Wasomi wamfagilia Sumaye uongozi Pwani

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Dar es Salaam. Wasomi nchini wamesema iwapo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye atakuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, atasaidia kukijenga chama hicho cha upinzani nchini, kuanzia ngazi ya chini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema jana kuwa Sumaye ambaye juzi alirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo, katika ofisi za kanda hiyo Dar es Salaam, akitumia uzoefu alionao kiuongozi, atakuwa msaada kwa chama hicho.

Walisema uamuzi huo umeonyesha kuwa hakuhamia CHADEMA kwa masilahi binafsi.

Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema: “Inaonekana (Sumaye) ana lengo la kusaidia upinzani ukue. Kwa mchango na uzoefu wake serikalini ataisaidia sana CHADEMA maana chama lazima kiwe na nguvu kuanzia ngazi ya chini.”

Sumaye ndiye Waziri Mkuu pekee katika historia ya Tanzania kushika wadhifa huo kwa miaka 10 baada ya kuwa msaidizi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kati ya mwaka 1995 hadi 2005.

Agosti mwaka jana, Sumaye aliyekuwa kete muhimu katika kampeni za aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa kutokana kuikosoa Serikali na kuwataka Watanzania kutoichagua CCM, alitangaza kuachana na chama hicho tawala na kujiunga na upinzani.

Shumbusho alisema ameonyesha kuwa yeye siyo aina ya wastaafu wanaopenda sifa na hakwenda kusaka ulaji CHADEMA huku akibainisha nchi ikiwa na upinzani imara, chama kilichopo madarakani hugangamala.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Gaudence Mpangala alisema: “Alijiunga (Sumaye) na upinzani unaohitaji viongozi kila siku. Yeye kuwa kiongozi ni jambo sahihi zaidi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim alisema uamuzi aliochukua Sumaye ni haki yake ya kikatiba, licha ya kuwa watu watamkosoa kutokana na nafasi aliyokuwa nayo awali.

“Wapo wanasiasa wanaohama kwa masilahi binafsi, pili chama tawala huwa na mtindo wa kuwatumia makada wake waliohamia upinzani na mtu anaweza kuhama chama kwa ajili ya kwenda kukijenga chama kingine.

Kama Sumaye lengo lake ni kuijenga CHADEMA hatua aliyochukua ni sahihi,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema: “Anaonekana siyo mtu wa kutaka masilahi. Wakati wa kampeni alisema anataka kujenga upinzani, alichokiamua sasa ni wazi anataka kuwaonyesha Watanzania kuwa anaishi katika maneno yake.”
 
Wasomi kadhaa nchini wamemwagia sifa mjumbe wa Kamati Kuu Chadema Fredrick Sumaye kwa uamuzi wake wa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani.

Wakizungumza na gazeti la mwananchi Profesa George Shumbusho wa Mzumbe na Gaudence Mpangala wa Ruaha wamesema ni kitendo cha kishujaa kwa mtu mwenye historia ya kuwa waziri mkuu miaka kumi kuamua kujishusha na kugombea nafasi ndogo kabisa katika chama cha upinzani kwa lengo la kukiimarisha.

Wamesema inavyoonekana Sumaye hakuwa na agenda yoyote binafsi wala maslahi binafsi kwa kuhamia upinzani.

Wamesema akipata nafasi hiyo atakiimarisha sana Chadema kuanzia ngazi ya chini kabisa kutokana na heshima na ushawishi wake alio nao kwenye jamii.

Fredrick Sumaye aliombwa na wanachama kadhaa katika kanda ya pwani akubali kugombea uenyekiti wa Kanda ili atumie nafasi hiyo kukiimarisha chama na akakubaliana na wito huo.
 
Dar es Salaam. Wasomi nchini wamesema iwapo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye atakuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, atasaidia kukijenga chama hicho cha upinzani nchini, kuanzia ngazi ya chini.

Nchi hii tuna wasomi koko wa kutisha.Msomi huenda na ushahidi wa takwimu kabla ya kuongea.Msomi haongei kama mlevi tu wa kiroba bila takwimu.

Sumaye mkoa wa Pwani hajaingiza hata mwanachama mmoja mpya wa CHADEMA !!!! wanaoitwa wasomi tayari wameshaibuka eti ooooh atasaidia kujenga chama kuanzia chini!!! Kazi ipo kuwa na wasomi wa aina hii ni aibu.Ningekuwa nasoma kozi wanayofundishha nigehama na kubadilisha kozi.
 
...nina shaka kwanza kama ni kweli...huyu sumayi ni mtu ambae ktk siasa za alikotoka, ukiacha zali la "kufanyishwa"(na sio kuwa) waziri mkuu, hana chochote alichofanikiwa kisiasa.....kimbunga cha Mary Nagu, kilishampeperusha...ah! Chambilecho Peter Tosh..."just brand new, second hand!"
 
Dar es Salaam. Wasomi nchini wamesema iwapo Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye atakuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, atasaidia kukijenga chama hicho cha upinzani nchini, kuanzia ngazi ya chini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema jana kuwa Sumaye ambaye juzi alirejesha fomu ya kuwania nafasi hiyo, katika ofisi za kanda hiyo Dar es Salaam, akitumia uzoefu alionao kiuongozi, atakuwa msaada kwa chama hicho.

