Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya

Breaking News.....Esther Bulaya kwa kutunza heshima yake na wazazi wake ameamua ku achia ngazi baada ya kushauriana na uongozi wa CHADEMA na anateuliwa kuwa Mbunge viti maalimu.....mmoja naye anampisha Bulaya.
Chanzo.......Uwongo vijiwe vya kahawa.
 
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
Hahahaaa hapa ananikumbuusha mbaali Rais wa miaka hiyo Reigan R alikuwa anaaamini bado ni rais wa marekani hadi alipoaga dunia duu mwanangu kuwa uyaone ya walimwengu.
 
Ni haki yake kukata rufaa. Wacha aendelee mpaka kieleweke kwani haki haina umri.
Hii ndio tunu iliyopo ndani ya chama kwa sasa ndio maana Mzee kawashtukia mipiga dili na sifa za kinafki kapita mbaali kabisa na nyie .
 
Kwanini wenzie wasimshauri?? Mzee anadharirika sasa,umri wakulea vitukuu yeye anataka ubunge for what?
 
Daaa!!huyu mzee ni shidaaa,kaona teuzi serikalini zimeisha,juzi kichama nako hola japo alisikia sikia tetesi kupewa cheo cha pole pole kikayeyuka kakumbuka mahakamani kuna pointi alizisahau mzee wasira utafilisika kulipa gharama za kesi .wakili unayepambana nae Lissu mmm!!
 
Nia ya Wasira ni kuweka rekodi ya sheria vizuri kwa faida ya wajao. Hongera Wasira na endelea.
 
Mwenye ile video ya Makongoro JK Nyerere yenye kibwagizo cha, ".....Wasira yupo" aiweke humu tafadhari, naomba tu cause nina hamu ya kuisikiliza.
 
Kwanini Wassira asiachie vijana kuongoza maana mda wake umeisha, abaki kuwa mshauri tu.
 
WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.Nashauri mzee huyu afutiwe haraka leseni ya kumilki bunduki (before hand)

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
 
Wakati mwingine busara ni muhimu sana, huyu Mzee anashauriwa na wakina nani? Watoto wake wanajisikiaje sijui..njaa hii ya madaraka ni aibu kuu.. Shame shame
 
Hii ndio tunu iliyopo ndani ya chama kwa sasa ndio maana Mzee kawashtukia mipiga dili na sifa za kinafki kapita mbaali kabisa na nyie .
Hujaeleweka ndugu. Hapa tunaongelea Mzee Wassira na haki yake ya kukata rufaa sioni ni jinsi gani suala la mipiga dili ya kwenye chama linaingia hapa!
 
Back
Top Bottom