalilia umasikini, mwisho wake watoto wakifikia umri wa kudai ada ataanza kuwapiga mizinga ndugu zake, achilia mbali kwamba hana uwezo wa kusaidia ndugu yake hata mmoja. Baba yangu enzi zake (R.I.P) anakuja mchana kweupeee, atawatukana wewe na mkeo kwa muda wa masaa kama 2 halafu wote mtajua kwamba hamna akili kuanzia siku hiyo! hii style ndio inayofaa kujiepusha na matatizo mnayowekeza sasa!
 
Duuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!! npo tongue tied, kweli ndoa ndoano
 
hawa watu wa hili kabila ni kawaida yao kurundikana kwa ndugu na haijarishi huyo ndugu ana kipato cha kutosha au laah.

mimi na shangazi yangu kaolewa kwenye hilo kabila aisee nyumba yake ikiwa na watu wachache mpaka majirani wanashangaa ni watu 15.........ile nyumba inakuwaga na watu 30........tena mwingine anakuja na mke na watoto wake.......yani sijui wakoje.

Uvivu ndio sababu. Tena wakiondoka wanataka nauli. ukiwaendekeza, utaumia!
 
Back
Top Bottom