Wassira: Nitagombea urais 2015

Perry wanyama pori ikulu??? haitawezekana hata kidogo


Mkuu umenikumbusha wimbo mmoja wa chama cha ngangari enzi zile akigombea urais Bwakila toka south...walikua wanaimba....'....Mpaka mbona unatisha....kinyago cha mpapule'(kiitikio).
 
Rais wetu awe Sokwe? Haiwezekani. Kwanza anauelewa mdogo kuliko sisimizi, anasura mbaya, roho mbaya, kauli mbaya.hana elimu ...... yaani nashindwa kumuelezea ......!

Sijui hayo mengine,kwa upande wa elimu ana masters 3 tofauti za mambo ya uchumi......jama nchi hii tusiipeleke ki shabiki mponde mtu si kwakumwonea jamaa elimu ipo.
 
Mhe. WASSIRA amekuwa kielelezo cha utendaji uliotukuka hivyo kila wizara anayopelekwa anafanya vizuri na kumfanya rais awe anampa majukumu ya ambayo mawaziri wengine yamewashinda.Naomba uelewe Gwangambo sura na utendaji haviendani hii inanipelekea nikutilie shaka juu ya uwezo wako wa kufikiri na kupambanua mambo.WASSIRA ndiye kiongozi bora kati ya wote waliotangaza nia hivyo tumuunge mkono atuletee mabadiliko ya kweli nchini.
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru kumjua Rais wetu...hakuna haja ya kufanya tena uchaguzi tukae tujenge nchi yetu!
 
Hatuna haja ya mgombea urais anayechukua fomu ya urais (tena kwa mara ya kwanza) akiwa na miaka 70 au zaidi
 
kuna watu hata aibu hawana sasa huyu babu niwakumpigia promo?
 
Hapa kwenye jina la TYSON LILITOKANA NA KUMSHINDA UBUNGE WARIOBA NDANI YA CCM na NJE YA CCM.
Alipo hojiwa na waandishi wa habari ndio walimlinganisha na jina hilo kwa kumtoa Warioba kwa Knock Out.
Wasira anauwezo mkubwa kama utajadili hoja na si vihoja.
 
kuna watu hata aibu hawana sasa huyu babu niwakumpigia promo?

Alipaswa kujipambanua wakati wa BMK, uzalendo wake wa kutetea watanzania masikini angeuonyesha ndani ya BMK kwa kuikataa katiba inayopendekezwa. Tofauti na hapo ni porojo tu ambazo zimezoeleka. Halafu na nyie waandishi wa habari mlio pungukiwa uzalendo ipo siku tamaa zenu za visenti zitawatokea puani. Mmekosa kabisa journalistic ethics kisa tumbo.
 
Nakupongeza kwa kujitahidi kumuelezea wasira hakika umemtendea, Kwa sifa hizo anafaa kuwa raisi.achana na huo upuuzi mwingine.
 
Bwana mkubwa kila jina la NYERERE ina maanisha ni yule Baba yake Makongoro? Nyerere nyingine inamaanisha Vicent,,,,
Nini Hoja yangu?
HOJA YANGU HAPA WASIRA ALIYE TAJWA SI HUYU RAIS MTARAJIWA NI KAKA YAKE.......JARIBUNI KUPUNGUZA UVIVU WA KUJISOMEA KUMBUKUMBU ZA NCHI.
 
Nyerere aliwahi kumteua Wassira kuwa RC wa Mara... Kwa kutumia wadhifa wake alimwandikia barua GM wa Mutex kumtaka kiwanda kiwaajiri watu wa Mara pekee!!! GM alikasirika sana kiasi cha kupeleka ile barua kwa JKN! ... JKN alimwita wassira Butiama! Katika Mazungumzo Wassira alijikojolea baada ya kugundua kuwa Barua yake ilimfikia JKN aliekuwa anapinga Ukabila kwa nguvu zote... Baada ya hapo, wassira alipotezewa hadi Rostam alipompa fedha kwaajili ya Kampeni ya JK 2005 ... Huyu Mkabila, Mdini na Mkanda Gaidi mwenye kuabudu nguvu dhidi ya wapinzani Hastahili kamwe kuongoza hata Tarafa ndani ya nchi yetu ... Kama mnampenda sana Mpelekeni akawe msimamizi wa Mapori ya Gombe ...
 
Hapo Mkuu marekebisho...aliyekuwa miongoni mwa waasisi wa CHADEMA ni kaka yake George Wassira...wakati huyu ni Steven Massatu Wassira
Kwa sifa hizo,huyu ni mtu ndani ya chama anayestahili kuppeperusha bend era,hayo mengine ya maumbile nk si hoja,hakuna mwanadamu aliyejitengeneza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…