Mimi ni Msukuma 110% na sijawahi kamwe kuusikia huo utamaduni.
Ni wa Wasukuma wa wapi labda?
Babu yangu ni Pacha,Baba yangu amefuata mapacha na mimi tumezaliwa mapacha na mdogo wangu wa kike,mashangazi zangu na dada zangu wengi tu wana mapacha,hii sherehe nishafanyiwaga,tena ziko mbili...ile mkiwa vitoto vidogo mama yenu hawezi akaenda ugenini akalala nanyi huko,mpaka mfanyiwe tambiko kidogo,zinachinjwa kondoo kulingana na jinsia yenu (kama ni wa kiume,kondoo atakua wa dume,km sivyo basi kondoo watakua jike na dume) watu wanakula.Kuna ngozi kutoka kwa wale kondoo mnavalishwa kama pete (watoto na mama yenu).Tambiko hilo likiisha basi mnaruhusa ya kulala ugenini.
Pia mtu akijifungua mapacha, kiongozi wa jadi wa kanda (Lugoye) atapiga Kalulu ili kujulishwa wanazengo wote (hii kalulu inaashiriaga majanga au mkosi,mfano ikinyesha mvua ya mawe,mtu kuzaa mtoto mfu au mtu kufa akiwa anazaa huwa wanapiga kalulu pia) hii "kalulu" huwa inapigwa afu mpiga anatamka neno "Boyo" then anataja jina la familia.
Kuzaa mapacha ilikua kama mkosi flani hivi kama alivyosema mwandishi,watoto wa mapacha tulikua tunafichwa sana tulikua tunajulikana kama "Basebu" ikiwa na maana wa "moto" ikimaanisha mapacha wanaweza kufa muda wowote na huwa wanafanyiwa matambiko sana.Kama ulisoma kitabu cha Things Fall Apart,kwenye kabila la akina Okonkwo mapacha walikua wanaitwa "Osu" na walikua dalili ya mkosi katika jamii na walikua wanatupwa porini.
Zamani usukumani mwanamke anayezaa mapacha alikua anaachwa....Natokea Bariadi,wilaya mpya ya Itilima....kwenye ukoo wetu akina saka (mtoto pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa wakati wa kuzaliwa au kufa baada ya muda mchache ni wengi sana.
Majina haya kwetu ni common
1.Kulwa-Pacha wa kwanza kutoka (mkubwa)
2.Doto - pacha wa pili kutoka (mdogo)
3.Kija- mtoto wa kwanza(kiume) kufuata mapacha
4.Hoja-Mtoto wa pili(kiume) kufuata mapacha
*Saka ni mtoto mapacha ambaye mwenzake hayupo (ashakufa) Maana ya neno SAKA ni "BAKI" Kwa hiyo SAKA ni pacha aliyebaki baada ya mwenzake kufa.
Kwa hiyo Nyani Ngabu wewe ni msukuma fake umeongea uongo,mimi ni mshosha ng'ombe halisi,Msukuma grade A,Mnyantuzu pure kabisa na natoka familia ya mapacha kutoka babu yangu hadi mimi.