Wasomi mmemsikia Edward Lowassa?

Wasomi mmemsikia Edward Lowassa?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Kile kilio cha siku nyingi cha maumivu ya mkopo wa elimu ya juu kinakaribia kupatiwa jibu. Mgombea wa Urais wa CHADEMA/UKAWA Edward Lowassa ameahidi kuwasamehe wale wote waliokopeshwa na kodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB). Lowassa anamaanisha kuwa wanaodaiwa hawatalipa tena na itakuwa ni kama wamesomeshwa bure tu na Serikali yao.

Wakati huohuo, Lowassa anaendelea kusisitiza kuwa elimu ya chuo kikuu itakuwa bure. Wasomi wa wakati wa nyuma na wale wa sasa, mnataka nini tena? Lowassa, kutokana na ahadi zake za kiuchaguzi, anatamani kuona elimu inakuwa bure na hata wale waliokopeshwa wakijisikia kuwa wamesoma bure. Lengo kuu ni kutoa elimu ya bure na bora kwa maendeleo ya Tanzania yetu.

Mtampa kura wasomi wa Tanzania? Wale waliolipa hadi kumaliza mkopo, Serikali itawarudishia fedha zao? Tutege masikio tena kumsikia Lowassa atalisemeaje hili.
 
Hello Mwanamabadiliko Mwenzangu, Tarehe 25 Octoba ndo siku ya kulikomboa Taifa letu toka mikononi mwa maccm. WAPIGIE SIMU BABU NA BIBI, MASHANGAZI NA WAJOMBA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI wa Vijijini na Mijini waambie juu ya TAARIFA za UKOMBOZI HUU.
Wampigie KURA ✌EDWARD LOWASSA na WABUNGE na MADIWANI wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD tu.
 
Asante rais wa awamu ya tano.Bodi ya mikopo ni wizi mtupu watafute kazi ya kufanya baada ya kuapishwa
 
Ahsante mheshimiwa kwa kuahidi kufuta deni...
Haya wasomi mwenye macho haambiwi tazama

Good news. Inashangaza sn nchi zinazotukopesha mara kibao zinatusamehe madeni lkn hatuoni tija ya hiyo misamaha. Kwa nn tusishangilie kwa lowasa kugusa maisha ya mtu mmoja mmoja badala ya chama cha majambazi????
HAPA NI MABADIRIKO TU
 
Naomba kumuahidi lowasa Mimi sio mwanasiasa ila kura ya mama yangu mke wangu wadogo zangu ninaosomesha na ndugu zangu nitapambana kufa na kupona wampe kura maana baada ya hapo hera nayokatwa nitakuwa nawatumia kule kijijini . Kwa mara ya kwanza naona umhimu wa uchaguzi tangu nizaliwe. Mungu mubariki Lowasa maana ananifanya kwa mara ya kwanza nipige kura ili nisamehewe 10,000,000. sina lingine zaid
 
Lowassa hizo ni sound wala so kweli magufuli ndo rais
 
Hello Mwanamabadiliko Mwenzangu, Tarehe 25 Octoba ndo siku ya kulikomboa Taifa letu toka mikononi mwa maccm. WAPIGIE SIMU BABU NA BIBI, MASHANGAZI NA WAJOMBA, NDUGU JAMAA NA MARAFIKI wa Vijijini na Mijini waambie juu ya TAARIFA za UKOMBOZI HUU.
Wampigie KURA ✌EDWARD LOWASSA na WABUNGE na MADIWANI wa vyama vya CHADEMA, CUF, NCCR MAGEUZI na NLD tu.

Babu na bibi hawajui kusoma. Nimewaambia ukiona m2 mwenye mvi weka tiki hapo hapo. Huyo ndo 'mwalimu' wetu wa leo
 
Good news. Inashangaza sn nchi zinazotukopesha mara kibao zinatusamehe madeni lkn hatuoni tija ya hiyo misamaha. Kwa nn tusishangilie kwa lowasa kugusa maisha ya mtu mmoja mmoja badala ya chama cha majambazi????
HAPA NI MABADIRIKO TU

Lowasa anatosha
 
Naomba kumuahidi lowasa Mimi sio mwanasiasa ila kura ya mama yangu mke wangu wadogo zangu ninaosomesha na ndugu zangu nitapambana kufa na kupona wampe kura maana baada ya hapo hera nayokatwa nitakuwa nawatumia kule kijijini . Kwa mara ya kwanza naona umhimu wa uchaguzi tangu nizaliwe. Mungu mubariki Lowasa maana ananifanya kwa mara ya kwanza nipige kura ili nisamehewe 10,000,000. sina lingine zaid

Mie bodi wananidai wataanza kunikata wakati wowote. Njoo lowassa uniondolee hili deni. Alaaa.
 
Huyu ndiye aina ya Rais aliyekuwa anahitajika ktk nchi hii toka miaka 20 iliyopita,ungekuta leo hii haya tunayoyaona ni historia,Lowasa ni mpango wa Mungu tusifanye makosa watanzania wenzangu
 
Back
Top Bottom