Wasukuma wanaoendelea kufanya hizi mila za kimabavu zilizopitwa na wakati wapewe kesi za ubakaji, mabinti waheshimiwe.

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Hata wasukuma walioelimika waliachana na utamaduni huu lakini kuna baadhi ya maeneo bado unaendelea kwa kisingizio cha kudumisha mila,

Kuna baadhi ya maeneo ya wasukuma bado elimu ya kuachana na haya mambo haijafika kikamilifu, unawakuta wachungaji wa kisukuma wamevaa mavazi yao ya asili sketi za mashuka na gum boots za shambani, wamemuona binti wanamzingira ili aolewe kimabavu.

Kama binti amekuvutia ongea nae, haya mambo ya kutumia mabavu kwa karne hii ni mambo ya ajabu sana

Kama binti umempenda binti ongea nae, Sio kuanza kutumia nguvu kama jogoo
Una uhakika na unachokisema?

Hao kwenye video yako ni waigizaji wa Tik Tok wanaigiza ili wapate viewers.

Niko huku Misungwi kijijini ndani ndani huku na hakuna kitu kama hicho. Na natembea sana vijijini kwenye ngoma za kienyeji (mbina) na hayo mambo hayapo.

Watoto wa kike inabidi wasome wewe leo umkamate kisa Chagulaga mbona utapigwa mvua 30 hivi hivi unajiona?

Hayo ni mambo ya zamani miaka ya 80 huko wakati mvuvumko wa elimu na utii wa sheria ukiwa bado mdogo.

Na usiamini kila kitu unachokiona mitandaoni. Watu wako tayari kufanya cho chote ili kupata views!
 
Wasukuma wametapakaa kuna baadhi ya maeneo wasukuma walielimika waliachana na haya mambo lakini bado kuna maeneo haya mambo bado yapo;

Haya mambo yanaendelea sio uigizaji ni uhalisia, Hawa ni wasukuma wanaoishi halmashauri ya mpimbwe
 
Mpimbwe ni wapi?

Maana ni suala la kuwasiliana tu na mkuu wa wilaya pamoja na Ofisa Elimu wa Wilaya basi tatizo kwisha!

Nazunguka sana vijijini mkoa wa Simiyu, Mwanza, Shinyanga pamoja na Geita na sijaona kitu kama hicho.

Kama bado hii inatokea basi ni remnants tu maana kufuta mila kabisa kabisa wakati mwingine ni kazi ngumu ndiyo maana kila kabila ukifuatilia vizuri utakuta kuna mila ambazo pengine haziendani na wakati lakini bado zinafuatwa - japo kwa kiwango kidogo..
 
Hili suala pengine limekuuma ila suluhisho sio kutetea kwamba halipo, ni kweli ni mambo yanayotia aibu hasa ukiwa unahusiana na watu hao aidha kwa kabila, undugu, eneo, n.k. ila suluhisho la kuondokana na hii aibu sio kukana bali waelimishwe.

Hawa ni wasukuma wanaoishi halmashauri ya mpimbwe, kibaoni, majimoto na vijiji vinginevyo,
 
Hata wasukuma walioelimika waliachana na utamaduni huu lakini kuna baadhi ya maeneo bado unaendelea kwa kisingizio cha kudumisha mila,

Kuna baadhi ya maeneo ya wasukuma bado elimu ya kuachana na haya mambo haijafika kikamilifu, unawakuta wachungaji wa kisukuma wamevaa mavazi yao ya asili sketi za mashuka na gum boots za shambani, wamemuona binti wanamzingira ili aolewe kimabavu.

Kama binti amekuvutia ongea nae, haya mambo ya kutumia mabavu kwa karne hii ni mambo ya ajabu sana

View attachment 2872757
Hakuna mila hizo kwa sasa! Usidanganye watu!
 
😂😂😂😂Weeeeh haya mie ntaenda kwa mababu zangu nione hiyo chagulaga
 
Hili suala pengine limekuuma ila suluhisho sio kutetea kwamba halipo, ni kweli ni mambo yanayotia aibu hasa ukiwa unahusiana na watu hao aidha kwa kabila, undugu, eneo, n.k. ila suluhisho la kuondokana na hii aibu sio kukana bali waelimishwe.

Hawa ni wasukuma wanaoishi halmashauri ya mpimbwe, kibaoni, majimoto na vijiji vinginevyo,
Liniume tena? Kwa nini liniume? Kwamba mimi ndiye mlinzi wa mila za Wasukuma ama?

Hapana mkuu. Kama umenisoma vizuri nimesema kwamba karibu kila kabila lina remnants za hizi mila ambazo tunaziona kuwa pengine zimeshapitwa na wakati. Hata kwenye kabila lako ukichunguza zipo tu mf. Ukeketaji!

Mbali na kushirikisha mamlaka, kuelimisha jamii husika pengine ndiyo njia sahihi zaidi japo kama mila ikifungamanishwa na ishu za ushirikina inakuwa ngumu zaidi kuing'oa.

Kama uko huko jaribu kuwasiliana na mkuu wa Wilaya na Ofisa Elimu ukiwa na ushahidi. Hata Waziri Gwajima ambaye yupo humu JF. Bila shaka hatua stahiki zitachukuliwa. Na jamii iendelee kuelimishwa....
 
Back
Top Bottom