Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Wasomi waiponda PAC, wataka tume huru

Ingilia kati suala hili mheshimiwa rais kulinda taasis ya rais

Nadhani hata kuchaguliwa kusomea kozi za mafuta ni favour walipewa na huyo wanayemtetea,watoe majina yao na kozi wanazosoma ili tuangalie kama walikidhi vigezo vya kupewa hizo scholarship.Wanawakilisha wasomi wangapi?wana uhusiano gani na maesrow?
 
Ningekuwa rais muhongo na maswi wangekuwa ndani muda huu na sethi angeshanyongwa wanahonga vijana pesa za pombe na condom kutoa matamko ya kipuuzi kama haya; hii inayotumika ni pesa ya umma.

haaaahaaaaa urais hauji kwa kujikwaaa ndio maana haujawa rais mkuu
 
....Mpaka muandaliwe ndiyo muongee? Elimu mliyopata haijawakomboa kifikra. Nyie siyo msaada kwa waTanzania.
 
Tunawaahidi watanzania wote na watetezi wa Rasilimali, kwamba tutazunguka nchi nzima kuhamasisha watanzania kusimamia ukweli, kutetea haki, wajibu na kuhakikisha hakuna mtanzania mtetezi wa Rasilimali ataonewa na wanasiasa wasaka tonge kama ilivyotaka kutokea hivi karibuni.

Tunaanzisha sasa hati ya maombi maalum kwa Raais (Petition Form) itakayosainiwa na mamilioni ya watanzania wanaoitakia mema nchi yetu kumuomba Rias apuuze maazimio haya ya mabepari, wahujumu uchumi na wasaka tonge walioungana na wasaka Urais.

Mungu ibariki Tanzania
Mungu wabariki wazalendo na watetezi wa kweli wa Rasilimali.
 
Zitto arudishe mgao alopewa na Mengi na Mkono wa kumng'oa Muhongo na Maswi maana Rais kishagundua huo mchezo mchafu,, usiporudisha hela zao jiandae kudaiwa hats kwa gharama ya juu sana
 
Muhongo kwa sababau tu tangu kuingia kwake ofisini ameziba mianya ya uchotwaji mkubwa wa pesa za watanzania kupitia sekta ya madini, na sasa mabepari wameungana na wabunge wenye husda kupambana dhidi ya kweli na haki anayosimamia Muhongo.

Kumpoteza Muhongo kwa sababu tu yeye na Katibu mkuu wake Eliakim Maswi, hawana mawasiliano mazuri na Mwenyekiti wa PAC Zitto Kabwe (Hii inatokana na kitendo chao kudhibiti udalali wa Rasilimali).
 
wanazuoni majina yenu ama uongozi wenu
wanazuoni mmesajiliwa huko ughaibuni au tz
kwaiyo mlisomea madini mikataba sheri kodi upelelezi ubunge udhibiti wa fedha au?
 
Eti wasomi!! my foot.. haya yote kayasababisha jk ..angekuwa ashafanya maamuzi muda mrefu ..hawa wahuni wasinge ibuka na upuuzi Kama huu.
 
Hao misukuke issue ya katiba pendekezi hawakuona mapungufu wanaona mapungufu kwenye hii issue inayomgusa mtu au watu wawili kuliko katiba inayowagusa watanzania wote kwa miongo kadhaa ijayo? Hii elimu ya siku hizi balaa sana.
 
njaa mbaya sana nyinyi ni wanzuoni gani kwa sifa zipi na kwa sura gani achane kutumia jina la wanazuoni vibaya kwa njaa zenu mbaya...hakuna mwanazuoni anayeweza kuwazia ujinga huu..
 
hao misukuke issue ya katiba pendekezi hawakuona mapungufu wanaona mapungufu kwenye hii issue inayomgusa mtu au watu wawili kuliko katiba inayowagusa watanzania wote kwa miongo kadhaa ijayo? Hii elimu ta siku hii balaa sana.

unajua imefika wakati tutambue kuwa nchi hii ni ya demokrasia na kila mtu ana haki ya kuongea na kutoa mawazo yake kadiri anavyoona inafaa bila kudhuru wengine, acheni kukejeli watu na maoni yao, au unadhani wakiongea kuhusu katiba watatoa mawazo yanayokufurahisha wewe
 
Back
Top Bottom