Ni sheeedah....
1. Katika CCM Mzee wasira ndio kiongozi anayeweza kurudisha mshikamano na umoja ndani ya chama kwa kuwa hana makundi ya kisiasa.
2. Uadilifu wake ni sifa ya kiongozi tunayehitaji kwa sasa ili aweze kusimamia maendeleo ya nchi hii lakini pia kusimamia maadili ya nchi yetu ambayo yamepotoka kwa hali ya juu sana
3. Usafi wake dhidi ya ufisadi ndio silaha tunahitaji kwa kiongozi ajaye ili awe huru na jasiro kupambana na mafisadi na wala rushwa bila aibu kwani atakuwa hadaiwi na mtu na atakuwa hahitaji kumlipa mtu fadhira zozote.
4. Ujasiri wake ndio nguzo katika kutetea na kusimamia amani ya nchi yetu, hatakuwa legelege.
5. Uwezo wake katika masuala ya kiuchumi na mipango ndio tunachohitaji katika kuelekea katika uchumi wa gesi na jinsi ya kusimamia vizuri rasilimali za taifa katika kukuza uchumi.....
Mzee wasira ni mteteZi wa Taifa
Mzee wasira ni mtetezi wa Chama
Mzee wasira ni hazina ya Taifa
Akigombea uraisi atatufaa, tumuombee afya njema na umri mrefu.