SoC03 Wastaafu kuchelewa kupata mafao

Stories of Change - 2023 Competition

ASHA KAMATA

New Member
Jul 4, 2023
1
0
Kumekuwa na Malalamiko ya Wastaafu kutokupata Mafao yao kwa wakati huku sababu kubwa ikitajwa kuwa ni Waajiri wanachelewa kuwasilisha michango Kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na kusababisha kuchelewa kwa uchakataji Mafao ya wastaafu.

Licha ya kuwepo kwa sheria zinazotetea haki zao ikiwemo Sheria ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (2018) inayoelekeza mwajiri kuchangia 20% ya mshahara wa mfanyakazi katika Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF),ambapo asilimia 15 mchango wa mwajiri na asilimia 5 inakatwa kwa mwajiriwa..

Aidha sheria hiyo inaelekeza kila mwajiri,Serikali kuu,Serikali za Mitaa,Mashirika ya Umma,Taasisi na Wakala wa Serikali wanapaswa kuwaandikisha waajiriwa wao PSSSF mara tu wanapo waajiri.

Pia Kifungu cha 19(1) cha sheria hiyo kinaelekeza mwajiri ambaye atashindwa kuwasilisha michango ya mfanyakazi, atatozwa faini zilizoainishwa kulingana na muda wa ucheleweshaji.

Ripoti ya Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Mwaka 2020/21 inaeleza kuwa halmashauri 42 hazikuwasilisha bilioni 182.24/- kwa PSSSF (milioni 888.97/- ni michango, bilioni 181.35 adhabu). Kati ya fedha hizo,bilioni 180.7/- ni adhabu zilizotozwa halmashauri tano za Chato Sh. bilioni1.83; Jiji la Dodoma Sh. bilioni 56.81; Meatu Sh. milioni 578.74; Wilaya ya Nzega Sh. bilioni 117 na Mji Nzega Sh. bilioni 3.67.

Kutowasilisha michango kwa wakati, kunachelewesha mafao ya wastaafu na kufanya halmashauri kulipa faini.Hatahivyo halmashauri zipo kimya hazisemi chochote kuhusu kuchelewesha Michango ya watumishi.

Je, nini sababu ya kuchelewa?

Nani anawajibika katika hili?


MALENGO

1.kufahamu kwanini michango ya watumishi haikuwasilishwa kwa wakati?

2. Kufahamu nani anawajibika?

MATARAJIO

1. Michango ya watumishi wa umma inawasilishwa kwa wakati kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii ili wastaafu wasiwe wanachelewa kupata mafao yao na halmashauri kuepuka faini zisizo za lazima.

2. Hatua za kiutumishi na kisheria zichukuliwe dhidi ya waliosababisha michango ya watumishi kutowasilishwa kwa wakati kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

VYANZO VYA TAARIFA

-Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la dodoma

- PSSSF

-NSSF

-Wastaafu
 
Back
Top Bottom