Wasomi wazidi kuikosoa Serikali

Huyo msomi ni mnafiki kaongea mambo yaleyale bila kuleta solution!!

Solution ni kila mtu afuate sheria.Hakuna aliyejuu ya SHERIA.Na rais ameapa kuilinda SHERIA NA KATIBA ya NCHI basi avilinde na kuvitetea pia
 

I believe we are on the same page but deferent approaches. Malipo yasiyostahili kwa wanataaluma / wasomi ni chanzo kikubwa cha wengi kukimbilia siasa inayotoa malipo mapana ambayo wakati mwingine hayana mashiko katika ustawi wa jamii inayokusudiwa kujengwa.
 
Hapo sawa!!!
 
Naomba uelewe bosi Rais haitumii katiba kuwa dicteta ila imempa madaraka makubwa kiasi ambacho maamuzi anayoyafanya unaweza kusema ni dicteta.Wewe unatakiwa ulie na kupigania mabadiliko ya katiba na si kusema Rais dicteta haitasaidia kitu
 
Huwezi kusema kuna wasomi wakati utafiti unasema 61%ya waitimu wa elimu ya juu wana uwezo mdogo wa maarifa na ufahamu
 
Unaposoma hiyo ibara ya 36 pia soma ibara ya 46A ibara ndogo ya 1na 2 na ya3.
Utaona kuwa rais hayuko juu ya sheria, na kuna hatua ambazo bunge linaweza kumchukulia kama atavunja katiba ya nchi au kwenda kinyume na maadili. Ni kweli ibara ya36 inampa madaraka makubwa lakini sio ya kuvunja katiba.

Sijaona mahali katiba pamoja na kasoro zake inaweza kumpa raisi uwezo wa kuwa dikteta. Labda tunatumia hili neno dikteta vibaya ndio maana Lisu hataki kusema dikteta akaishia hapo, anasema 'dikteta uchwara'.
 
Kuna watu wanataka unapoandika maelezo lazma uandike neno solution wapate kuona kuna suluhisho la mada husika limetolewa.Solution- read between the lines.
 
Nimekupata DANNY JULLY lakini hoja zangu hazijasema kuwa rais yupo juu ya sheria ila amepewa madaraka makubwa kiasi ambacho anauwezo wa kufanya maamuzi yoyote kwa mwamvuli wa katiba kuhusu jambo lolote na mtu wa kawaida(ordinary person)anaweza kusema kuwa anafanya maamuzi ya kidikteta.

Pili,ibara ulioitaja inahusu kumtoa madarakani Rais(impeachment of president) kabla ya kumshtaki.Hivyo hoja yako hiyo haiendani na kiin cha hoja yangu ya madaraka makubwa ya Rais,pia kumbuka hiyo ibara ya 46A inatumika pale tu ambapo unatak kumshtaki Rais kwa kosa la jinai au la kiraia,hivyo mimi kusema Rais anamadaraka makubwa kupitia ibara ya 36 sijamaanisha kuwa huwezi kumshtaki Rais kupitia ibara ya 46A.
 
Una interests fulani chama tawala hongera kwa kuwa mtumwa wa fikra za chama.Changamoto za nchi hii ni zilezile sababu ya watu kama wewe wasioweza kutoka kwenye comfort zone zao kwa kuogopa kukinzana na watawala wasijepoteza walicho nacho ingawa ukweli halisi wanaujua.
 

Dikteta wa ukweli ni Umma-" Dictatorship of the mass" ukiteta wa mtu mmoja mmoja ni uchwara tu
 
Sawa nimekuelewa mkuu.
 
Ndugu zangu mnaosema Rais ni dikteta na ambao mnasema Rais siyo dikteta je mnajua sifa na tabia ya mtu ambaye ni dikteta? Na je sifa na tabia hizo rais anayo? Majibu ya maswali haya yatahalalisha au kubatilisha udikteta wa rais kazi kwenu wasomi wa nchi hii
 
Unaweza kukuta hao polisi wanajishauri wenyewe na wala hawatumwi na mtu kwenda kumkamata TL: najiongeza tu kuw hao RPC na Mkuu wao wanajipa kazi ya kushinda mitandao kusikiliza JPM amesemwaje leo na wana act ingali yeye hana wazo wala hajawatuma! Polisi waache kujipendekeza! Wafanye kazi yao!! Kulind amani sio kulinda ukawa wasifanye maandamano!! Waache kujikomba!!!
 
haa haa hapo kwenye wasomi nimemkumbuka Dr RYOBA wa TBC....
 
Kesi za Mtikila mpaka leo hazijatekelezwa na zingine serikali ilizikatia rufaa licha ya marehemu kuwabwaga mara kadha. Ukweli ni kuwa watawala wa ki Africa walikubali mfumo wa vyama vingi shingo upande. Wewe Tz tangu tuingiie mfumo wa vyama vingi lakini tumeshindwa kutunga sheria zinazoendana na vyama vingi vya siasa. Badala yake zinatumika sheria za mfumo wa chama kimoja tena chama dola.

Maghufuli ni Rais mzuri ila anaonekana mwenye hasira na kutokupenda kukosolewa, nchi haiendeshwi hivyo.

Nashauri ategemee sana upendo wa wananchi wake asitegemee sana vyombo vya dola vitamharibia zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…