Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya

WAZIRI mwandamizi wa serikali ya Tanzania kwa awamu nne za uongozi, Stephen Masato Wassira, kupitia kwa wafuasi wake watatu, amekata rufaa Mahakama ya Rufaa, akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu kwa kuhalalisha ushindi wa Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema).

Wassira (71 ) alikuwa waziri kwa mara ya kwanza tangu Desemba 07, 1973 akiwa naibu waziri wa Kilimo na ameendelea kuwa kiongozi mwandamizi wakati wa serikali ya Mwalimu Julius Nyerere, akarithiwa wakati wa Rais Ali Hassan Mwinyi, baadaye Rais Benjamin Mkapa na hatimaye uongozi wa awamu ya nne wa Rais Jakaya Kikwete.

Tayari wafuasi hao wa Wassira; Magambo Masato, Matwiga Matwiga na Ascetic Malagaila, wamefungua kesi hiyo na imesajiliwa katika ofisi za mahakama ya rufaa jijini Mwanza tarehe 16 Desemba, 2016 na itakuwa ni kesi ya rufaa namba 199 ya mwaka 2016.

Katika rufaa hiyo iliyoandikwa na wakili wao, Constatine Mutalemwa, wametoa sababu kadhaa kama hoja zao za kukata rufaa.

Kwanza, wanadai kwamba jaji hakuzingatia makosa yaliyofanyika baada ya zoezi la kupiga kura.

Pili, Wassira au wakala wake wanadai hakuitwa kwenye majumuisho kujulishwa siku, mahali wanafanyia majumuisho.

Tatu, wanadai kuwa jaji hakutilia maanani kesi zinazofanana na hii zilizotolewa kama mfano mahakamani.

Nne, Jaji alikosea kutoa uamuzi kwa misingi ya maoni binafsi badala ya kuzingatia mambo ya maana.

Wanadai kuwa jaji alisema wananchi wa Bunda ni maskini waachwe wafanye shughuli za maendeleo kwa sasa.

Tano, wanadai jaji alikosea kuamua kuhusu sheria ya viapo na matamko iliyotajwa katika kanuni za kuendesha kesi za uchaguzi.

Novemba 18, mwaka huu, katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza ilitoa uamuzi wa kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge uliompa ushindi Mbunge wa Bunda Mjini, Esther Bulaya (Chadema) dhidi ya Stephen Wassira (CCM).

Kesi hiyo ya kupinga matokeo ya uchaguzi ilifunguliwa katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, lakini ilikuwa inasikilizwa mjini Musoma, mkoani Mara.

Mahakama hiyo ilieleza kutoridhishwa na ushahidi wa kupinga matokeo hayo uliowasilishwa na upande wa walalamikaji, hivyo ikamthibitisha Bulaya kuwa mbunge halali wa jimbo hilo.

Kesi ya kupinga matokeo hayo ilifunguliwa na wafuasi wa Wassira ambaye alikuwa mbunge wa jimbo hilo kabla ya kuondolewa kupitia uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Katika kesi ya msingi, walalamikaji ambao ni wakazi wa Bunda walidai kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki kwakuwa uligubikwa na vitendo vya rushwa, mgombea wanaemuunga mkono kunyimwa fursa ya kuhakiki matokeo pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kupigia kura visivyo halali.

Katika kesi hiyo, Bulaya alitetewa na mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu.

CHANZO: Wassira akimbilia Mahakama ya Rufaa kumpinga Bulaya | FikraPevu
Saidi, unaweza kupata hukumu ya mahakama kuu.
Kuna kitu if you have information let me know. Mahakama katika kesi ya Lema ya ubunge huko nyuma, ilisema voters have no locus stand if their direct right are not affected. Sasa hawa watatu walitumia case law ipi kupinga ile ya kwanza.
 
Nakumbuka Hotuba Maarufu ya Makongoro Nyerere na Historia ya Wassira kwamba YUPO TU.Enzi za baba wa Taifa Wassira alikuwa YUPO,Akaja Mwinyi Jamaa YUPO,Akaja Mkapa YUPO,Kaja Kikwete YUPO,Sasa Magufuli anataka tena AWEPO.
Kweli Jamaa Kiboko.
 
