Waswahili Walisema Ndoa........!???Cheki Hii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waswahili Walisema Ndoa........!???Cheki Hii!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Majigo, Aug 13, 2012.

 1. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #1
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  NILOSIMULIWA.....

  poleni kwa majukumu na ninatumaini wote humu ni wazima, kwakweli ninajuwa kwamba kila binadamu anamatatizo yake lakini matatizo mengine kamwe
  hayawezi kuvumilika.

  Kaka yangu ameoa msichana wa kitanga, sio kwamba anauwezo sana hapana wanamaisha tu ya kawaida wanakaa kwenye nyumba yao ambayo ina vyumba viwili yani chumba na sebule, na wanawatoto wawili wote wa kike, baada ya mwaka wa ndoa wifi yangu huyu mama yao akafariki na baba yao alishafariki zamani sana kwahiyo yeye akiwa kama mkubwa akaamua kuchukua wadogo zake ambao ni wakubwa kuja kuishi kwao, wakati wanaweza tu kupangishiwa chumba kimoja labda na msaada wa kazi na maisha yakaendelea.

  Japo wanapata tabu maana inabidi sasa wale wadogo wa wifi yangu walale sebuleni...yaani nyumba ukiingia sebleni kuna mabegi ya nguo, magodoro yani sio sehemu unayotaka ukae upumzike baada ya uchovu, kaka yangu wakigombana na mkewe ndio anaona kama wale kuwa pale ni tatizo lakini kama hawajagombana wewe kama ndugu ukimwambia anaenda kukusemea kwa mkewe basi utafumbiwa taarabu mkikutana kwenye shughuli mpaka uchoke.

  Jumapili iliyopita kaka yangu akanipigia simu kwamba ametoka kazini kufika nyumbani akakuta
  ugeni, na vitu nje yani kama kuna chumba ki wazi kimepata wapangaji, alipomuuliza mkewe vipi mke wake akamjibu mtoto wa mama yangu mdogo kapata matatizo kwenye nyumba aliyopanga ndio amekuja hapa mpaka atakapopata nyumba ya kuhamia!!!!!! na huyo dada yake anawatoto saba, jumlisha wale wadogo wa mkewe tisa, na mkewe na mume kumi na moja, pamoja na watoto wawili kumi na nne, jumlisha mjukuu wa dada (mtoto wa yule dada mmoja anamtoto) kumi na tano wote hao wanaishi kwenye chumba
  kimoja na sebule!!!!!!!!!!!! imebidi sasa kaka yangu awe analala kwa rafiki yake apishe watu waweze kulala mpaka chumbani kweli hii ni haki???????
  Ndoa ndio inavyotufundisha hivi jamani?
  kisa umeoa ndio ubebe msalaba kiasi hiki???
  kweli hii ni akili ya mtu kweli ama kuna mengine hapo yamechovewa????
  Ari ile inamkera kila mtu lakini kaka yeye amekaa tu kimya hana la kufanya, nyumba yake mwenyewe kushinda anaiona chungu
  kutwa anashinda kwa marafiki zake jioni ndio anarudi kula halafu aondoke akalale.

  Kweli ndoa sio mchezo wa kuigiza!!!!.
   
 2. S

  Starn JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 400
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama ningekuwa ni mimi kuanzia wadogo zake na hao wageni wapya wote wangecheza gwaride mguu kushoto kulia gwaride songa mbele mpaka kijijini kwao.
   
 3. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  hahahahahahah!
  tena Na Mwendo wa Hli Life!?
   
 4. r

  rtha New Member

  #4
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 3, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Da! yakweli hayo? Mwe! Huruma huzaa dhambi mwambie huyo kaka ako.
   
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Aug 13, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  The guy should act like a man
  Sioni kwa nini akalale kwa majirani
  Anatakiwa kuwaonyesha hao ndugu kwamba hakuoa ukoo..
  Kitendo cha kuhama mjii ni udhaifu!!
   
 6. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #6
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  ya kweli Kabisa Tena Hata mtaani Kwenu Yanasibu.
   
 7. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Imetulia Kaka!
   
 8. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #8
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  hahahahahahahahahahaha......................kweli kuna haja ya kupigania katiba
   
 9. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  una Maana Gani Mkuu!
   
 10. d

  dandabo JF-Expert Member

  #10
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  hizo ndio sifa hasi za kuoa mkoa wa tanga! Jamaa yangu ilimlazimu kutoa talaka. Alipomuoa huyo binti wa kitanga alijikuta anafamilia kubwa ajabu!
   
 11. NyotaMalaika

  NyotaMalaika Senior Member

  #11
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 6, 2012
  Messages: 153
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Huyo mwanamke hayuko serious....
   
 12. sister

  sister JF-Expert Member

  #12
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  na hao watu hawana aibu wanaona nyumba yenyewe ndogo lakini wataendelea kulazimisha tu kuishi hapo.
  ndo wakati wa huyo mume kuonyesha uanaume wake aache kuwachekea.
   
 13. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #13
  Aug 13, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Mi naomba nichangie mambo mawili:

  1. Hili si tatizo la ndoa kama ndoa, ni tatizo la uelewa mdogo wa mke wa kaka yako wa namna ya kuihudumia familia yake na mapenzi ya upofu ya kaka yako. Uelewa mdogo na kushindwa kupima uzito wa mambo humpata yeyote aliye kwenye ndoa na asiye kwenye ndoa, hivyo si jema kila baya la ndani ya ndoa lionekana ni tatizo linalosababishwa na ndoa!!! Akili gani ya kumpenda kuhudumia ndugu mpaka unaitesa familia yako mwenyewe?

  2. Hapo penye bold ndugu yangu maelezo yako wazi sana kuwa kaka yako haoni taabu na hiyo extended family na mzigo wa kuhudumia hiyo familia. Wewe na ndugu wengine ndo mnaona shida. Mi nakushaurini tu kwa kuwa kaka yako hana taabu ni bora msiiingilie hiyo ndoa, utakuja kuonekana kuwa una chuki na mke wa kaka yako au pengine unataka kubomoa ndoa ya kaka yako. Ndiyo maana mambo mnayomshauri anakwenda kumwambia mkewe mnaanza kuimbiana taarabu ....! Mwache akifunguka akili, atawatafuta yeye mwenyewe!

  Kuna wimbo ulikuwa unaimbwa zamani unasema "bibi na bwana wakigombana nyumbani, waache wenyewe mpaka watakapo elewana, lakini usiwangilie eheeee, wakijapatana, utabiki na aibu weee mtoto wa mamaaa"
   
 14. sister

  sister JF-Expert Member

  #14
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,026
  Likes Received: 3,932
  Trophy Points: 280
  hawa watu wa hili kabila ni kawaida yao kurundikana kwa ndugu na haijarishi huyo ndugu ana kipato cha kutosha au laah.

  mimi na shangazi yangu kaolewa kwenye hilo kabila aisee nyumba yake ikiwa na watu wachache mpaka majirani wanashangaa ni watu 15.........ile nyumba inakuwaga na watu 30........tena mwingine anakuja na mke na watoto wake.......yani sijui wakoje.
   
 15. s

  sambestman Member

  #15
  Aug 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kaka yako dhaifu
   
 16. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #16
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  haaaaaaaaaaaaaaa hayuko serious namna gani,yuko serious ndo maana kawaleta wakazi ili kuongeza ulinzi shirikishi
   
 17. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #17
  Aug 13, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  inatakiwa ujue wakoje,coz ukisema hujui utakuwa unalalmika kila cku
   
 18. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #18
  Aug 13, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,033
  Trophy Points: 280
  sasa huyo kaka yako anafaidi chakula cha ndoa saa ngapi....?..
  inaudhi sana lakini.....
   
 19. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #19
  Aug 13, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,188
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Fukuza kuanzia dada mtu , mama mdogo na wadogo zake timua. Kauli mojatu KAMA SIO MKE WANGU NA SIO MTOTO WANGU SITAKI KUKUONA UNANG'AA SHARUBU HAPA KWANGU........
   
 20. d

  dandabo JF-Expert Member

  #20
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 303
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Mimi nimeishi tanga. Hilo kabila ni balaa usijaribu utakufa na stress!
   
Loading...