Wasomi wa Biashara CBE Dodoma Campus wampa Certificate Maua Sama.

Wasomi wa Biashara CBE Dodoma Campus wampa Certificate Maua Sama.

mchumihalisi

Member
Joined
Oct 8, 2015
Posts
28
Reaction score
98
9a103251-11a2-4bce-89a1-a0b739a041d9.jpg

Ni dhahiri sasa kwamba Sanaa ya Taifa letu inazidi kukua siku hadi siku na baadhi ya Watu waliokua wanadhani hii sanaa uhuni kama sio kubadilika basi hawapo tena.

Kwa hivi sasa imekua kawaida Waimbaji mbalimbali wa 'Bongo Fleva' wakialikwa sehemu nyeti na kupewa upendeleo wa hali ya juu jambo ambalo kama sio nadra basi ilikua haiwezekani kabisa kwa nyakati zilizopita.

Leo nimetazama XXL iliyokua ikifanya kipindi chake LIVE kutokea Chuo cha CBE Dodoma mwishoni mbele ya Mbunge wa Dodoma nimeona Vijana wasomi na Viongozi wa CBE wakimkabidhi tuzo Maua sama kwa kubadilisha kipaji chake kuwa 'Biashara' na kukifanya bila kutafuta Kiki wala tuhuma ili kupush muziki wake.

Hongera sana Maua, endelea kukazia hapo hapo tunaamini utaendelea kuwa 'role model' Bora wa Vizazi vijavyo. Hongera pia kwa wimbo wako wa Zai kuwa kwenye Jiwe la Wiki ambalo mara nyingi sio kila nyimbo inapata hio nafasi.

Aminia Maua mtoto wa Sama
 
Back
Top Bottom