Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya

Yani viongozi wa kiafrika kwa kupenda kung'ang'ania madaraka mpka inatia aibu, kila anapokwenda jamaa wanamkataa ila bado anataka kulazimisha tu, halafu watu wanakuja wanakwambia vijana wakajiajiri wakati wao kazi hyo hawaiwezi
 
Saidi, unaweza kupata hukumu ya mahakama kuu.
Kuna kitu if you have information let me know. Mahakama katika kesi ya Lema ya ubunge huko nyuma, ilisema voters have no locus stand if their direct right are not affected. Sasa hawa watatu walitumia case law ipi kupinga ile ya kwanza.
Wanajua kila kitu wameamua kumchuna tu
 
" What you want, one more, now what you get one more" bob marley. Wapo watu ambao wanaamini wamezaliwa ili wawe viongozi na kwamba wao wanastahili yaliyo bora zaidi kuliko wengine. Wao wanadhani ni watu bora kuliko wengine. Bob marley daid "you can fool some people sometimes but you cant fool all the people all the time"
 
Huyu mzee nahisi kuna 'dunia' nyingine inamwita sasa anatafuta sababu ya kwenda huko. miaka 71 bado kila kukicha ni mahakamani eti uwe mbunge? ulisahau nini Dodoma? Dandia Bunda Exp. inaenda Dom chukua ulichosahau rudi kwenu ukacheze na wajukuu! Ebo!
 
wasira inatakiwa ajue kwamba hata mti huchipua , hukua, hutoa majani na mwishowe hunyauka na kukauka. mti ulio kauka hata ukimwagiliwa maji hauwezi kuchipua tena, ila bado utafaa kwa matumizi mengine ya binadamu kama vile kuni.
Khaaa.......mkuu maneno yako ya hekima yanaumiza moyo..... ila ukweli unauma.........
 
Huyu mzee kama vipi anyang'anywe bunduki haraka maana anasumbua sana.
 
Hii mbinu
Bulaya inabidi awe makini... Maana Wasira akishinda rufaa kwa msaada wa ccm... Yeye(Bulaya) rufaa yake itakuwa ngumu kusikilizwa...
 
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
ana lipi jipya au la ziada?tumechoka kusikia ndoto za alinacha juu ya Tz kuwa Poland in Agric sector
 
Kutaka madaraka kwa gharama yoyote ndo tabia za WAJITA.

Simshangai Wasira.
 
031e70ab9553a0f0f3a8751d271f0598.jpg
 
Huyu mzee wangu vipi tena! OK isiwe tabu, ngoja nimuombe mh.Rais amtafutie kijinafasi somewhere ili mzee atulie. Maana hizi ni dalili tosha za kutuma salamu ikulu imfikirie pia.
Rais wetu mtulize huyo mzee wetu, mteue awe makamo wa Agostine Mrema huko Parole maana ni kama wanafanana kitabia.
 
Back
Top Bottom