Waswahili tuna vijimisemo..!!

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
353
1.Gari la kuvutwa hali overtake.
2.Hata uwe na bahati vipi hauwezi kuokota nyumba.
3.Mganga wa jadi haagizi tembele.
4.Wimbo wa taifa haupigwi disco.
5.Kandambili haipigwi kiwi
6.Usiteme Big G kwa karanga za kuonjeshwa.
7.Hata bibi alikuwa binti.
8.Mke wa mtu sumu, mume wa mtu maziwa.
9.Kipara bila pesa ni KOVU.
10.Mbwa hanenepi miguu
11.Picha ya Rais haina bodyguard.
12.Mjini shule kijijini tuition.
13. Uzuri na shepu mjini, Heshima kijijini
14.Mjini heshima pesa, shikamoo makelele.
15.Silaha pesa, kisu na bastola mizigo.
16.Kuku ni kuku jogoo jina tu
17.Kusoma kuelewa kukesha mbwembwe!
18. Urefu na ufupi ni majaliwa ya Mungu, unene na wembamba ni juhudi binafsi

TUPIA INGINE MUPYA ZAIDI KAMA UNAYO...
 
Makonda nao....

Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
Konda; Yesu bado hajatoa albam.

Matozi; humu ndani joto
Konda; kapande friji

Abiria; kuna siti?
Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?

Sistaduu: Konda unanibana
Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!

Mama: sikai siti za mwisho
Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?

Abiria : we konda vipi kuwa kama umeenda shule
Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule
 
Makonda nao....

Mlokole; konda weka nyimbo za Yesu
Konda; Yesu bado hajatoa albam.

Matozi; humu ndani joto
Konda; kapande friji

Abiria; kuna siti?
Konda; Kwani hawa walioko wamekalia madumu?

Sistaduu: Konda unanibana
Konda; hiyo suruali inakubana mbona husemi!

Mama: sikai siti za mwisho
Konda; Kwani hizo siti za mwisho ziko nje ya gari?

Abiria : we konda vipi kuwa kama umeenda shule
Konda: Mimi ndiyo kwanza nimetoka shule

lazima atakuwa konda wa mbagala kariakoo
 
mkuu jina lako linanikumbusha machame kwetu kuna mfereji unaitwa, mfongo wa nsungu.
Nimepiga A level Umbwe, tulikua tunachapa lapa hadi mitaa ya Machame kufata totoz, huku unavuka mito na mabonde mengi tu, afu ukifika huko shuleni kwao uko hoi hata mate hupati!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom