Wasomi wa IT ni watulivu kwenye ndoa.

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,278
6,673
Habari zenu wana JF, Ni mwezi mmoja sasa umepita binti mmoja jirani yangu amegoma kuolewa na mwanaume ambaye ni Dereva na kutoa maelezo yafuatayo.

  • .Hataki mwanaume Dereva
  • Askari aina zote

Eti anadai kuwa aina hizo za wanaume huwa wanatoka sana nje ya ndoa. Alichoniacha hoi ni pale alipodai kuwa Wasomi wa IT ndio wanaoongoza kwa utulivu kwenye ndoa. Nilipomuuliza sababu hakunieleza hivi hili nalo ni kweli kuwa wasomi wa IT ndiyo watulivu zaidi? kama ni kweli ni kwanini? Na kuna ukweli kuwa baadhi ya fani zinaongoza kwa kuwa na mafataki?
 
Kwasababu kutwa killa siku macho pima wamedokolea ma computer akiamka kaenda kujisaidia karudi kwenye screen ya computer. Kama anafikiri ni watulivu kwamba wana mda wa kupetpet mpenzi imekula kwake, mimi ni mtu wa IT.
 
  • Thanks
Reactions: Mbu

...Rubani/Air Crews mnh!...

Jamaa wa IT wanatumia muda mwingi ku "blog" hata usiku kucha majumbani kwao!
JF wamo kibao, ha ha ha ...LOL!
 
Kwasababu kutwa killa siku macho pima wamedokolea ma computer akiamka kaenda kujisaidia karudi kwenye screen ya computer. Kama anafikiri ni watulivu kwamba wana mda wa kupetpet mpenzi imekula kwake, mimi ni mtu wa IT.

...ha ha ha, there you go!
 
Si kweli kama ni kutulia zaidi Waalimu tunaongoza na mafataki wengi ni wasanii hasa wa filamu.
 
Me pia niko kwenye IT,kutulia sawa ila anaweza shangaa hata mda wa kupata game sometimes hamna,....computer ni mke mwenza wake kama hajui
 
Mmmmhhhbhh
Hivi kumbe utulivu kwenye ndoa
Inatokana na kazi ya mtu ae mmhhh

Yap sasa hata ma porn star watasema ndoa
zao zina utulivu ......
 
Wanaboa muda wote kwenye computer kama sio hivyo ni blackberry yake halafu ikitokea story fulani tu tayari anaijua na anavyoiongelea utadhani alikuwa kwenye tukio kumbe kasoma kwenye blogs au web lol nawajua hawa kna ndugu yangu kila siku analalamika, halafu hawajui kucare kabisa sababu ya ubize wao na pc
 
Nina ndugu yangu mtu wa IT NA ni askari vile vile je yeye kwa mujibu wa maelezo hapo juu yuko kundi gani?
 
mmmh!! haya tena makubwa! hongereni wenye waume wa IT na wake wa IT kumbe mmetulia ndoani.......ila mimi bado naamini utulivu wa mtu au tabia njema ya mtu inatokana na uamuzi wake binafsi + ufahamu+ hofu ya Mungu ndani ya moyo wake+ kupenda kufanya kile anachopenda yeye kufanyiwa. LAKIN eti ukiwa mtu wa IT basi moja kwa moja wewe ni mtulivu????!!!!.HONGERENI SANA WATU WA IT KAMA KWELI UPO HIVI 100%.
 
Yap Bana watu wa IT ni watulivu ila ajiandae pia kukosa haki yake kwan ni watu walio busy na computer mda mwingi, kitu cha kawaida kushutuka kumekucha hajalala atayaweza haya.
 
sasa huyo mdada anaejifanya kuchagua, anauzoefu gani na hao madreva na wajeda??, au kaambiwa tu na kaskia kama anavyosikia kikombe cha babu kuwa kinaponya, msiniulize babu kaingiaje hapa, natoa mfano tu..
akili za kuambiwa achanganye na zake...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom