Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya

Nakumbuka niliwahi kuona clip ya makongoro nyerere akimzungumzia wassira kila utawala "yupoo". Kama kuna mwana jamvi anayo aiweke ili tumjadili huyu mroho wa madaraka
 
Umri wa miaka 71 bado unataka uende bungeni ukafanye maamuzi yatakayo athiri kundi kubwa la vijana ambalo ni 20s and 30s!! This is absolutely nonsense!! Matokeo yake hawa wazee wanaenda kututungia sheria mbovu coz wao huangalia sheria zitakazowa-favour katika kipindi chao cha madaraka kuliko kuangazia zaidi vizazi vijavyo, baada ya hapo mbeleni tunakuja kupata shida na kuingia gharama kuzirekebisha ama kuzibadili.

Jamani vijana tuamke! Wazee tunawapenda sana lakini kwa maoni yangu naomba wakae pembeni wawe washauri wetu na si kutufanyia maamuzi.
 
Nakumbuka niliwahi kuona clip ya makongoro nyerere akimzungumzia wassira kila utawala "yupoo". Kama kuna mwana jamvi anayo aiweke ili tumjadili huyu mroho wa madaraka
Hapana jamanii. Ni haki yake ya kikatiba! Ndio namna demokrasia inavyokua! Mnadhani majaji wasipopata kesi kama hizi watafanya kazi gani ?

Hata hivyo wanasema ni wafuasi au washabiki waliopeleka kesi mahakamani. Wasira mwenyewe alishajichokea anaendesha chama tu kule.mbona upinzani ukiwa unakata kata rufaa kama hizi huwa hamzungumzi mnakaa kimyaa. Its ridiculous.

Mimi nimeamua kuwa mzalendo kwa manufaa ya nchi. Lakini kisiasa tumeshapigizwa sana mara michango mara sijui nini. Utadhani kuna malaika angeshuka kutawala nchi. Kumbe ni uhuni wa baadhi yetu kupiga dili kama lile la kupokea watuhumiwa wa ufisadi na kuwasafisha. Baada ya hapo eti waende sasa ikulu. Khaaaaaaaaaa.
 
Nakumbuka niliwahi kuona clip ya makongoro nyerere akimzungumzia wassira kila utawala "yupoo". Kama kuna mwana jamvi anayo aiweke ili tumjadili huyu mroho wa madaraka
Mbona kuna wanasiasa walihamia upinzani, wakataka kwenda ikulu kwa kugombea urais. Wamekuwepo tangu awamu ile ya kwanza ya Nyerere wapoo. Kwa Mwinyi walikuwepo, kwa Mkapa walikuwepo. Kwa Kikwete walikuwepo. Baada ya kukatwa majina? Hao wakakimbilia upinzani kutafuta madaraka kwa nguvu. Wapoo tuu. Mpaka leo bado wapooo, wanataka kwenda ikulu.

Tena huko nyuma wamekuwa wakipitia maskendo mbalimbali ambayo yalikuwa labda hayafunuliwi. Unasema nini kamanda ?. Hahahaha hizo ndio siasa.

Mifano mnaijua wenyewe. Nyani mnajua haoni kundule. Ni bora tujadili hili la msingi kuliko kujadili yule mzee ambaye kwanza ni issue ta ubunge tuu. Hauna mashiko.
 
Umri wa miaka 71 bado unataka uende bungeni ukafanye maamuzi yatakayo athiri kundi kubwa la vijana ambalo ni 20s and 30s!! This is absolutely nonsense!! Matokeo yake hawa wazee wanaenda kututungia sheria mbovu coz wao huangalia sheria zitakazowafavour katika kipindi chao cha madaraka kuliko kuangazia zaidi vizazi vijavyo, baada ya hapo mbeleni tunakuja kupata shida na kuingia gharama kuzirekebisha ama kuzibadili.
Jamani vijana tuamke! Wazee tunawapenda sana lakini kwa maoni yangu naomba wakae pembeni wawe washauri wetu na si kutufanyia maamuzi.
What about umri wa kama Kingunge ,Sumaye Lowasa na wengineo ambao wanataka kwenda ikulu kwa sasa. wana tofauti gani nao. Kama ni sheria iwe kama msumeno. Ikate pande zote. Mnadhani upinzani hatuna wazee. Mnajidanganya. Kwa hiyo tuseme kama hawafai iwe kwa wote. Acheni ujinga
 
angepewa uraisi angeondoka madarakani kweli huyu baada ya muda wake kuisha
 
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
Duh! Babu sugu !
 
..Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa.

Ni aibu na fedheha kwa huyu babu kuendelea kukimbizana na hii kesi. Tena kwa mila na desturi za kwao, ni fedheha zaidi kwa lizee janamume kulambishwa mchanga na mtoto mdogo tena wa jinsia ya kike. Kama anadhani ule mhimili uliochimbiwa chini kabisa utaingilia kati, atakua anajidanganya.
 
Mimi ni mwanachama wa CCM , lakini hili la huyu Mzee limenichosha.
Umeshindwa na umri umekuzidi si apumzike.

Kama pesa anazo basi si angeamua kufanya mema na kuwapa yatima au masikini wa Bunda badala ya kushindana nawe umeshindwa.
 
Nahisi mzee Wasira hana nia ya kuchukuwa ushindi ila ni kumfanya mbuge huyo kuwa busy na kesi kuliko kushughulikia mahitaji ya wananchi ili uchaguzi ujao asiwe na kitu cha kuonyesha kuwa kafanya nini...
 
Tushukuru mungu wassira alikuwa mbunge na kama angekuwa rais wa Nchi kwa mtindo huu asingetoka madarakani
 
Huyu Mzee apumzike tu Mbona anatuaibisha CCM. kwanza ingawa mimi ni CCM sijampenda hata kidogo anataka afie madarakani! Kwanza nawalaumu sana CCM wenzangu kule Bunda, kwa nini walimpitisha huyo mzee kugombea tena Si wangemkata tu. Nafikikiri lile Jimbo leo lingekuwa mikononi mwetu CCM. Lakini wakampa huyu mzee ndio maana watu walipiga kura za Hasira.
Aache bhna, kwanza 2020 huyo mzee asahau kupitishwa na CCM tena.
 
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
Anaanza fanans na kufata sipa za Mugabe
 
Back
Top Bottom