Wassira abwagwa: Mahakama ya Rufaa Dar yatupilia mbali Rufani ya Jimbo la Bunda Mjini

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Mahakama ya Rufani Dar imeanza kusoma hukumu ya rufaa ya ubunge wa Bunda mjini, inayomhusu mbunge wa jimbo hilo Esther Bulaya asubuhi hii.

=====

UPDATES

=> Habari tumezipata muda huu tukiwa njiani kuelekea Mahakamani kuna baadhi ya waandishi wa habari wamezuia na Jeshi la Polisi kuingia ndani kusikiliza hukumu hiyo...

=> Mahakama ya Rufani imetupia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura 4 wa Jimbo la Bunda Mjini kupinga ushindi wa Mbunge, Esther Bulaya.
Bulaya.png

Esther Bulaya​

=>Baada ya ushindi huo Mbunge wa Jimbo la Bunda Mjini Esther Bulaya ameandika ujumbe huu: Wana Bunda wameshinda tena na tena,asante Mungu

Shauri hilo lilifunguliwa na Magambo Masato na wenzake wanne, wakiiomba mahakama kutengua matokeo yaliyompa ushindi mbunge Ester Bulaya9CHADEMA), aliyekuwa kada wa CCM kabla ya kuhamia Chadema.

Miongoni mwa madai ya msingi ya walalamikaji yaliyowasilishwa mahakamni wakiwakilishwa na mawakili wawili, Constatine Mutalemwa na Denis Kahangwa, walidai aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM, Stephen Wasira alikataliwa ombi la kuhesabu wala kuhakiki kura baadhi ya vituo, kuwapo mianya ya rushwa na kunyimwa haki yao ya kuchagua.
 
Nawashangaa sana kanda ya Ziwa na maziwa makuu ambao bado wako chadema. maana mlishaonyeshwa pa kwenda na Lisu.
 
Back
Top Bottom