Walisema uamuzi huo umeonyesha kuwa hakuhamia CHADEMA kwa masilahi binafsi.

Profesa George Shumbusho wa Chuo Kikuu cha Mzumbe alisema: “Inaonekana (Sumaye) ana lengo la kusaidia upinzani ukue. Kwa mchango na uzoefu wake serikalini ataisaidia sana CHADEMA maana chama lazima kiwe na nguvu kuanzia ngazi ya chini.”

Sumaye ndiye Waziri Mkuu pekee katika historia ya Tanzania kushika wadhifa huo kwa miaka 10 baada ya kuwa msaidizi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa kati ya mwaka 1995 hadi 2005.

Agosti mwaka jana, Sumaye aliyekuwa kete muhimu katika kampeni za aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa kutokana kuikosoa Serikali na kuwataka Watanzania kutoichagua CCM, alitangaza kuachana na chama hicho tawala na kujiunga na upinzani.

Shumbusho alisema ameonyesha kuwa yeye siyo aina ya wastaafu wanaopenda sifa na hakwenda kusaka ulaji CHADEMA huku akibainisha nchi ikiwa na upinzani imara, chama kilichopo madarakani hugangamala.

Profesa wa Chuo Kikuu cha Ruaha, Gaudence Mpangala alisema: “Alijiunga (Sumaye) na upinzani unaohitaji viongozi kila siku. Yeye kuwa kiongozi ni jambo sahihi zaidi.”

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria (OUT), Hamad Salim alisema uamuzi aliochukua Sumaye ni haki yake ya kikatiba, licha ya kuwa watu watamkosoa kutokana na nafasi aliyokuwa nayo awali.

“Wapo wanasiasa wanaohama kwa masilahi binafsi, pili chama tawala huwa na mtindo wa kuwatumia makada wake waliohamia upinzani na mtu anaweza kuhama chama kwa ajili ya kwenda kukijenga chama kingine.

Kama Sumaye lengo lake ni kuijenga CHADEMA hatua aliyochukua ni sahihi,” alisema.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM), Richard Mbunda alisema: “Anaonekana siyo mtu wa kutaka masilahi. Wakati wa kampeni alisema anataka kujenga upinzani, alichokiamua sasa ni wazi anataka kuwaonyesha Watanzania kuwa anaishi katika maneno yake.”
Wasomi feki ndo wanamfagilia little achiever mwenzao.
Waziri Mkuu mstaafu anagombania cheo cha mitaani!
Alishindwa kuongoza taifa na hiyo mitaa nayo takuwa fedheha kwake.
 
Tehetehee TE="YEHODAYA, post: 16865201, member: 315573"]Nchi hii tuna wasomi koko wa kutisha.Msomi huenda na ushahidi wa takwimu kabla ya kuongea.Msomi haongei kama mlevi tu wa kiroba bila takwimu.

Sumaye mkoa wa Pwani hajaingiza hata mwanachama mmoja mpya wa CHADEMA !!!! wanaoitwa wasomi tayari wameshaibuka eti ooooh atasaidia kujenga chama kuanzia chini!!! Kazi ipo kuwa na wasomi wa aina hii ni aibu.Ningekuwa nasoma kozi wanayofundishha nigehama na kubadilisha kozi.[/QUOTE]
Tehetehee.. Naona povu miingii.. una angalau degree moja lakini?
 
Sumaye kschsnanyikiwa kwa kweli, na namhurumia.
Ila kuna precedence inajitokeza hapa.
Mawaziri wakuu wastaafu wawili wamehamia CHADEMA, na wote ni wa kutoka sehemu ileee!!!
 
Nchi hii tuna wasomi koko wa kutisha.Msomi huenda na ushahidi wa takwimu kabla ya kuongea.Msomi haongei kama mlevi tu wa kiroba bila takwimu.

Sumaye mkoa wa Pwani hajaingiza hata mwanachama mmoja mpya wa CHADEMA !!!! wanaoitwa wasomi tayari wameshaibuka eti ooooh atasaidia kujenga chama kuanzia chini!!! Kazi ipo kuwa na wasomi wa aina hii ni aibu.Ningekuwa nasoma kozi wanayofundishha nigehama na kubadilisha kozi.
Kwani yeye na mkewe sio wanachama? Na wewe kama sio msomi koko ungeweza kuelewa hilo kwa urahisi tu?
 
Sumaye kschsnanyikiwa kwa kweli, na namhurumia.
Ila kuna precedence inajitokeza hapa.
Mawaziri wakuu wastaafu wawili wamehamia CHADEMA, na wote ni wa kutoka sehemu ileee!!!
Mbona Cheyo amefungamana na serikali inayoongozwa na mtu wa kwao na watanzania wanaona haina tatizo! Usituletee ubaguzi wakati watanzania hatutaki siasa zitufikishe huko!
 
Sumaye anavizia uenyekiti wa chama and nothing else! Hii yaweza kuwa ni mpango wa muda mrefu au mfupi pia. Hongera zake kwa kujjdemote.
 
Back
Top Bottom