Bornvilla
JF-Expert Member
- Feb 17, 2011
- 924
- 271
Wataalam wetu Tanzania ni fake jamani? Mbona umeme imekuwa balaa? Sasa ngoja niulize swali,je ni lazima umeme upatikane kwenye mabwawa na maporomoko? Mbona tuna maziwa yenye maji mengi na hayategemei mvua? Tuna Ziwa Victoria,Tanganyika,Nyasa,Eyasi,Natron,Manyara na Rukwa! Haya yooote ni bure,yaani tumeshindwa kuyatumia kupata umeme wa uhakika? Wataalam na mainjinia kazi zao ni zipi? Wanaisaidiaje nchi? Nakumbuka kuna mbunge mmoja aliuliza bungeni juu ya kutumia bahari kwa kuyabadilisha maji kuwa baridi kutoka chumvi ili yatumeke kuzalisha umeme,jibu kutoka kwa serikali likawa mradi kama huu unagharama kubwa sana! Ha! Mbona pesa nyingi zinapotea kwenye miradi ya ajabu tu na tena mingine ya mifukoni? Yaani mnashindwa kugharamika ili nchi iondoke gizani? Jamani! Hata hapa napost kwa simu yangu umeme hakuna yaani ni giza totoro.Wataalam,wasomi kwa namna hii tunaelekea wapi? Miaka 50 gizani ndio tunajivunia?