Wasomi Mlimani kizimbani kwa wizi NMB | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wasomi Mlimani kizimbani kwa wizi NMB

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 27, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Wasomi Mlimani kizimbani kwa wizi NMB
  • Yaelezwa walitumia simu za mkononi kuibia wateja

  na Julieth Mkireri, Kibaha


  [​IMG] UMEIBUKA mtindo mpya wa wizi wa fedha katika Benki ya NMB kwa kutumia teknolojia ya simu za mkononi, ambapo wanafunzi watano wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Pwani kwa tuhuma za wizi wa sh 20,280,000 unaodaiwa kufanywa kwa njia hiyo.
  Wizi huo unadaiwa kufanywa na wanafunzi hao Desemba mwaka jana kwa mbinu mpya ya kutumia simu zao za mikononi katika kuiba fedha za wateja wa benki hiyo ya wananchi ambayo inatumiwa na wafanyakazi wengi wa serikali.
  Wanafunzi hao ambao walifikishwa mahakamani jana mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mkoa, Nsekela Mwaiseje, kujibu tuhuma hizo wametajwa kuwa ni Boniface Kyaga (23) anayedaiwa kuiba sh 9,030,000 na David Mwani sh 4,900,000.
  Wengine ni Deodatus Buyokwe anayedaiwa kuiba kiasi cha sh milioni tano, Idota Makena, anayedaiwa kushiriki zoezi hilo na kujipatia sh laki tisa na Gloria Joseph anayetuhumiwa kuiba sh 450,000 kwa kutumia njia hiyo hiyo ya simu ya mkononi.
  Akielezea kuhusu tukio hilo la wizi, Mwendesha Mashitaka, Mrakibu wa Polisi Hatib, aliweka bayana mbele ya Hakimu Mwaiseje kuwa wanafunzi hao wa Chuo Kikuu Mlimani waliiba fedha hizo zote zikiwa za wateja wawili wa benki hiyo ya NMB Tawi la Rufiji, mkoani Pwani.
  Washitakiwa wote watano walikana mashitaka hayo na kesi yao imetajwa kusikilizwa tena Februari 8, mwaka huu.
  Idota Makena na Gloria Joseph waliachiliwa baada ya kudhaminiwa na wakazi wawili wa Kibaha kwa dhamana ya sh milioni moja kila mmoja, wakati wanafunzi wengine watatu waliobaki walishindwa kutimiza masharti ya dhamana, hivyo kuendelea kubaki rumande.
  Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu madai ya wateja wengine 20 wa benki hiyo Tawi la Kibaha, wanaodaiwa kuibiwa kwa njia hiyo, akiwamo mwandishi wa Radio One Mkoa wa Pwani, Ayoub Mtawazo.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi UDSM kortini kwa wizi wakitumia mtandao Wednesday, 26 January 2011 20:16

  Julieth Ngarabali, Pwani


  WANAFUNZI watano wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Pwani, kujibu tuhuma za wizi wa Sh20 milioni wanazodaiwa kuzichota kimafia katika Benki ya Makabwela (NMB).

  Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa fedha hiyo iliibwa kwa nyakati tofauti kupitia mfumo wa simu za mkononi, kuanzia mwaka jana katika tawi la Kibiti wilayani Rufiji.

  Mrakibu wa Polisi, Hatibu aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Boniface Elias, David Ezekiel Mwani, Deodatus Edward Buyokwe, Dota Makena na Gloria Joseph Simfukwe.

  Mrakibu huyo wa polisi alifafanua kuwa Boniface Elias aliiba Sh9,030,000, David Ezekiel Mwani Sh 4,900,000, Deodatus Edward Buyokwe Sh 5,000,000, Idota Makena Sh 900,000 na Gloria Joseph Simfukwe Sh450,000.

  Mrakibu huyo wa polisi, alidai watuhumiwa wote ni wanafunzi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam sehemu ya Mlimani.

  Alidai fedha hiyo ni mali ya wateja wawili wa NMB; William Valentino na Salim Bakari.

  Mwendesha mashitaka huyo alidai wanafunzi hao wanatuhumiwa kuiba fedha hizo kwa kutumia njia ya simu za mkononi ya kampuni ya Air Tel zamani ikiitwa Zain na kwamba kila mmoja aliiba kiasi tofauti na mwenzake.

  Washitakiwa hao wote walikana mashitaka hayo na kesi yao inatarajiwa kutajwa tena Februari 8, mwaka huu.

  Hata hivyo watuhumiwa wawili Gloria na Idota wapo nje baada ya kupata dhamana ya milioni moja kila mmoja na wadhamini wawili kila mmoja ambao wote ni wakazi wa Wilaya ya Kibaha na wezao watatu walipelekwa rumande kutokana na kukosa dhamana na wadhamini kama wenzao.

  Wakati huo huo Jeshi la Polisi mkoani humu linaendelea na uchunguzi wa madai ya wateja wengine zaidi ya 20 wa benki hiyo Tawi la Kibaha ambao nao wanalalamika kuibiwa fedha katika akaunti zao.

  Wakati polisi ikiahidi kufuatilia madai hayo,wananchi waliozungumza na gazeti hili jana wengi wao wakiwa ni wateja wa NMB waliilalamikia kampuni ya simu za mkononi kwa kuendesha huduma za kibenki huku wakiwa wagumu wa kutoa ushirikiano pindi inapotokea malalamiko ya wizi kama huo

  Mmoja wa wateja hao Ayoub Mtawazo alisema alishatoa taarifa NMB kuhusu kuibiwa fedha zake na uongozi wa NMB ulifuatilia suala hilo ,lakini uongozi wa kampuni ya simu unadaiwa haukutoa ushirikiano wa kutosha katika kuwabaini wahusika

  "Huu wizi upo sana wateja tunaibiwa kidogo kidogo,lakini cha kusikitisha ni kampuni ya simu za mkononi ambayo viongozi wake wanadai hawawezi kutoa majina ama picha za watu
  waliohusika na wizi wa fedha zangu hadi mwanasheria wao aje kwani muda huu yupo likizo hivyo kutoa mwanya wa kupoteza ushahidi ama wahusika"alisema Mtawazo.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,208
  Likes Received: 414,656
  Trophy Points: 280
  Haya wasomi wetu hilo ndilo soko la ajira binafsi?
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Duh, kwa hiyo its official sisi wateja wa NMB ni makabwela?? dah, powa tu lakini..kitaeleweka mbele kwa mbele.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Nways nahitaji shule hapa, wanaibajeibaje? huenda hata akina yakhe tukajihami.
   
Loading...