Wasomi wetu ni shida!

Wasomi wetu ni shida!

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,289
Reaction score
2,472
Nipo katika mazingira ambayo huwa naona kazi za hawa vijana wa chuo kikuu cha DSM mara kwa mara. Kiukweli misingi yao ya kielimu ni mibovu. Assinment wanazopewa huwa wanapata shida sana kuzijibu kiufasaha, hasa kiingereza kinapohusika. Kiingereza chao ni kibovu mno. Aghalabu sisi wabongo huwa tunajua zaidi kingereza cha kuandika kuiko cha kuongea, lakini kwa hawa vijana wetu ni tabu tupu. Huwa najiuliza hao walimu wao wanaposoma kazi zao huwa wanakuwa katika hali gani.

NB: Nami pia ni alumni wa UDSM
 
kuna asilimia kubwa haujasoma UDSM, ulitamani kusoma udsm ukanyimwa nafasi na una bifu na udsm. kwa taarifa yako, ile cream ya juu kwenye matokeo ya form six tz ndio huwa inaenda udsm, huko kwingine utawakuta division kuanzia three na kuendelea. jiulize why ninyi mnaojifanya kujua kiingereza hamkupata division one form six? acha kuchukia chuo bora tz bwana.
 
Thread ya kitoto kwa mwezi May 2015.
Hivi uelewa au umahiri wa msomi unapimwa kwa kujua kingereza? Kuna walevi kibayo wanamwaga kimombo you can't believe ila kwenye familia zao hata mboga hawanunui, kuna wengine makahaba wako bongo movie wanapiga ung'eng'e ila kazi yao kujiuza.
 
usijejikuta wewe ndiyo problem uelewa wako mdogo ..... au kweli wanafunzi tatizo ...

kwa sababu unawapima kupitia uelewa wako wewe na unachojua wewe..
nakubaliana na wewe. unajua mtu ambaye haelewi huwa hajijui kuwa haelewi yeye huwa anaamini kuwa anaelewa kuliko wengine wote. ila wale walio karibu naye ndio wanaweza kumtathimini. hivyo, yeye pia anatakiwa apate third party opinion juu ya uelewa wake kama kweli kutakuwa na mtu honest anayeweza kuwa na ujasiri wa kumwambia ukweli hata kama mchungu. ila kuna dalili za chuki dhidi ya udsm kasababu hakupata bahati ya nafasi kusoma udsm. iyo ameionyesha wazi.
 
Majuzi niliona mahali huko UK nao wanalalamika vijana wao kufanya vibaya ktk masomo ya English na Maths! Sasa sisemi tujiweke nyuma, kwa sababu hata mataifa ya dunia ya kwanza yana changamoto ktk sekta ya elimu, la! Bali tuone mbinu na mikakati sahihi kulingana na mazingira yetu na kutatua mizizi ya tatizo.
 
nakubaliana na wewe. unajua mtu ambaye haelewi huwa hajijui kuwa haelewi yeye huwa anaamini kuwa anaelewa kuliko wengine wote. ila wale walio karibu naye ndio wanaweza kumtathimini. hivyo, yeye pia anatakiwa apate third party opinion juu ya uelewa wake kama kweli kutakuwa na mtu honest anayeweza kuwa na ujasiri wa kumwambia ukweli hata kama mchungu. ila kuna dalili za chuki dhidi ya udsm kasababu hakupata bahati ya nafasi kusoma udsm. iyo ameionyesha wazi.
kila jambo linaweza ongozwa kihisia au kiakili.. ukitumia hisia lazama uongee bila data .. mimi sikubaliani nae wala simpingi ila nataka tu asiwe bias asije jikuta yeye uelewa wake mdogo .....
 
Mkuu kuto kujitambua na kutambua Hali ya Dunia kwa sasa inakwendaje, kuendeza starehe wanapokuwa vyuoni.

Luck of attitude to success also is the reason.

Luck or Lack??? Sikubahatika kufika chuo kikuu lakini nafahamu kuna vigezo vingi mbali na lugha vinatumika kupima umahiri wa mwanafunzi. Kuna wale wa fani za uhandisi huko tokea o'level kiingereza chao ni CONSIDER, TAKE a EQUALS TO b,GIVEN x IS CONSTANT n.k leo hii unampatia aandike essay ya somo wanaita DS kama sikosei halafu eti utumie ufanisi katika kiingereza kama kipimo,shame on you!!!
 
Nipo katika mazingira ambayo huwa naona kazi za hawa vijana wa chuo kikuu cha DSM mara kwa mara. Kiukweli misingi yao ya kielimu ni mibovu. Assinment wanazopewa huwa wanapata shida sana kuzijibu kiufasaha, hasa kiingereza kinapohusika. Kiingereza chao ni kibovu mno. Aghalabu sisi wabongo huwa tunajua zaidi kingereza cha kuandika kuiko cha kuongea, lakini kwa hawa vijana wetu ni tabu tupu. Huwa najiuliza hao walimu wao wanaposoma kazi zao huwa wanakuwa katika hali gani.

NB: Nami pia ni alumni wa UDSM
Sahihisha kwanza hizo halafu utuelezee uzima wako wa kiingereza uko wapi??
 
kuna asilimia kubwa haujasoma UDSM, ulitamani kusoma udsm ukanyimwa nafasi na una bifu na udsm. kwa taarifa yako, ile cream ya juu kwenye matokeo ya form six tz ndio huwa inaenda udsm, huko kwingine utawakuta division kuanzia three na kuendelea. jiulize why ninyi mnaojifanya kujua kiingereza hamkupata division one form six? acha kuchukia chuo bora tz bwana.

we ni zaid ya mchawi. et cream zote zinaenda UDSM . ila utakua ni mtoto wa first yeah bado una ujinga wa kichuo.

apo UDSM kuna koz zote za afya? engineering na zinginezo?

udaktar wa muhimbili na KCMC UDSM hamuingii.
computer science na education UDOM wanawakimbiza sana.
tourism, agricultural, and enviromental courses SUA wako juu.
maswala ya economic,accounts Mzumbe wako poa sana.
UDSM Mpo vizur sana kwenye law
 
Dah! nashukuru kwa majibu mazuri
 
Luck or Lack??? Sikubahatika kufika chuo kikuu lakini nafahamu kuna vigezo vingi mbali na lugha vinatumika kupima umahiri wa mwanafunzi. Kuna wale wa fani za uhandisi huko tokea o'level kiingereza chao ni CONSIDER, TAKE a EQUALS TO b,GIVEN x IS CONSTANT n.k leo hii unampatia aandike essay ya somo wanaita DS kama sikosei halafu eti utumie ufanisi katika kiingereza kama kipimo,shame on you!!!

Mbona mapovu sana? Hao wahandisi hutumia kichina au kiingereza? Kiingereza cha DS na cha Civil vinatofautiana katika nini? Wacha kukimbia kivuli chako
 
Hahahaa hata mi nimekuja mbio, kuangalia picha hola!!
Kuwa na uwelewa ni pamoja kujua jambo gani linatakiwa liwe eneo gani.
Kama mtoa mada hajui mambo ya elimu yanawekwa jukwaa la elimu na sio PHOTOS, hapo ipo mushkeli!!
 
Back
Top Bottom