Mbavu mbili
JF-Expert Member
- Apr 25, 2011
- 1,456
- 872
Habari, Naandika uzi huu kwa machungu makubwa! Mara nyingi huwa sipendi kuandika andika humu,
Mzeewangu alistaafu kazi katika shirika la reli la Tazara mwaka 2005-
ni miaka 11 mpaka sasa anafuatilia mafao yake pasipo mafanikio yoyote. Wazee hawa wana hali mbaya sana mitaani kwa sasa. Ombi langu kwa wahusika, muwasaidie wazee wetu hawa waliojenga reli hiyoo miaka ya 1970's na kulitumikia Taifa kwa uzalendo na weledi wa hali ya juu.
Binafsi, ninataambua juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kusimamia ustawi wa watumishi wake. Ninaomba wahusika waanze na hili, wawakomboe wazee wetu hawa ambao wamekata tamaa kwa hali ngumu ya maisha. Kuna wakati huwa najiuliza Wazee wetu hawa walimkosea nini Mungu?