Nikiona sura yake huwa napata majonzi kwasababu huwa nakumbuka kusanyiko la watu wengi wenye huzuni na wengine wanalia mpaka kuzimia hasa pale tunaposogelea kile kitanda cha kubebea mtu aliyeshindwa kupumua
 
Hivi umri wa kustaafu kwa lazima ni miaka
mingapi vile? sijuhi kama nakumbuka vizuri
ni miaka 60,sasa baba yangu huyu naona Mungu
kaishamuongezea 11 ya ziada kati awamu zilizopita.
Nashauri hao wanaokata rufaa,mahakama iamuru
wapimwe kwanza akili.

Nashauri hivyo kwa sababu ukiishazeeka
hata kama ulikuwa unafanya vizuri enzi za ujana wako
umri ukiishaenda unaanza kuvuruga,kwani kumbukumbu hupotea,
Namkumbuka babu yangu alikuwa akikuambia 100,ujue anazungumzia 1000.
Pamoja na kwamba miaka ya nyuma kabla ya uzee alikuwa vizuri.

Sasa maadamu Mh.mwenyewe kama amekubali yaishe
hao wanaoshinikiza ndo watashika nafasi hiyo ya ubunge?
 
Wassira ana hangaika bure,waliotoa hukumu ya kumukataa ni wananchi wa Bunda wenye jimbo,kama haamini kuwa kakataliwa asubiri mpaka 2020 akate rufaa kwa wananchi wa Bunda wenye jimbo,kama walifanya kosa kumpiga chini,watasahihisha makosa yao kwa kumuchagua Wassira kuwa mbunge wao kwa mara nyingine.
 
Mambo mengine ni aibu tu, inabidi JPM amtafutie kaulaji ka kishikaji ili apunguze kihoro
 
Huyu mzee nafuu CCM walimuona mapema,wakamwenguamapema kwenye kinyang'anyiro cha urais mapema,angepitishwa na CCM akashinda urais,angegeuka kuwa Mugabe wa Tanzania.
 
Mzee kinachomtisha ni ule mradi wa Maji Bunda,ambao tender yake alimpigania mwanae Kambarage akapewa.Mradi ulitakiwa kukamilika mwaka jana kabla ya uchaguzi mkuu.Na ili kutengeneza mazingira mazuri ya Chama chetu kushinda,Waziri Mkuu wa wakati huo Pinda pamoja na Prof Maghembe walienda kuuzindua na kuahidi maji ndani ya week mbili.

Baada ya muda huo,hakukuwa si tu na maji,bali hata matone ya maji ktk mabomba "hewa" yaliyotandazwa.Pesa zote za mradi zilishatolewa,tatizo Mzabuni ambaye ni "Kampuni ya mfukoni" ya mwanae ikashindwa kuendelea.

Sasa hapa Mutalemwa anakula hela tu za Mzee,Mzee lengo lake arudi ili akae na uongozi wa Halmashauri waone wanafichaje "jibu" hili...But,It is too late to catch the Train.From 1970's to 2015 inatosha!!!
Aliwahi ulizwa na wapiga kura kuhusu swala la maji, akawajibu " mnasema maji hamna, kwani dawa mnamezea nini??
Huyu mzee ana majibu ya shombo kwelikweli, hapo akishindwa najua ataenda hadi kwenye ile mahakama ya chadema kule uholanzi,akishindwa na hapo basi atamuomba Trump aje ampindue Esther kwa special force.
 
Huyu babu akalee wajukuu,amezeeka sana.Akiba alizojiwekea ni muda muafaka azitumie.
 
Dah,aibu sana mizee kama hiyo ikiwa serikalin hupenda sana kuhubiri vijana mjiajiri ardhi ipo ya kutosha.Sasa tunaomba na yeye achangamkie hizo fursa alizokuwa anahubiri
 
Back
Top Bottom