Wassira: Nitagombea urais 2015

Hahahah watanzania pia wana vigezo vingine visivyo vya kisayansi kabisaaaaa hasa akina mama utasikia aaaaahhh JK anavutia aisee hasa akivaa suti mashaallah! ana mvuto.... kwa wagombea wazee wenzangu ka kigezo haka soooo
 
Umechambua mambo mengi kuhusu Wasira lakini kwenye kasoro zake naomba nikurekebishe kidogo.
Wassira ni kiongozi anaependa Siasa za Suluhu, na amekuwa mstari wa mbele kusuluhisha Migogoro ndani ya CCM NA Nje ya Chama, Migogoro ya Udini na Kuchinja aliimaliza yeye, CCM Mkoa wa Arusha kama Mlezi na mengine mengi ndani ya CCM amekuwa akiaminiwa na Wenzake kutatua na kusuluhisha.

Sasa huwezi kuwa Msuluhishi kama huna Subira, Subira,Uvumilivu na Kusikiliza ni part kubwa ya Moyo,Akili na Busara za Mtu yeyote anae tatua Migogoro.

Wassira Ana SIFA ya Uvumilivu na Subira, Uchapakazi na Muadilifu. Lug ha na Tone yake ni nzuri tu, kwani huyo ni Mtu wa Mara hata Nyerere alikuwa hivyo tu.

ukimsikiliza jukwaani lazima uelimike na utacheka sana na utashawishika kuwa upande wake kwa hoja tu.
 
"Lengo lake ni rufaa yake kusikilizwa ili
apewe ushindi ambao aliamini ndiyo haki
yake, hivyo apate fursa ya kukiwakilisha
chama chake (CCM) katika kuwania
ubunge Jimbo la Bunda kwenye Uchaguzi
Mkuu 1995, kwa hiyo alipojibiwa hivyo,
aliona hakuna njia nyingine zaidi ya
kutafuta haki yake akiwa nje ya chama.
Akahama, hivyo kutekeleza kauli ya
Mwalimu Nyerere: “Mama CCM si mama
yangu mzazi.”

KAMA CHAMA KIMESHINDWA KUTENDA HAKI MIONGONI MWA WANACHAMA WAKE KITAWEZAJE KUTENDA HAKI KWA WATANZANIA WASIOKUWA WANACHAMA WAKE?
 
Usitumie nguvu zako bure huyo kashakataliwa ndio maana nyumbani kwake wamechukuwa wapinzani. Eti raisi akienda nyumbani ofisi ya kijiji ni ukawa ataripotije. Alafu kingine huyo ni mchumia tumbo hafai ccm wakimtosa anaenda act-tz



Wakuu si vyema kuquote gazeti lote la mtia mada.
 
Wassira amekuwa mtetezi wa Wakulima, anaamini Uchumi unajengwa kwa kuimarisha Viwanda na anaamini Wakulima kama Tabaka kubwa wanatakiwa waunganishwe kwa Kilimo Cha Kisasa na soko la uhakika, Viwanda na kuboresha Viwanda vtasaidia sekta za Serikali na Binafsi kukuza Mitaji na kutoa Suluhu la Ajira kwa Vijana.

Rushwa lazima ipingwe kwa nguvu zote Ili kodi itumike kwa Malengo yaliyopangwa, Biashara lazima itengenezewe sera ili Wafanyabiashara wakubwa na Wadogo waendelee kufaidi soko la kibiashara la ndani na Nje ya Nchi.

kutumia Rasilimali zilizopo kama Madini,Gesi na mengineyo kuimarisha Uchumi wa Nchi na Mtu mmoja mmoja ili kufanya ndoto ya Tanzania kuwa Nchi ya Kipato na Uchumi wa kati.

Hii ni moja ya Nukuu zake kwenye Hotuba zake na semina mbalimbali.

Wassira yuko vizuri.
 
wapendwa msipoamini maneno yangu hata neno la mungu basi mtakuwa hamuamini kwa kifupi ni kwamba akili za kuambiwa changanya na zako.. mzee wasira ndiye anayeandaliwa kumrithi kiwete na ukijaribu kuchunguza kwa umakini utaona kuwa mh wasira amekuwa chachu kubwa kwa prof kikwete kiasi kwamba hata kwenye maadhimisho ya CCM mkoani ruvuma bado alisema kuwa chagueni kiongozi asiyetiliwa shaka nikiamini kuwa wasira hatiliwi shaka hata kidogo na kikubwa zaidi ni kidogo kwani amekuwa ni mmoja wa viongozi wenye mfano wa uadilufu... Wasira ndiye rais wengine mnajisumbua
 
for sure iwill fight till death for wssira kwakweli ukiacha hoja za kishabiki wasira ni kiongozi mzuri na muadilifu wewe unayezungumzia sura bado huna uchungu na taifa hili
 
Rockspider umetumwa wewe rudisha bahasha ya watu, haya mutex sasa umetoa wapi??? Unazusha uongo hadi unaonekana mwehu.
Na arudishe haraka kabla mwenyewe hajasoma andiko lake maana kuna mengine yatamkumbusha machungu, baada ya kushinda ubunge mwaka 1995 kwa ticket ya NCCR- Mageuzi alipingwa mahakamani akavuliwa ubunge na kupigwa marufuku asigombee ubunge kwa kipindi cha miaka mitano hivyo kipindi chote cha awamu ya tatu, 1995-2005 hakuwa mbunge wala hakuwa katika utumishi wa umma alikuwa mwambao wa ziwa victoria akivua sangara, hivyo mheshimiwa mpambe uwe mwangalifu na upambe wako kuna watu wanaoijua historia yake kuliko wewe; na awamu ya JK ndiyo iliyomrudisha serikalini mwaka 2006 alipoteuliwa kuwa waziri, usimpambe kihivyo mchango wake kwenye taifa ni wa kawaida kabisa hauna uzoefu mkubwa kuwazidi Sitta, Lowassa, Lukuvi na hata mama Nagu.
 

Ha ha ha,
Endelea kujiburudisha hivyo hivyo. Hata mateja wakibwia Unga hua wanaotaga wako Ulaya kumbe wako Maskani Lebanon, Ferry!!
 
for sure iwill fight till death for wssira kwakweli ukiacha hoja za kishabiki wasira ni kiongozi mzuri na muadilifu wewe unayezungumzia sura bado huna uchungu na taifa hili

Ameshaondoka kwenye ile nyumba anayoikomalia bila kulipa kodi?
 
Sifa unazo watu wanakusubiri tu utangaze nia wakuunge mkono maana wewe ndio tegemeo lao!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…