Wasomi ni muhimu sana CCM

fisi 2

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
3,273
4,626
Tumeona jinsi CCM ilivyoteswa na wasomi wa upinzani kiasi cha kutumia nguvu kuzima hoja zao. Angalizo sasa Chama cha Mapinduzi kitumie wasomi walioomba nafasi za Ubunge ili kujenga base yenye nguvu hata kimataifa.

Tumeona pia Rais anavyoteseka kupata mawaziri mpaka analazimika kula matapishi yake kwa kurecycle wale aliowatumbua. Kuiwepo kwa wagombea wengi ma hasa wasomi wenye sifa ni fursa sasa kwa Chama na Taifa kupata viongozi imara.

Angalizo Chama kiache kuwavua akili wasomi wake. CV za wasomi zitangulie mbele. CCM.
 
utashangaa vyeti fake Bashite anakuwa mbunge PhD holder Ndugulile anawekwa kapuni...halafu unategemea uchumi wa viwanda wa sayansi na teknolojia.
 
Hakunaga msomi ccm. Wan amakaratasi tu. Makaratasi yao hayajawahi kulataga impact yoyote kwa jamii mahalia
 
Kama ni hivo kuwa upinzani kuna wasomi wengi ungeshauri ccm ipumuzike iwapishe wapinzani, au ni wale wasomi uchwara mlioko ccm
 
Mkuu hebu tengua upesi hii Kauli kwani usidhani kila mwana CCM ni ' Popoma / Pumbavu ' kama hao uliobahatika kuwa nao au hata kuwajua pia.
 
Hata ukiwa msomi chaguzi ni mbili utumie usomi wako ufe njaa au utii maagizo usife njaa.Ukileta usomi imekula kwake.Check Ndungulile alitumbuliwa sababu ya kutumia usomi wake.
Tii maagizo,sifia mchana, asubui na jioni kila upatapo camera, wakomoe, washughulikiwe wadhalilishe waumize wapinzani hii ni Kinga tosha ya utumbuzi na teuzi.
 
Kama Profesa aliyeko CCM anazidiwa hoja na darasa la NNE aliyeko CCK, ni bora ungeanza kuchunguza kwa nini ukiingia CCM tu ghafla unakuwa Zuzu.
 
Kama Profesa aliyeko CCM anazidiwa hoja na darasa la NNE aliyeko CCK, ni bora ungeanza kuchunguza kwa nini ukiingia CCM tu ghafla unakuwa Zuzu.
Mdee pekee anaweza akaburuza ccm wote kwa hoja za uchumi na wasipate jibu wakaishia muongozo muongozo na personal attack ili kupoteza time bungeni rejea uchangiaji wa bajeti iliyopita ya Mipango bungeni,thus bossi wao hataki kabisa bungelive kuwafichia aibu.
 
Baada ya chuo cha siasa cha ccm kufa tegemeo pekee ni kuazima toka upinzani ndo chuo pekee cha siasa kilichobaki,japo nao wakiingia tu getini akili ukabidhi kwa mmiliki wa chama,kitachotembea ni maagizo na kudumisha fikra tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom